Tunajua na hakuna Mtanzania hasa mfuatiliaji wa Mambo asiyejua kuwa kiukweli COVID-19 ni hatari na ' inapukutisha ' Watu kweli kweli kuanzia Mataifa ya Kitajiri (Ulaya na Marekani) na hata katika baadhi ya nchi zetu za Afrika na kwa Majirani zetu wakubwa Kijiografia Kenya, Uganda na Rwanda.
Nimekuwa nikifuatilia hasa kwa baadhi ya nchi zenye Maambukizi na hata Vifo jinsi Mawaziri wao wa Afya wanavyokuwa ' Smart ' kama kutoa Taarifa kwa Wananchi Wao katika njia ya Kiumakini na iliyojaa zaidi Saikolojia ya Kimawasiliano kiasi kwamba haiwezi Kuwashtua.
Hakuna asiyejua (labda awe Mpumbavu tu) kuwa karibia 85% ya Wananchi wa hizi nchi zetu Masikini (za Kingumbaru) Tanzania ikiwemo upataji Wao wa Kipato unategemea mno Kutoka na Kutafuta katika sehemu mbalimbali hivyo ikitokea tu wakapewa Taarifa kwa Kitisho itawatesa zaidi Kisaikolojia.
Muda si mrefu Waziri wa Afya wa Tanzania Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametoka Kutoa Kauli ambayo kwa tulio Mtaani sasa (katika Jamii) tunaanza Kuona jinsi Watu wakianza Kuchanganyikiwa na Kupata ' taharuki ' ukizingatia tayari harakati za Sikukuu ya Pasaka zimeshaanza kwa wengi.
Kauli yake Waziri ya kuwataka Watanzania wajiandae kwa Maambukizi Makubwa zaidi ya COVID-19 ndani ya Siku chache zijazo kutoka sasa mwenyewe akiyaita ' Community Transmission ' ilipaswa itolewe Kiumakini na ikiwezekana awahusishe Wataalam wa Mawasiliano na sivyo alivyofanya.
Tayari huku Mitaani naanza Kushuhudia Watu wakitishana kuwa sijui kuanzia Wiki ijayo Watanzania wengi hasa wana Dar es Salaam watakufa sana kwa CORONA. Kuna Watu nimewasikia wakisema kuwa wanataka Kulikimbia Jiji la Dar es Salaam ili Wasife na tufe Sisi tu Mapopoma wa Jiji hili.
Na asichokijua huyu Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ni kwamba hii Kauli yake inaweza ikapelekea hata hali ya Maisha na ya Kibiashara (hasa kwa Bidhaa na Huduma) kuanza kuwa ngumu na Watu Kuteseka. Na kuna Uwezekano hata Uhalifu ukaongezeka na hali kuwa mbaya zaidi.
Kwa ' Udhaifu ' huu wa utoaji wake Taarifa na hasa hii ya leo kuwa Watanzania wajiandae kwa ' Dhahama ' kubwa ya CORONA na Mwenendo wake mzima katika Kukabiliana na hili Janga sasa ni rasmi huyu Mwamama na Dada yetu ' ajiuzuru ' tu upesi awapishe wenye uwezo zaidi yake.
Nimesikitika sana!
Nawasilisha.
Mkuu Genta,
Nafikiri waziri dada Ummy ameaua kutangaza hivyo, baada ya kushauriana na jopo la wataalam na kubaini kwamba bado hakuna lockdown.
Lockdown ingeweza kupunguza ile maambkizi baina ya watu khasa kwenye mikusanyiko ya watu wengi.
Ila ukweli ni kwamba raia wengi wa kigeni wakiwemo wachina , na watanzania ambao walitokea huko nje na ambao hawakuwekwa kwenye karantini, wote hao ndo sasa wako kwenye kilele cha ugonjwa yaani "Peak"
Hivyo basi kitakwimu kama kungekuwa na lockdown basi kwa Tanzania mtu mmoja angeambukiza labda watu watano badala ya watu ishirini kwenye misongamano na zaidi.
Lakini kwa kuwa hakukuwa na lockdown tokea mwanzo na karantini za kutosha kuzuia wale waloambukizwa wasieneze ugonjwa, basi watu wote ambao waliambukizwa mwezi wa tatu mwznzoni na wale waloambukizwa mwanzoni mwa mwezi April wote hao kwa sasa wataambukiza zaidi watu wengi khasa makanisani na kwenye mikusanyiko kama pale mtaa wa Kongo na sokoni Kariakoo.
Hivyo serikali isingefanya lockdown kwa Dodoma tu bali ingetafuta namna ya "lock down in Tanzania style" labda kuweka masaa maalum ya kufanya biashara na wananchi kununua bidhaa halafu kunafungwa.
Tunakubali kwamba nchi yetu ni maskini sana lakini tungechukua hatua kadhaa za angalau kuonekana tumejitakidi kukabiliana na hili tatizo.
Masoko makuu yote yangefungwa, kungebakia maduka ya kawaida na wananchi wangekuwa wanafuata masharti kama kawaida kutosogoleana na kutumia vitakasa mikono na kunawa mikono.
Ila kiukweli waziri yuko sahihi akimaanisha kwamba wale wote ambao ni wagonjwa kwa sasa wapo kwenye hatua ya kuambukiza kabla hawajafa kwasababu wameachwa wakizagaa mitaani.
Hivyo, wananchi hakuna haja ya kwenda makanisani na kwenye misongamano mikiubwa kwani huko ndiko kwenye matukio makubwa ya maambukizi ya karne ya 21.
Jambo jingine ambalo lanistua sana kiukweli ni kwamba pia lanishangaza sana, ni uamuzi wa serikali kupokea misaada itokayo huko Uchina misaada ambayo hatuelezwi ni ipi yaani labda ni hizo mask au gloves au ni nini khasa hiyo misaada?
Je Serikali yetu yatambua kwamba serikali nyingi duniani zimekataa misaada hiyo ya kutoka China?
Utawezaje kupokea misaada kwa mfano ya mask ambazo hatufahamu kama zimetengenezwa lini na wapi?
Na kwanini China amekazana kutoa sana misaada huku kwetu baada ya misaada hiyo kukataliwa huko Ulaya na Marekani?