Kauli za sasa za Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kuhusu CORONA zimeshaanza Kuzua 'taharuki' nchini, hivyo ama adhibitiwe au ajiuzuru upesi

Kwa mawazo yako unadhani waziri kakurupuka tu bila ya kupewa data na wataalamu?
Jaribuni kufuata maelekezo ya serikali na wataalam,tatizo nilioliona ni kwa nini waziri katoa tamko wakati wa pasaka!
Una hiyari kufuata wataalam, au akili yako
Kama utakumbuka Kwa zile wiki za mwanzo waziri ummy alitoa tamko watu tujikinge Kwa kuvaa barakoa(face masks) lkn baada ya siku 2 akaja mtaalamu WA afya akatuambia kuwa hizi barakoa zinasababisha maambukizi kama hatutavaa Kwa usahihi na pia ukishika mara Kwa mara ni rahisi kujiambikiza na mikwala kibao ikiwemo ya kunawa mikono Kwa sabuni..
Tuliambiwa tukinawa Tu haina shida ni rahisi kuuwa virui wala hakuna haja ya sanitizer..

Ukichunguza kauli hizo utaona kabisa jinsi gani serikali yetu haipo Makini juu ya ugonjwa huu maana kila mtu sikuhizi ni mtaalamu mpaka akina MAKONDA wametuambia tufanye biashara kama kawaida bila kujali chochote pia hata raisi alituambia tusitishwe na ugonjwa kila mtu ajiachie kufanya kazi yaani Kwa ufupi siasa imemeza tahadhari yenyewe
 
Kweli kabisa mkuu, wameficha sana mwisho wanaanza kuumbuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa kosa kuwacheka wakenya kwa jinsi walivyorespond wakati ugonjwa unaingia,Tz sio kisiwa ugonjwa huu tulijua unakuja na tayari ulishaleta taaruki nchi kubwa zilizoendelea. Prevention ndio ilikuwa silaha kubwa kwetu,ukizingatia huduma za afya bado ni changamoto kwenye nchi zetu za dunia ya tatu. Kiukweli tumechukua muda kurespond the way we were suppose to respond kwa maoni yangu. Ugonjwa huu ukishakuwa ndani kuudhibiti ni kazi kubwa kwani lazima uwadhibiti watu wasikutane na hata wakikutana basi wawe katika hali ya kuwa makini sana ili ugonjwa usitoke kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Since ugonjwa upo ndani ya jamii iliyozoea maisha ya kukutana katika kuendesha maisha yao ya kila siku changamoto kubwa iliyopo ni namna gani tutapigana vita hii ndani ya jamii yetu. Wenye imani za kidini tuendelee kuomba wakati huo tukiendelea kuchukua hatua ambazo tumeelekezwa na wataalamu wetu wa afya.
 
Unnecessary dramatization. Waziri amezungumza ukweli hata kama amechelewa,sasa ajiuzulu au kudhibitiwa kwa lipi?
Kudhibiti Corona inahitaji open government, uwazi yaani.
No offense, lakini embu tujifunze kupenda objectivity kabla ya kuandika ujinga ujinga humu.
 
Na ukiwa kiongozi alafu ukakosa namna nzuri ya kuwasilisha taarifa matokeo yake ndo haya.
Off course kauli yake imetufanya wengine tuamini kwamba data alizokuwa akizitoa zilikuwa Ni za kupikwa,
Sijajua aliwaza Nini kutamka hivo, Lakini kauli yake imezua maswali mengi.
 
Huyo waziri anaujua ukweli kuwa tatizo la Covid-19 nchini ni kubwa kuliko anavyoitangazia dunia!!
Naungana na WHO kuwa pengine data zetu si za kweli kutokana na ama aina ya vipimo vinavyotumika au tunapika data makusudi kabisa!!
Pitia data za jana tarehe 8.4.2020 (imeambatanishwa hapa).
Kwa akili ya kawaida miongoni mwa hao 410 na 129 (pamoja na walioko majumbani na mitaani wanaojitibu wenyewe kwa PCM na vidonge vya chenga) kuna "wagonjwa" wengi sana tu!!
(Ieleweke kuwa sifurahii idadi kubwa ya wagonjwa nchini... Lakini pia sipendezwi na jitihada za kuwarubuni Watanzania)!!
Mwisho; utaratibu wa kutoa taarifa chini ya waziri Ummy unaibua maswali mengi sana ambayo inapunguza imani kwenye taarifa zake...!!

