Kauli za sasa za Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kuhusu CORONA zimeshaanza Kuzua 'taharuki' nchini, hivyo ama adhibitiwe au ajiuzuru upesi

Ukitaka Kujigundua na hata Kujithibitisha kuwa ' You're a BONA FIDE MORON ' hapa Jamvini JamiiForums angalia Wenzako wote hapo juu walivyochangia na ulivyochangia Wewe Mrithi Mwandamizi wa Upumbavu nchini Tanzania.
Msamehe! Hajakuelewa tu!
 
Tunajua na hakuna Mtanzania hasa mfuatiliaji wa Mambo asiyejua kuwa kiukweli COVID-19 ni hatari na ' inapukutisha ' Watu kweli kweli kuanzia Mataifa ya Kitajiri (Ulaya na Marekani) na hata katika baadhi ya nchi zetu za Afrika na kwa Majirani zetu wakubwa Kijiografia Kenya, Uganda na Rwanda.

Nimekuwa nikifuatilia hasa kwa baadhi ya nchi zenye Maambukizi na hata Vifo jinsi Mawaziri wao wa Afya wanavyokuwa ' Smart ' kama kutoa Taarifa kwa Wananchi Wao katika njia ya Kiumakini na iliyojaa zaidi Saikolojia ya Kimawasiliano kiasi kwamba haiwezi Kuwashtua.

Hakuna asiyejua (labda awe Mpumbavu tu) kuwa karibia 85% ya Wananchi wa hizi nchi zetu Masikini (za Kingumbaru) Tanzania ikiwemo upataji Wao wa Kipato unategemea mno Kutoka na Kutafuta katika sehemu mbalimbali hivyo ikitokea tu wakapewa Taarifa kwa Kitisho itawatesa zaidi Kisaikolojia.

Muda si mrefu Waziri wa Afya wa Tanzania Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametoka Kutoa Kauli ambayo kwa tulio Mtaani sasa (katika Jamii) tunaanza Kuona jinsi Watu wakianza Kuchanganyikiwa na Kupata ' taharuki ' ukizingatia tayari harakati za Sikukuu ya Pasaka zimeshaanza kwa wengi.

Kauli yake Waziri ya kuwataka Watanzania wajiandae kwa Maambukizi Makubwa zaidi ya COVID-19 ndani ya Siku chache zijazo kutoka sasa mwenyewe akiyaita ' Community Transmission ' ilipaswa itolewe Kiumakini na ikiwezekana awahusishe Wataalam wa Mawasiliano na sivyo alivyofanya.

Tayari huku Mitaani naanza Kushuhudia Watu wakitishana kuwa sijui kuanzia Wiki ijayo Watanzania wengi hasa wana Dar es Salaam watakufa sana kwa CORONA. Kuna Watu nimewasikia wakisema kuwa wanataka Kulikimbia Jiji la Dar es Salaam ili Wasife na tufe Sisi tu Mapopoma wa Jiji hili.

Na asichokijua huyu Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ni kwamba hii Kauli yake inaweza ikapelekea hata hali ya Maisha na ya Kibiashara (hasa kwa Bidhaa na Huduma) kuanza kuwa ngumu na Watu Kuteseka. Na kuna Uwezekano hata Uhalifu ukaongezeka na hali kuwa mbaya zaidi.

Kwa ' Udhaifu ' huu wa utoaji wake Taarifa na hasa hii ya leo kuwa Watanzania wajiandae kwa ' Dhahama ' kubwa ya CORONA na Mwenendo wake mzima katika Kukabiliana na hili Janga sasa ni rasmi huyu Mwamama na Dada yetu ' ajiuzuru ' tu upesi awapishe wenye uwezo zaidi yake.

Nimesikitika sana!

Nawasilisha.
Huyu mama "hususan" hana hadhi ya kuwa waziri huenda ni ...
 
Watanzania tuache ujinga
Tuache tabia ya kutaka kusikia tunayotaka kusikia badala ya kupenda kusikia ukweli.

Kama kauli ya Waziri ndiyo ukweli wenyewe, wacha ukweli usemwe wazi na bila ya kupindisha. Mleta mada una uhakika gani kuwa hiyo kauli ya Waziri haijatokana na projections za wataalam?
 
Tuache uzwazwa, ameongea kwa ufasaha sana, bora kuambiana ukweli kuliko kufichaficha.
 
