Kauli za sasa za Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kuhusu CORONA zimeshaanza Kuzua 'taharuki' nchini, hivyo ama adhibitiwe au ajiuzuru upesi

Kauli za sasa za Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kuhusu CORONA zimeshaanza Kuzua 'taharuki' nchini, hivyo ama adhibitiwe au ajiuzuru upesi

Tunajua na hakuna Mtanzania hasa mfuatiliaji wa Mambo asiyejua kuwa kiukweli COVID-19 ni hatari na ' inapukutisha ' Watu kweli kweli kuanzia Mataifa ya Kitajiri ( Ulaya na Marekani ) na hata katika baadhi ya nchi zetu za Afrika na kwa Majirani zetu wakubwa Kijiografia Kenya, Uganda na Rwanda.

Nimekuwa nikifuatilia hasa kwa baadhi ya nchi zenye Maambukizi na hata Vifo jinsi Mawaziri wao wa Afya wanavyokuwa ' Smart ' kama kutoa Taarifa kwa Wananchi Wao katika njia ya Kiumakini na iliyojaa zaidi Saikolojia ya Kimawasiliano kiasi kwamba haiwezi Kuwashtua.

Hakuna asiyejua ( labda awe Mpumbavu tu ) kuwa karibia 85% ya Wananchi wa hizi nchi zetu Masikini ( za Kingumbaru ) Tanzania ikiwemo upataji Wao wa Kipato unategemea mno Kutoka na Kutafuta katika sehemu mbalimbali hivyo ikitokea tu wakapewa Taarifa kwa Kitisho itawatesa zaidi Kisaikolojia.

Muda si mrefu Waziri wa Afya wa Tanzania Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametoka Kutoa Kauli ambayo kwa tulio Mtaani sasa ( katika Jamii ) tunaanza Kuona jinsi Watu wakianza Kuchanganyikiwa na Kupata ' taharuki ' ukizingatia tayari harakati za Sikukuu ya Pasaka zimeshaanza kwa wengi.

Kauli yake Waziri ya kuwataka Watanzania wajiandae kwa Maambukizi Makubwa zaidi ya COVID-19 ndani ya Siku chache zijazo kutoka sasa mwenyewe akiyaita ' Community Transmission ' ilipaswa itolewe Kiumakini na ikiwezekana awahusishe Wataalam wa Mawasiliano na sivyo alivyofanya.

Tayari huku Mitaani naanza Kushuhudia Watu wakitishana kuwa sijui kuanzia Wiki ijayo Watanzania wengi hasa wana Dar es Salaam watakufa sana kwa CORONA. Kuna Watu nimewasikia wakisema kuwa wanataka Kulikimbia Jiji la Dar es Salaam ili Wasife na tufe Sisi tu Mapopoma wa Jiji hili.

Na asichokijua huyu Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ni kwamba hii Kauli yake inaweza ikapelekea hata hali ya Maisha na ya Kibiashara ( hasa kwa Bidhaa na Huduma ) kuanza kuwa ngumu na Watu Kuteseka. Na kuna Uwezekano hata Uhalifu ukaongezeka na hali kuwa mbaya zaidi.

Kwa ' Udhaifu ' huu wa utoaji wake Taarifa na hasa hii ya leo kuwa Watanzania wajiandae kwa ' Dhahama ' kubwa ya CORONA na Mwenendo wake mzima katika Kukabiliana na hili Janga sasa ni rasmi huyu Mwamama na Dada yetu ' ajiuzuru ' tu upesi awapishe wenye uwezo zaidi yake.

Nimesikitika sana!

Nawasilisha.
Jamaa huyu hapa anatuombea,so ninyi pigeni kazi serikali isikose hela
 
kila mara nasema corona INAJIONYESHA YENYEWE..
Hata usipopima watu kama wapo wanaoumwa wataonekana..
JE wapo hao wanaonekana?.
WANA DALILI KUWA WANA CORONA?.
Korona haijifichi mzee.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"

Kwa hiyo waliowekeza kwenye vipimo na kuwatenga walioathilika hawajui kua unaonekana?!
Kwa taarifa yako kuna wengine wengi ni asymptomatic wanaeneza na mtu kawaida anaanza kuugua baada ya wiki mbili au zaidi
 
Wewe ulivyo popoma badala ya kuelezea nini kifanyike baada ya tamko la waziri. Unaishi kulalama tu hapa.

Ok. Ulitaka mh Ummy abaki na taarifa ili kesho na kesho kutwa muanze kusema serikali inaficha taarifa. Nyumbu mnatakiwa kibadilika.

Serikali inachukua kila hatua ili kudhibiti ili janga halafu wewe unaleta midhaa hapa.
Hatua zipi serikali imechukua mkuu? Kutembeza bakuli au kutuambia tukachape kazi?
 
Kuchelewa kuwazuia Wachina na au kuwaweka karantini siku 14 kabla hawajaanza umachinga wao hapa Tz yaweza kutugharimu maisha ya WATZ wengi.

