Kauli za Bashiru na Tulia kuwa CCM itatumia dola kubaki madarakani zimefafanuliwa na Humphrey Polepole

Kauli za Bashiru na Tulia kuwa CCM itatumia dola kubaki madarakani zimefafanuliwa na Humphrey Polepole

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,483
Reaction score
40,130
Great Thinkers.

Leo tunashuhudia Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA akishtakiwa kwa kosa asilotenda la Uhaini. Sote yaani sisi raia na mpaka wanaomshtaki wanajua Lisu hajatenda wala kuthubutu kuwa mhaini.

Bila kuzunguka sana, naenda kwenye hoja yangu.

Kwa nyakati tofauti, viongozi waandamizi wa taifa yaani Spika wa Bunge na Bashuri Ally Kakurwa ambaye wakati huo alikuwa Katibu Mkuu wa CCM walisema na kunukuliwa na vyombo vya habari kwamba, CCM ITATUMIA DOLA (Vyombo) KUENDELEA KUBAKIA MADARAKANI.



Mwezi Juni 2025, Spika Mstaafu bi Amne Semamba Makinda alinukuliwa akimwambafai kwamba wapiga kura hata wasipoipigia CCM kura, ndiyo itakayounda serikali watake wasitake.

Kauli hiI za viongozi wakubwa, zimetolewa mbele ya hadhira. Chama cha Mapinduzi hakijakanusha kauli hizo. Na tumeona makada wa CCM wakijinadi kuwadhuru hata kusema wanaweza kutoa uhai wa watakaoonekana kupinga wizi wa kura vituoni. Tumesikia pia kauli za IGP akiwataka Watanzania kukimbia nchi yao akidai wanaoleta vurugu watafute nchi ya kwenda. ZPC Muliro amesema kuwa atakayeandamana tarehe 29 Oktoba anajitakia kufa.

Kauli hizi, zimeweza kuthibitisha mchezo mchafu unaoandaliwa na CCM ikishirikiana na vyombo vya dola kupoka ama kupora haki za raia kwenye mchakato wa demokrasia hususani uhuru wa Kuchagua na kuchaguliwa. Kuna mambo kadhaa ya kuangazia ambayo yanatokana na kumuelewa Humphrey Polepole
  1. CCM imebebwa na vyombo vya dola hususan Polisi ambapo wamekuwa wakishiriki kukandamiza upinzani kwenye kila tukio la kisiasa na uchaguzi. Vifo vinavyohusiana na siasa vimeongezeka na watuhumiwa wakubwa wakiwa ni vyombo vya dola.
  2. Polepole ametoa ushuhuda ushiriki wake kwenye katika kuunganisha CCM na mifumo ya usajili wa raia yaani BVR na NIDA ili kufanikisha wizi wa kura. Hivyo inadhihirika kwamba hakujawahj kuwa na Uchaguzi Mkuu huru na haki nchini kwa sababu dola imeendeleza ndoa isiyo na afya baina yake na CCM
  3. CCM imejipambanua kuwa zoezi la Uchaguzi Mkuu na Chaguzi za TAMISEMI ni kiinimacho dhidi ya Uhuru na Ustawi wa Tanzania. Hivyo CCM kwa kushirikiana na dola wamepindua matokeo ya kura za wananchi. Mfano mzuri ni kwamba Kura za Urais wa JMT 2020 mpaka leo hayajawekwa hafharani mpaka leo. Tunaweza kusadiki kwamba sababu za kutoipa CCM ushindi na hivyo matokeo kufichwa.
  4. Mtandao unaodadavuliwa na Polepole umeonesha kuwa umeimiliki serikali, hivyo hakuna uhalali kwa serikali kuendelea kumilikiwa na kikundi cha watu badala ya kufuata Katiba, Sheria na maslahi ya Watanzania.
  5. Hata ndani ya CCM wanaibiana kura na hakuna wa kukemea. Viongozi wabaopitishwa na CCM hawapatikani kwa njia halali




Kwa mazito tuliyoyasikia kwa Polepole, je ndugu msomaji, mwenye hila za kuleta mtafaruku Tanzania kati ya pande hizi ni nani?
  1. Lissu ambaye anapambana kutaka Haki za kila raia ziheshimiwe pamoja na Reforms ili kupata uchaguzi ulio huru na haki?
  2. CCM iliyoshirikiana na vyombo vya dola kuiba na kubaka chaguzi zote nchini?
JIbu unalo, tujadiliane kwa mustakabali wa Taifa l
 
Back
Top Bottom