Hangaikeni wee ila tambueni hakuna mtu anayeweza kulinda uhai wake duniani. Hakuna aliye na mamla na uhai wake..Muda ukifika utakufa kama bado huwezi kufa kamwe!
.....Bwana asipoulinda mji waulindao wanakesha
Sure........

Watu sasa hivi wengine wapo plan C kwamba hali ikiwa hivi nitafanya hivi hawajui yupo anayefanya wawepo au wasiwepo,siyo kwa uwezo wetu unaweza ukasema unajifungia ndani ukapigwa shot ya umeme ukafa muhimu tumuachie Mungu na tuzingatie shauri tunazopewa na wataalamu wa afya.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Wewe unamtukana Waziri wetu wa Afya your Umentally fit. tena Koma kabisa kutukana viongozi wew
 
Ukweli mchungu
Mkuu mtu asiye elimika katika basic principles za hygine ni vigumu sana kumuelimisha ukubwani.
Watu hawaelewi.
Nakumbuka Miaka ya Mwalimu Mzee Bryceson aliposema ugonjwa wa kipindupindu unatokana na kula uchafu wako mwenyewe.
Waswahili pamoja na wanasiasa w TANU miaka hiyo hapa walikuja juu kama moto wa nyika, wakisema mzungu kawatukana.

Bryceson alikuwa sawa kabisa kisayansi maana kipindupindu kinatokana na bacteria wa ecoli ambao hutkana na kinyesi cha binadamu.
Wangekuwa wameelimika wangejua jinsi ya kujikinga.
Hili gonjwa la corona tukisema linhitaji total lockdown, watu wanasema tunampinga mhasehimiwa Magufuli.
Hivyo hkuna njia watu wapukutike tu ili tupate akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunajua na hakuna Mtanzania hasa mfuatiliaji wa Mambo asiyejua kuwa kiukweli COVID-19 ni hatari na ' inapukutisha ' Watu kweli kweli kuanzia Mataifa ya Kitajiri (Ulaya na Marekani) na hata katika baadhi ya nchi zetu za Afrika na kwa Majirani zetu wakubwa Kijiografia Kenya, Uganda na Rwanda.

Nimekuwa nikifuatilia hasa kwa baadhi ya nchi zenye Maambukizi na hata Vifo jinsi Mawaziri wao wa Afya wanavyokuwa ' Smart ' kama kutoa Taarifa kwa Wananchi Wao katika njia ya Kiumakini na iliyojaa zaidi Saikolojia ya Kimawasiliano kiasi kwamba haiwezi Kuwashtua.

Hakuna asiyejua (labda awe Mpumbavu tu) kuwa karibia 85% ya Wananchi wa hizi nchi zetu Masikini (za Kingumbaru) Tanzania ikiwemo upataji Wao wa Kipato unategemea mno Kutoka na Kutafuta katika sehemu mbalimbali hivyo ikitokea tu wakapewa Taarifa kwa Kitisho itawatesa zaidi Kisaikolojia.

Muda si mrefu Waziri wa Afya wa Tanzania Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametoka Kutoa Kauli ambayo kwa tulio Mtaani sasa (katika Jamii) tunaanza Kuona jinsi Watu wakianza Kuchanganyikiwa na Kupata ' taharuki ' ukizingatia tayari harakati za Sikukuu ya Pasaka zimeshaanza kwa wengi.

Kauli yake Waziri ya kuwataka Watanzania wajiandae kwa Maambukizi Makubwa zaidi ya COVID-19 ndani ya Siku chache zijazo kutoka sasa mwenyewe akiyaita ' Community Transmission ' ilipaswa itolewe Kiumakini na ikiwezekana awahusishe Wataalam wa Mawasiliano na sivyo alivyofanya.

Tayari huku Mitaani naanza Kushuhudia Watu wakitishana kuwa sijui kuanzia Wiki ijayo Watanzania wengi hasa wana Dar es Salaam watakufa sana kwa CORONA. Kuna Watu nimewasikia wakisema kuwa wanataka Kulikimbia Jiji la Dar es Salaam ili Wasife na tufe Sisi tu Mapopoma wa Jiji hili.

Na asichokijua huyu Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ni kwamba hii Kauli yake inaweza ikapelekea hata hali ya Maisha na ya Kibiashara (hasa kwa Bidhaa na Huduma) kuanza kuwa ngumu na Watu Kuteseka. Na kuna Uwezekano hata Uhalifu ukaongezeka na hali kuwa mbaya zaidi.

