Kauli za sasa za Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kuhusu CORONA zimeshaanza Kuzua 'taharuki' nchini, hivyo ama adhibitiwe au ajiuzuru upesi

Umenena vyema mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
siku Ukija waza positivity utakua mbali..

Jitu Jinga..kukumaji
Uchangiaji wako, unathibitisha uwezo wako mdogo wa kufikiri, kwa kawaida hoja inapingwa na hoja yenzie na si kama ulivofanya ww, hatupo kwenye uwanja wa mapambano bali tupo kwa ajili ya kushirikishana mambo mbalimbali, yamkin kama huna cha kuchangia ni vema ukabaki kimya kuliko kuonesha mapungufu yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkuu Msamehe tu huyo ' Mpumbavu ' kwani hajawahi Kumiliki Akili ( Upeo ) hata Siku moja.

Cc: Anti-Hacker
 
Binafsi sina tatizo na Kauli ya Waziri.Tatizo lipo katika kauli za mwanzo za viongozi wetu waliotupatia matumaini kwamba tusitishane tuchape kazi,tusipofanya kazi tutakufa .......

Kifupi kauli za mwanzo zilitutia kibri na Sisi wananchi wanyonge tukaanza kujimwambafai na kuendeleza tabia zetu za mwanzo pengine tukifikiri Coronavirus ipo kwaajili ya waItaliano,Wamarekani labda jirani zetu WaKenya.

Wanaporudi tena kwa kupitia viongozi wa dini ambao wengi wao ( Sheikh wa Dar) wameacha kazi zao za msingi na kugeuka kikundi cha kutumikia wanasiasa wenye madaraka.Inafikirisha sana kama si kustaajabisha jinsi hizi kauli zinavyobadilika badilika kila uchwao
 
Ulitaka awasilishe kwa njia gani? Maana naona ...ueleweki watu wanapaswa kuambiwa ukweli..local transmission inaenda kuchukua nafasi ni jambo zuri / isipokuwa mapopoma wetu watz wanaogopa kifo sana.
Mswahili siku zote anataka adanganywe ili nafsi yake iridhike. Na pale Waziri kaongea kistaarabu, tukumbuke nchi nyingine mfano Uganda hili suala la Corona anaongea Museveni mwenyewe, amri zote anazitoa yeye moja kwa moja.

Waziri kaongea ukweli, kama unaweza kununua mask nunua nyingi tu na uanze kuzitumia, maambukizi kutoka nje yamedhibitiwa kwani wahusika wengi wanapona, kasheshe ni yale ya mwananchi mmoja kwenda kwa mwingine aidha ndani ya daladala, benki, kwenye foleni za ATM na maeneo mengine yenye mikusanyiko.
 
Navyohisi mimi wagonjwa wa corona wapo wengi tu sema wanapunguza idadi ili kupunguza taharuki ,kufikia week ijayo siku moja kabla ya kufungua shule na vyuo wanaweza kusema idadi ya ukweli,maana kwa utafiti wangu nilioufanya inaonyesha kwenye kutangaza wanatumia mfumo wa kuongeza watu 2 kila wanapotangaza
 
Walikuwa wanaficha ficha ukweli Sasa itakuwa ni stage ya kufuniana ndani soon

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hangaikeni wee ila tambueni hakuna mtu anayeweza kulinda uhai wake duniani. Hakuna aliye na mamla na uhai wake..Muda ukifika utakufa kama bado huwezi kufa kamwe!
.....Bwana asipoulinda mji waulindao wanakesha
Jipe moyo na usichukue hatua za kujihami na Covid 19...sema kama bado huwezi kufa kamwe....kuna watu waliimba usimchezee Chatu..ohoo Chatu oooh...mengine utajazia kama mkongwe...Nawa mikono Mara kwa Mara epuka mikusanyiko......jielimishe dalili za wagonjwa au ugonjwa wa Covid19..utaepuka vivo au kifo cha kizembe....

Pasaka njema ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujumbe wa Waziri hakika umefika ikiwa hata wewe unataharuki ati ... kuna Watu nimewasikia wakisema kuwa wanataka Kulikimbia Jiji la Dar es Salaam ili Wasife na tufe Sisi tu Mapopoma wa Jiji hili!

Iwapo kila mtu atawajibika ipasavyo hataambukizwa wala kuambukiza, pawepo au pasiwepo na sheria, kanuni, taratibu au amri za kusimamia. Usipozingatia ushauri utaambukizwa pasi na shaka.
 
shida hatutaki kusikia ukweli....ila mh ummy ametoa dokezo kuonyesha tayari tuna wagonjwa ambao wameupa huu ugonjwa ndani ya jamii zetu zinazo tuzunguka


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ndugu yangu hapo hata umtoe umeweke dr.mwinyi nae atakueletea longolongo hizi hizi. Maana unapewa tu usome....
Ndo maana simlaumu sana.
Unadhani wa juu kabisa hawajashauriwa cha kufanya na wamekaza shingo. Sasa Ummy afanyeje.
Ndo maana imebidi awatishe kabisa...msiende vijijini but at the same time PM na Pr wameshindwa kuzuai watu wasisafiri now wanategemea kuwaomba watanzania wasisafiri serious......Ummy hawezi tangaza lockdown ....kuna wa kufannya hivyo but hata hajulikani alipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika nchi fulani, Kamanda Mkuu wa Wanamaji alitoa tahadhari kwamba watu wake watakufa kwa wingi iwapo ugonjwa huo hautadhibitiwa mapema. Waziri mhusika akamfuta kazi ya ukamanda huyo Kamanda ambaye watu wake walimshangilia sana alipotoka kwa mara ya mwisho katika manowari hiyo. Siku chache baadae Kamanda akadondoka kwa hilo gonjwa. Baadhi ya viongozi katika Sekta hiyo wakajiuzuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…