Tuendelee kujipange jamani... Covid-19 ipo mtaani toka kitambo!!! Serikali ilipuuzia toka awali...
Sema sisi tutaendelea kupona kama tunavyoponaga!!

 
Majirani zetu Kenya, Uganda na Rwanda walichukua maamuzi mazito mapema mara baada ya ugonjwa kuanza kuingia. Pamoja na hatua kubwa walizo chukua bado wana idadi kubwa ya wagonjwa kuliko sisi.

Nikiwaza kwa sauti namwona waziri wetu wa afya kama mtu anaye fahamu ukweli fulani ambao sisi hatuujui lakini yeye kama waziri hana nguvu ya kuusema hivyo pengine hadhira aliyokuwa nayo leo ya watumishi wa Mungu imempa ujasiri wa kusema alicho kisema na pengine anaona amechelewa na hivyo asiendelee kuchelewa ili asije kuwa mmoja wa watu watakaopewa lawama hapo baadaye.

Nafikiri tusianze kumpa lawama bali tuanze kuwa makini zaidi hasa wale waliokuwa wanaona mambo safi tu na kuchapa kazi bila kutishika.
 
Ni nani kati yetu amemuona jirani yake, ndugu yake au mfanyakazi mwenzake anaugua korona? Hizo hofu mnazitoa wapi? Kama korona imeua ulaya lazima iue na hapa? Mbona ukimwi unatuua hapa lakini ulaya sio tishio? Acheni kujaza watu hofu siku ya kufa ikifika utakufa tu... Hata ungekua nani..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiuhalisia sisi tuna maambukizi mengi kuliko majirani zetu
Nakubaliana na wewe 100% kwamba leo Kenya wamepimwa watu watatu ambao wametoka Tanzania na wamekutwa na CORONA wote halafu juzi kuna watu wawili walitokea Tanga walikwenda Zanzibar wamepimwa huko ZNZ wamekutwa na huu ugonjwa.Sasa kwa hali kama hii unafikiri kwa jinsi gani huu ugonjwa ulivyoenea hapa Nchini bila ya sisi wenyewe kujitambua,na yote haya yanatikea kwa vile idadi ya wanaopimwa ni ndogo sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Na kwa jinsi hii ' Social Distancing ' isivyokuwa ' serious ' nchini Tanzania nina uhakika hii ' Community Transmission ' ya Waziri Ummy Mwalimu ikianza tu huenda ' Dhahama ' ikawa Kubwa kuliko ya hata kule Jimbo la Wuhan nchini China ambako Betrii ndiyo ilichomolewa na Wachina wenyewe kwa mara ya Kwanza.
 
Leta source ya habari yako
 
UCHAGULIWE WEWE WAZIRI AMA
KHA SI DUNIANZIMA WANGEJIUZULU NA WA ITALY UNGEMUUA KABISA..HIZOO NYOTA KAMA UAMINI FATILIA MAIAHA YAKE UONE KILE CHUMA HATA AONGELEWEJE HUMU..
 
ZAWADI GANI.MM NITAMTOLEA BWANA WANGU ILA ROHO YANGU TU POKEA SADAKA HIZI BWANA TENA UZIBARIKI BWANA UZIJAZE BARAKA ZAKOOOO....

MM NITOE NN AMBACHO CHA THAMANI KWAKO ILA ROHO YANGU TU.......
 
Mie ninacho nisikitisha hatoi mikakati gani wanafanya kuikabili hali hiyo,na lazima hawa wasomi wajijue kuwa wana wajibika kwa mamilion ya watu masikini wasio na elimu,hizi taarifa anazozitoa na tahazari hazitoshi kwa mtu wa mangala changanyikeni asie na elimu,haitoshi law watu wakulima wa kijijini.
 
Mimi nilitegemea angetoa maelekezo kwa viongozi wa dini kuacha kufanya mikusanyiko wakati hali inapoelekea kuwa tete lakini kama vile amewaogopa. Tutakufa sana kwakuwa tunaogopa kuchukua hatua. Tumefunga mikusanyiko ya lazima kama shule na vyuo halafu tunaruhusu mikusanyiko isiyo ya lazima kama ya makanisani na misikitini. Watu wasali majumbani kwao mpaka hali itengemae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…