Kwa ' Udhaifu ' huu wa utoaji wake Taarifa na hasa hii ya leo kuwa Watanzania wajiandae kwa ' Dhahama ' kubwa ya CORONA na Mwenendo wake mzima katika Kukabiliana na hili Janga sasa ni rasmi huyu Mwamama na Dada yetu ' ajiuzuru ' tu upesi awapishe wenye uwezo zaidi yake.

Nimesikitika sana!

Nawasilisha.
Waziri yuko sahihi kwa hili
 
Aisee anachokiongea ummy ni sahihi ila wanalumumba huwa mmezoea kuwa njia ya kupambana na vitu kama maradhi,rushwa na maafa ni kudanganya na kufoji Statics ndo maana mnakaa kupinga u kwel kila wakati

Endeleeni kumpinga ummy mtakufa sana
 
Mjifunze kupenda kuambiwa ukweli mimi bioafisi nimemuekewa waziri agesema hii kitu toka ugonjwa ulipoingia na uhakika tungekuwa hatuna mahambukizi hata matano. lakn uzembe uzembe umetugalimu tujiandae.
 
Tunajua na hakuna Mtanzania hasa mfuatiliaji wa Mambo asiyejua kuwa kiukweli COVID-19 ni hatari na ' inapukutisha ' Watu kweli kweli kuanzia Mataifa ya Kitajiri (Ulaya na Marekani) na hata katika baadhi ya nchi zetu za Afrika na kwa Majirani zetu wakubwa Kijiografia Kenya, Uganda na Rwanda.

Nimekuwa nikifuatilia hasa kwa baadhi ya nchi zenye Maambukizi na hata Vifo jinsi Mawaziri wao wa Afya wanavyokuwa ' Smart ' kama kutoa Taarifa kwa Wananchi Wao katika njia ya Kiumakini na iliyojaa zaidi Saikolojia ya Kimawasiliano kiasi kwamba haiwezi Kuwashtua.

Hakuna asiyejua (labda awe Mpumbavu tu) kuwa karibia 85% ya Wananchi wa hizi nchi zetu Masikini (za Kingumbaru) Tanzania ikiwemo upataji Wao wa Kipato unategemea mno Kutoka na Kutafuta katika sehemu mbalimbali hivyo ikitokea tu wakapewa Taarifa kwa Kitisho itawatesa zaidi Kisaikolojia.

Muda si mrefu Waziri wa Afya wa Tanzania Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametoka Kutoa Kauli ambayo kwa tulio Mtaani sasa (katika Jamii) tunaanza Kuona jinsi Watu wakianza Kuchanganyikiwa na Kupata ' taharuki ' ukizingatia tayari harakati za Sikukuu ya Pasaka zimeshaanza kwa wengi.

Kauli yake Waziri ya kuwataka Watanzania wajiandae kwa Maambukizi Makubwa zaidi ya COVID-19 ndani ya Siku chache zijazo kutoka sasa mwenyewe akiyaita ' Community Transmission ' ilipaswa itolewe Kiumakini na ikiwezekana awahusishe Wataalam wa Mawasiliano na sivyo alivyofanya.

Tayari huku Mitaani naanza Kushuhudia Watu wakitishana kuwa sijui kuanzia Wiki ijayo Watanzania wengi hasa wana Dar es Salaam watakufa sana kwa CORONA. Kuna Watu nimewasikia wakisema kuwa wanataka Kulikimbia Jiji la Dar es Salaam ili Wasife na tufe Sisi tu Mapopoma wa Jiji hili.

Na asichokijua huyu Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ni kwamba hii Kauli yake inaweza ikapelekea hata hali ya Maisha na ya Kibiashara (hasa kwa Bidhaa na Huduma) kuanza kuwa ngumu na Watu Kuteseka. Na kuna Uwezekano hata Uhalifu ukaongezeka na hali kuwa mbaya zaidi.

Kwa ' Udhaifu ' huu wa utoaji wake Taarifa na hasa hii ya leo kuwa Watanzania wajiandae kwa ' Dhahama ' kubwa ya CORONA na Mwenendo wake mzima katika Kukabiliana na hili Janga sasa ni rasmi huyu Mwamama na Dada yetu ' ajiuzuru ' tu upesi awapishe wenye uwezo zaidi yake.

Nimesikitika sana!

Nawasilisha.

