Uchaguzi 2020 Kauli za Mgombea CCM Dkt. Magufuli kuhusu umwagaji wa damu zina maana gani?

Kama hakumwaga damu na hataki kumwaga damu wasiwasi unatoka wapi!?
 
Ukieleza kuwa kama tutashindwa, basi hatukubali tutawaeleza wanachama wetu waandamane mitaani! Huo si umwagaji wa damu kama ya akwilina?
Wapotoshaji kama ninyi mna sehemu yenu jehanamu. Sijui unaeneza huo upotoshaji kwa manufaa ya nani?
 
Da!!! kwa kauli hizi kweli huyu ni mtu wa kumchagua tena jamani ...

Sijawahi kuona Raisi wa ajabu duniani kama Maguli
 
Na mimi katika miaka 5 niliyotawala sikumwaga damu!
Duuh.. anamaanisha akina Ben Sa8, Azory Gwanda, Mawazo, Akwiline, wale mamia wa kwny viroba baharini na mto Ruvu, risasi kwa Lissu, nk, nk... huo siyo umwagaji damu?!
 
Msamehe bure kuna tatizo mahali,ukizoea kula nyama ya mtu huwezi kuacha
 
Jiwe mwisho wake umefika..NEC ,Police,Tiss wala jeshi hakuna wa kumsaidia
 
MKIRU, Ben Saanane, Azory, Akwilina, Maiti za coco beach kwenye sandaru, kutekwa, kupotezwa et etc etc. hasya yote hayakutokea huko nyuma isipokuwa kwako ....
Pengine kumwaga damu kuna tafsiri zaidi ya mbili
 
Mwacheni huyo muuaji amekwisha changanyikiwa. Kwa mtu mwenye akili nzuri ni vigumu kumuelewa kichaa. Damu ya watu inamfanya asiongee kitu chenye kueleweka.
 
First things first.

Mkapa kamwaga damu Zanzibar. Mpaka kaomba radhi kwenye kitabu chake.

Magufuli hajui hili?

Hajasoma hata dondoo za kitabu cha Mkapa?

Au anachochea fake news tu?
 
Hawa jamaa wanashangaza sana; sijawahi kuwasikia wakiongelea HAKI.... wao kila siku ni amani, amani

Hawa watu ni hatari mno, asanteni watanzania kwa kuwashitukia.....wameshaligawa hili taifa vipande vipande...

Say NO kwa hawa watu.
 
Unaposema ccm itatawala milele wakati inashindwa kila uchaguzi huo si umwagaji damu
 
Ukieleza kuwa kama tutashindwa, basi hatukubali tutawaeleza wanachama wetu waandamane mitaani! Huo si umwagaji wa damu kama ya akwilina?
Kuandamana ni kumwaga damu? Hili ni tatizo la kutawaliwa na chama kimoja kwa miaka mingi akili inachoka na kudumaa.,
 
Siku ukirudi kwenu ukiwakuta ndugu zako wamechinjwa na Machettes ujue ndiyo umwagaji wa damu huo na vita ya wenyewe kwa wenyewe imesha anza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…