Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 51,453
- 41,274
Sote ni mashahidi dhidi ya kuweweseka kwa chama cha demokrasia na maendeleo, chadema baada ya mwanachama wake na nguli wa siasa za Tanzania, senior politician Joseph Selasini Shao, kupendeza kuundwa kwa kamati ya uchunguzi, kuchunguza ufisadi wa heche ndani ya chadema ili kujiridhisha na kujua ukweli wa sakata hilo.
Lakini pia pendekezo lingine la Joseph Selasini Shao ambae anatarajiwa kua kaimu mwenyekiti wa chadema taifa baada ya mkutano wa baraza kuu la chadema taifa September 15.2026, lililoibua mchecheto na maoni mseto zaidi ndani ya chadema, huku baadhi ya wanachadema wakiunga mkono pendekezo hilo, wengine wakipinga na wengine wakimporomoshea matusi J.Selasini bila sababu yoyote ile , ni lile la kwamba,
Joseph Selasini Shao anapendekeza kua ni lazima chadema iingie kwenye maridhiano jambo ambalo limeipa kiwewe zaidi chadema haswa kwa wafuasi wake wafuata mkumbo na hata kufikia hatua, wafuasi hao wakipendekeza mwenyekiti huyo mtarajiwa wa chadema taifa afutwe uanachama wa chadema.
Soma pia Selasini aishauri CHADEMA kuhusu maridhiano, asema CHADEMA lazima imshirikishe Rais Samia
Kama mdau wa jukwaa hili la siasa, una maoni gani kuhusiana na haki na uhuru wa kutoa maoni kwa mwanachama wa chadema? Uhuru huo hua ni unafiki tu au ni uhuru na haki inayowahusu watu fulani maalumu tu ndani ya chadema?
Kulikoni wengine wakitoa maoni kuhusu kinachoendelea chadema hawafukuzwi, ila wengine wanafukuzwa chamani au uongozini kwa haraka sana?🐒
Mungu Ibariki Tanzania