Kauli ya Waziri Mkuu kutilia shaka barakoa za kisasa na kutaka watu wajishonee matambara na kuyavaa usoni haiwezi kuachwa bila kujadiliwa

Before ilikuwa marufuku kusema Tz pana corona. ( tuliamini lakini wamekubali corona ipo,, pengine wametugeuka)
Now ni marufuku kusema chanjo ya ulaya inafaa.( tutaamini ,wenyewe watachanja na kutuacha tunashasumbuliwa na coeona.
 
Kuna utata kidogo kwenye maneno yanayi semwa na baadhi ya viongozi, eti wananchi vaeni barakoa lakini lazima mjiridhishe zimetoka wapi na usalama wake..

Na haya maneno ya wasiwasi wa viwango vya barakoa yametolewa na kiongozi senior kabisa (top 3 ).

Najiuliza , ina maana huyu kiongozi

1. Hajui kazi za TBS.. kwanini badala ya kuwaambia wananchi akaagiza TBS wafanye kazi yao.

2. Je hawajui kwamba wananchi tunajua kwamba bidhaa zote zinalindwa na sheria inayosimamia TBS?

Hakuna sababu ya viongozi wa siasa kuanza kututisha wananchi kwamba baadhi ya bidhaa hazina ubora wakati tumewaamini kuunda vyombo vya kusimamia ubora..

Tunahitaji kusikia TBS wamechoma makontena mangapi ya barakoa?

Wananchi tunaamini barakoa kama bidhaa nyingine ni salaam kwa sababu wale tulio wapa kazi ya kusimamia ubora wanafanya kazi yao.
 
Wanataka kupotosha kuwa barakoa toka nje ndio zimeleta corona hii second wave. Nadhani hawakukumbuka kuwa kwenye huo upotoshaji wao wanaotaka kuufanya, TBS wana wajibu huo. Haya ndio mambo yanayozidi kuchochea upatikanaji wa katiba mpya, kwani inaonekana kabisa mtu mmoja anapokuwa na maamuzi yote ya nchi nini kinaweza kutokea.
 
Upo sahihi, na huyo mtu mmoja kwanini asiache kuwalipa mishahara kama TBS wameshindwa kutambua barakoa fake ?
 
Ni propaganda za kipuuzi tu za viongozi wa hovyohovyo wa awamu ya tano.

Ukienda pale TBS ubungo au pale TMDA river side, utakuta wafanyakazi wamevaa barakoa hizo za kutoka nje.

Hata hao viongozi wa hovyohovyo kwenye maofisi yao wafanyakazi wanavaa hizo za kutoka nje.

Lakini wakiwa majukwaani ni kama kuna pepo la mauaji limewaingia.
 
Nadhani Barakoa ni ''medical device'' kwahiyo wanaohusika nayo ni TMDA.
Eneo la TBS weka TMDA, and you are very right in your entire argument.
Siasa inapovuka mipaka ndio tunafikia hatua hizi...
 
Hii nchi ina mambo ya ajabu sana!!
 
Tu nasubiri pigo kuu tukae sawa maana ujinga umetamalaki
 
Huyo anarudia tu maneno ya boss wake hebu tujiulize hizi dawa za mahospitali asilimia kubwa znatoka wap????
 
Baada ya kushindwa kwa hoja msala tunahamishia kwenye barakoa. Wanataka kusema tulizovaa mwaka jana ndo zimeibua hili Corona la sasa?
 
 
Unaona kabisa mtu anaongea asichokiamini na wakati huo huo ana ukweli anaoshindwa kuutoa. Hiyo ndio inaitwa uwajibikaji wa pamoja. Asante JK, akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…