Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Waziri wa Mawasiliano, Nae Nnauye ametoa kauli ambayo kwangu naona inashida aidha kwake kwenye kuitambua mawasiliano au digitali kwa ujumla. Bajeti ya Wizara ya mawasiliano ya mwaka wa fedha 2024/25 imetaja “Mapinduzi ya Kidijitali” mara kadhaa. Sera na mipango mingi ya wizara inataja Kwenda kuwafanya watu wawe connected wapate access muda wote.
Kauli ya Waziri kuona kuwa watu kuwa connected ni shida, inaonesha hana ufahamu wa jinsi watu wanatengeneza fedha online, na inakuwa kinyume na mapinduzi ya kidigitali ambayo bajeti imeyataja. Kauli hii inaashiria kuna kiama kwa watumiaji wa mtandao kwa kuwa tu Waziri mwenye dhamana anaona kuna shida.
Ni zaidi ya mara moja wabunge wametaka kuwe na tozo kwa laini za simu. Na ni muda mfupi uliopita ambapo tumepigwa gharama kubwa kwenye vifurushi vya internet. Matumizi ya internet yako chini sana kwa wastani wa GB 2 kwa mwezi kwa watu wenye smartphone, maana yake kuna baadhi ya watu wenye simu hawanunui vifurushi.
Mbali na hayo yote Waziri anaona ni shida watu kuwa online, naona kama wanahisi watu wapo online kuwakosoa wao tu, ilhali watu wako na mishe nyingi wanafanya.
Nadhani Waziri inabidi aoneshe kwa nia kuwa anatamani kuona watu wako online badala ya maneno yake ambayo yako kinyume na sera hata bajeti aliyoisoma mwenyewe bungeni