Mkuu Genta,

Nafikiri waziri dada Ummy ameaua kutangaza hivyo, baada ya kushauriana na jopo la wataalam na kubaini kwamba bado hakuna lockdown.

Lockdown ingeweza kupunguza ile maambkizi baina ya watu khasa kwenye mikusanyiko ya watu wengi.

Ila ukweli ni kwamba raia wengi wa kigeni wakiwemo wachina , na watanzania ambao walitokea huko nje na ambao hawakuwekwa kwenye karantini, wote hao ndo sasa wako kwenye kilele cha ugonjwa yaani "Peak"

Hivyo basi kitakwimu kama kungekuwa na lockdown basi kwa Tanzania mtu mmoja angeambukiza labda watu watano badala ya watu ishirini kwenye misongamano na zaidi.

Lakini kwa kuwa hakukuwa na lockdown tokea mwanzo na karantini za kutosha kuzuia wale waloambukizwa wasieneze ugonjwa, basi watu wote ambao waliambukizwa mwezi wa tatu mwznzoni na wale waloambukizwa mwanzoni mwa mwezi April wote hao kwa sasa wataambukiza zaidi watu wengi khasa makanisani na kwenye mikusanyiko kama pale mtaa wa Kongo na sokoni Kariakoo.

Hivyo serikali isingefanya lockdown kwa Dodoma tu bali ingetafuta namna ya "lock down in Tanzania style" labda kuweka masaa maalum ya kufanya biashara na wananchi kununua bidhaa halafu kunafungwa.

Tunakubali kwamba nchi yetu ni maskini sana lakini tungechukua hatua kadhaa za angalau kuonekana tumejitakidi kukabiliana na hili tatizo.

Masoko makuu yote yangefungwa, kungebakia maduka ya kawaida na wananchi wangekuwa wanafuata masharti kama kawaida kutosogoleana na kutumia vitakasa mikono na kunawa mikono.

Ila kiukweli waziri yuko sahihi akimaanisha kwamba wale wote ambao ni wagonjwa kwa sasa wapo kwenye hatua ya kuambukiza kabla hawajafa kwasababu wameachwa wakizagaa mitaani.

Hivyo, wananchi hakuna haja ya kwenda makanisani na kwenye misongamano mikiubwa kwani huko ndiko kwenye matukio makubwa ya maambukizi ya karne ya 21.

Jambo jingine ambalo lanistua sana kiukweli ni kwamba pia lanishangaza sana, ni uamuzi wa serikali kupokea misaada itokayo huko Uchina misaada ambayo hatuelezwi ni ipi yaani labda ni hizo mask au gloves au ni nini khasa hiyo misaada?

Je Serikali yetu yatambua kwamba serikali nyingi duniani zimekataa misaada hiyo ya kutoka China?

Utawezaje kupokea misaada kwa mfano ya mask ambazo hatufahamu kama zimetengenezwa lini na wapi?

Na kwanini China amekazana kutoa sana misaada huku kwetu baada ya misaada hiyo kukataliwa huko Ulaya na Marekani?
 
Mkuu Genta,

Nafikiri waziri dada Ummy ameaua kutangaza hivyo, baada ya kushauriana na jopo la wataalam na kubaini kwamba bado hakuna lockdown.

Lockdown ingeweza kupunguza ile maambkizi baina ya watu khasa kwenye mikusanyiko ya watu wengi.

Ila ukweli ni kwamba raia wengi wa kigeni wakiwemo wachina , na watanzania ambao walitokea huko nje na ambao hawakuwekwa kwenye karantini, wote hao ndo sasa wako kwenye kilelelcha ugonjwa yaani "Peak"

Hivyo basi kitakwimu kama kungekuwa na lockdown basi kwa Tanzania mtu mmoja angeambukiza labda watu watano badala ya watu ishirini kwenye misongamano na zaidi.

Lakini kwa kuwa hakukuwa na lockdown tokea mwanzo na karantini za kutosha kuzuiia wale waloambukizwa wasieneze ugonjwa, basi watu wote ambao waliambukizwa mwezi wa tatu mwznzoni na wale waloambukizwa mwanzoni mwa mwezi April wote hao kwa sasa wataambukiza zaidi watu wengi khasa makanisani na kwenye mikusanyiko kama pale mtaa wa Kongo na sokoni Kariakoo.