Wamefikia wangapi hadi jioni hii?

Kuna waliotangulia mbele za haki?
Tumeshaambiwa mmoja mkuu.
 
kila mara nasema corona INAJIONYESHA YENYEWE..
Hata usipopima watu kama wapo wanaoumwa wataonekana..
JE wapo hao wanaonekana?.
WANA DALILI KUWA WANA CORONA?.
Korona haijifichi mzee.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
We kenge soma hii attachment alafu uache kutetea ujinga
 

Attachments

  • IMG-20200409-WA0030.jpg
    IMG-20200409-WA0030.jpg
    50 KB · Views: 1
Mbona kauli ya Ummy ya kistaarabu nchi za ulaya wanaambiwa kuna watu mtapoteza ndugu na marafiki kabla ya wakati wao huo ndio ukweli ambao muwe tayari kuupokea.

Hakuna kurembua macho kwenye vita ya Corona watu wanatakiwa kupewa ukweli ili waongeze umakini wa kujilinda simple as that.
 
Tatizo watanzania tunapenda kuremba maneno, hata kama ni kibaya wanataka ukiongelee kwa uzuri, tujifunze kusema ukweli, nyeusi siku zote itabaki kuwa nyeusi na haiwezi kuwa nyeupe. Hivyo alivyosema ndio ukweli ulivyo, hata hiyo Italy na USA walipitia stage kama hizo tunazopitia sisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu namna alivyoiwasilisha kwa wengi ni kama amewatisha na imezua taharuki pia Kwao. Na hii ni kwa mtazamo wangu ambao simlazimishi Mtu mwingine akubaliane nao japo anatakiwa Kuuheshimu kama nami pia ninavyoheshimu Mitazamo yao.
Bro asilimia kubwa ya watu wanaoishi mijini wanajua corona ni nini na namna gani ya kuepuka maambukizi ya corona, unataka asemaje sasa? Huo ndio ukweli na kitakachofuatia ni lock down hizo propaganda za kina Bashite zisitupumbaze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenyezi Mungu tunasulu sisi waja wako .


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu mtu asiye elimika katika basic principles za hygine ni vigumu sana kumuelimisha ukubwani.
Watu hawaelewi.
Nakumbuka Miaka ya Mwalimu Mzee Bryceson aliposema ugonjwa wa kipindupindu unatokana na kula uchafu wako mwenyewe.
Waswahili pamoja na wanasiasa w TANU miaka hiyo hapa walikuja juu kama moto wa nyika, wakisema mzungu kawatukana.

Bryceson alikuwa sawa kabisa kisayansi maana kipindupindu kinatokana na bacteria wa ecoli ambao hutkana na kinyesi cha binadamu.
Wangekuwa wameelimika wangejua jinsi ya kujikinga.
Hili gonjwa la corona tukisema linhitaji total lockdown, watu wanasema tunampinga mhasehimiwa Magufuli.
Hivyo hkuna njia watu wapukutike tu ili tupate akili.

Wangefanya curfew siku za weekend, yaani ijumaa Hadi jumapili hakuna kutoka nje... Kwa majaribio.
Alisikika raia mmoja wa Kongo akiongea.
 
Umejaribu kuongea kuhusu uwasilishaji wa taarifa na namna unavyoweza kuleta madhara makubwa kisaikolojia Ni vizuri.

Lkn mimi sidhani kwa upande mwingine inaweza leta taharuki kiasi hicho ambacho umejaribu kuaminisha umma. Watanzania kwa asilimia kubwa kwa utafiti nilioufanya katika kipindi hiki ambacho Dunia na Taifa letu linapitia katika wakati mgumu wavkuoambana na COVID-19, Wamekuwa wakifuatilia kwa ukaribu mkubwa Sana yanayoendelea katika nchi nyingi duniani na namna wanavyohangaika na janga Hili.Haijalishi serikali kupitia wizara ya afya itanawasilishaje ujumbe kuhusu Hali ya corona lkn watanzania wanaelewa Hali iliuopo duniani.

Chamsingi tulipo sahivi sio jukumu la serikali tu kujaribu kujenga saikolojia ya watu kuhusu Tahadhari kubwa ya corona, initiatives zianzie katka family level ili Serikali iwe kazi rahisi Sana kuhusu Hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha muhimu ili Serikali iweze kuzuia maambukizi mapya na ugonjwa wa corona kufika sehemu ambazo bado hazijapata hata mgonjwa mmoja, ingegawa mask (barakoa) hasa kwa mikoa yenye magonjwa wa corona na kutoa amri kila mtu avae pindi anapokhwa nje ya nyumba yake au kwenye shughuli zake binafsi na kuzuia safari za kuvuka mkoa (mabasi na gari binafsi) isipokuwa maloli tuu ya mizigo ili kuendeleza shughuli za kiuchumi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom