Kauli za kisiasa zinavyoaribu elimu ya Tanzania

Kauli za kisiasa zinavyoaribu elimu ya Tanzania

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274
Mastaajabu hayajapoa katika sekta ya elimu nchini. Ukisahau walimu wa UPE miaka ile ya 1970 au wale wa ‘Voda Fasta miaka ya 2000’, utakutana na uamuzi wa kufuta masomo ya kilimo na michezo.

Hii ndiyo sekta ya elimu ambayo kwa miaka nenda rudi, baadhi ya maamuzi yanayofanywa na watendaji yamekuwa yakiwaacha midomo wazi Watanzania.

Kibaya zaidi ni maamuzi yanayoacha athari hasi katika sekta ya elimu. Fikiria kwa mfano, mwanafunzi wa shule ya msingi anayefundishwa na mhitimu wa elimu ya msingi.

Au Taifa limeathirika kwa kiwango gani kufuatia uamuzi wa masomo ya michezo na kilimo kufutwa wakati wa utawala wa Serikali ya awamu ya tatu?

Wakati kumbukumbu hiyo ikiwa haijapoa kwenye vichwa vya Watanzania, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, hivi karibuni ilisitisha utekelezaji wa mtalaa mpya wa kidato cha tano.

Uamuzi huo umekuja wakati tayari wanafunzi walisharipoti shuleni. Baadhi sasa watalazimika kubadili tahasusi ili kwenda sambamba na mahitaji ya mtalaa wa zamani unaoendelea kutumika.

Chanzo: Mwananchi

Soma Pia: Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda: Mitaala ya mipya ya Elimu imeanza Shule ya Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu
 
Wataalamu wa mwaswala haya wanasemajeee
 
Back
Top Bottom