Hivyo serikali isingefanya lockdown kwa Dodoma tu (maana mazee si wamejifungia huko?), bali ingetafuta namna ya "lock down in Tanzania style" labda kuweka masa maalum ya kufanya biashara na wananchi kununu a bidhaa halafu kunafungwa.

Tunakubali kwamba nchi yetu ni maskini sana lakini tungechukua hatua kadhaa za angalau kuonekana tumejitakidi kukabiliana na hili tatizo.

Masoko makuu yote yangefungwa, kungebakia maduka ya kawaida na wananchi wangekuwa wanafuata masharti kama kawadia kutosogoleana na kutumia vitakasa mikono na kunawa mikono.

Ila kiukweli waziri yuko sahihi akimaanisha kwamba wale wote ambao ni wagonjwa kwa sasa wapo kwenye hatua ya kuambukiza kalba hawajafa kwasabau wameachwa wakizagaa mitaani.

Hivyo, wananchi hakuna haja ya kwenda makanisani na kwenye misongamano mikiubwa kwani huko ndiko kwenye matukio makubwa ya maambukizi ya karne ya 21.

Jambo jingine ambalo lanistua sana kiukweli ni kwamba nashangazwa sana na uamuzi wa serikali kupokea misaada itokayo huko Uchina misaada ambayo hatuelezwi ni ipi yaani labda ni hizo mask au gloves au ni nini khasa hiyo misaada?

Je Serikali yetu yatambua kwamba serikali nyingi duniani zimekataa misaada hiyo ya kutoka China?

Utawezaje kupokea misaada kwa mfano ya mask ambazo hatufahamu kama zimetengenezwa lini na wapi?

Na kwanini China amekazana kutoa sana misaada huku kwetu baada ya maisaad ahiyo kukataliwa huko Ulaya na Marekani?

Hali mbaya

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Yawezekana kuna Kitu Watanzania tunafichwa na nimekuwa nikijiuliza Maswali mengi sana kwamba kwanini Serikali ya China iko ' busy ' mno Kuisadia Tanzania kwa hii COVID-19 ambayo haina Kiwango hicho Kikubwa cha Maambukizi na hawafanyi hivyo kwa nchi kama ya Kenya ambayo kila Uchwao ina Maambukizi mengi.

Ukiangalia kwa umakini huu ukaribu wa Kimsaada wa Wachina na hivi leo Waziri wa Afya anasema anaangalia uwezekano wa Kuwaambia Watanzania wawe wanatumia Barakoa ( Mask ) yawezekana kuna lililojificha zaidi juu ya COVID-19 hapa Tanzania pengine hata huko Kenya, Uganda na Rwanda. Naanza Kuogopa sasa!
Mtoa mada ukweli unaujua kabisa kilichopo nyuma ya pazia hasa Kwenye kutoa matamko juu ya ugonjwa huu,sasa taarifa yako ni kuwa ummy mwalimu Hana mamlaka yeyote ya kutamka hayo aliyosema leo.

Ukiona taarifa umetoka juu ya Corona ujuwe imeshafanyiwa editing na adidu za rejea kutoka ikulu,wakati wenzetu wako serious na gonjwa Sisi Yuko busy na siasa ebu chukulia mfano wa pale bungeni baada ya mbunge Abdala bulembo kumtaka raisi achaguliwe bila kufanyika Kwa uchaguzi,Kwa kauli kama hiyo unafikiri inatoka Kwa Nani kama sio raisi?
Serikali imeshachua ugonjwa huu na kufanyiwa siasa za chama.
 
Mkuu inaelkea wewe ulisomea historia na kiswahili darasani, na hujui A toZ za sayansi.
Tumekuwa tukionya humu mtandaoni juu ya maambukizi ya huu ugonjwa na wengi wenu mmeamua kuwaamini wanasiasa.

Maambukizi kama ilivyo huko Ulaya hayaepukiki na dawa yake si sanitizer na kunawa maji ya kutiririka na sabuni tu.

Tunaposema total lockdown watu hamuelewi, ngoja watu waanze kuanguka kama nzi.
Piga magoti mwombe Mungu aepushe huu ubashiri wako. Watanzania hatupo tayari kuanguka kama nzi.
 
Si ndo tunachapa kazi huku tukiambukiza corona.maana sisi ni masikini na serikali tuliyoaminishwa na kiongozi wake kuwa ndo tajiri ndo choka mbaya kuliko sisi wanyonge
Chapa kazi kwa kwenda mbereeee
 
Back
Top Bottom