Kauli za Wasira zimethibitisha kuwa CCM haitaki maridhiano

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Screenshot 2026-09-09 113139.png

Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini uliofanyika Dar es Salaam jana, Septemba 8, 2026, ulikuwa na matarajio ya kuwa jukwaa la kutafuta majibu ya mgogoro wa kisiasa unaoikabili Tanzania.

Lakini badala ya kuibua picha ya chama tawala kilicho tayari kusikiliza hoja za wapinzani na kukubali mazungumzo yenye matokeo, baadhi ya kauli za Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, zimeacha maswali mazito kuhusu dhamira ya chama hicho katika mchakato wa maridhiano.

Kwa lugha rahisi, Wasira alionekana kutetea zaidi kile ambacho CCM tayari imeamua kuliko kukubali kwamba kuna tatizo la msingi la kisiasa linalohitaji mazungumzo ya dhati, yanayoweza kugusa hata masuala ambayo chama tawala hakikubaliani nayo.

Hapo ndipo tatizo linapoanzia.

Wasira alisisitiza kuwa mchakato wa Katiba Mpya si jambo la siku moja na kwamba tayari kuna nyaraka muhimu, ikiwamo Katiba ya mwaka 1977 na Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba. Hoja hii ni sahihi kwa sehemu, kwa sababu mchakato wa kikatiba unahitaji muda, ushirikishwaji na maridhiano.

Lakini swali muhimu si kama Katiba Mpya inaweza kuandikwa kwa haraka. Swali ni nani anaamua kuanza mchakato huo, kwa masharti gani na kwa ushiriki wa nani?

Wasira amesema ahadi ya kuanza mchakato ndani ya siku 100 ilitolewa kabla ya uchaguzi wa Oktoba 2025 na kwamba yaliyotokea Oktoba yalibadilisha mazingira kiasi kwamba mchakato usingeweza kuanza Januari.

Hii ni hoja inayoweza kujadiliwa, lakini haiwezi kutumika kama jibu la kudumu kwa madai ya wananchi wanaotaka mabadiliko ya kikatiba. Badala yake, inapaswa kufuatiwa na ratiba, hatua na dhamira inayoonekana ya kuanza mchakato.
Mkutano huo TCD.png

Kwa sababu tatizo kubwa si ukosefu wa nyaraka. Tanzania tayari ina rasimu ya Katiba iliyotokana na mchakato mpana wa kitaifa. Tatizo ni utashi wa kisiasa wa kufungua mjadala huo upya kwa misingi inayokubalika na pande zote.

Wasira pia alihoji wito wa baadhi ya wadau wa "kupambana" ili kupata Katiba Mpya, akisema CCM tayari imeamua kwamba Katiba itaandikwa. Lakini hapa ndipo kauli hiyo inahitaji kuhojiwa.

Kama CCM tayari imeamua, kwa nini bado kuna sintofahamu kubwa kuhusu lini mchakato utaanza, nani atasimamia, utatumia msingi gani na utahusisha kwa kiwango gani vyama vya upinzani, asasi za kiraia, wasomi, dini na wananchi?

Katiba si mradi wa CCM. Ni mkataba wa wananchi, kwa hiyo, chama tawala hakiwezi kuwasilisha uamuzi wake wa ndani kama mbadala wa maridhiano ya kitaifa.

Kesi ya Lissu na dhana ya "kesi za kisiasa"

Hoja nyingine iliyozua maswali ni msimamo wa Wasira kwamba hawezi kuelewa dhana ya "kesi za kisiasa" kwa sababu kesi zilizoko mahakamani ni masuala ya sheria, si siasa.

Ni kweli kwamba mahakama zinapaswa kuwa huru na kuamua kwa mujibu wa sheria. Lakini kusema hivyo hakumalizi mjadala wa kisiasa unaozunguka kesi fulani.

Kesi inaweza kuwa ya kisheria kwa upande wa mahakama, lakini ikaendelea kuwa na athari za kisiasa kwa taifa.

Hili ni jambo ambalo nchi nyingi hutambua. Ndiyo maana katika mazingira ya migogoro ya kisiasa, wanasiasa wanaweza kujadili namna ya kumaliza mgogoro huo bila kuingilia uhuru wa mahakama.

Katika mazingira ya Tanzania, kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, haiwezi kutazamwa kama jalada la kawaida lisilo na athari katika siasa za nchi. Lissu ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani na suala la hatma yake linaathiri moja kwa moja mazingira ya ushindani wa kisiasa na mjadala wa maridhiano.

Hapo ndipo kauli ya Wasira inapokosa upeo mpana wa kisiasa.

Hakuna anayesema CCM iwe mahakama na ifute kesi kwa amri. Hoja ya msingi ni kama viongozi wa kisiasa wanaweza kutafuta suluhu ya kisiasa ya mgogoro ambao unaendelea pia mahakamani.

Kama lengo ni maridhiano, ni vigumu kuzungumza kuhusu kuwaleta Watanzania pamoja wakati mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani bado yuko katikati ya kesi yenye uzito mkubwa wa kisiasa.

mkutano TCD.png

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, amekwenda mbali zaidi kwa kumlinganisha Lissu na Nelson Mandela wa Tanzania na kusema ni muhimu aachiliwe ili awe sehemu ya mchakato wa maridhiano.

Hata kama mtu hakubaliani na mfano huo, hoja yake kuu haiwezi kupuuzwa: maridhiano hayawezi kuwa kamili ikiwa upande mmoja wa mgogoro haushiriki kikamilifu.

Tumeshuhudia hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi akiwaita wasanii na influencers akiwamo pia Sheikh Said Mwaipopo aliyetangaza kuwa na kikundi cha kisheshi na akatishia kuwakata vichwa waandamanaji.

Waziri Katambi alitangaza kuwasamehe wasanii hao kwa tuhuma za jinai walizokuwa nao, huku akisema kuwa Sheikh Mwaipopo alikuwa na nia njema japo hakutumia njia nzuri. Sasa hapo unajiuliza, wangekuwa ndio wapinzani wangesamehewa hivi? Kwa nini watuhumiwa wengine wanatangaziwa msamaha na Serikali na wengine wanaambiwa hizo sio kesi za kisiasa?

"Amani si ya bunduki"

Wasira pia amesema Tanzania haijawahi kuwa na amani ya bunduki, akisisitiza kwamba amani inatokana na watu kufuata sheria na kwamba wanaokiuka sheria ndiyo wanaohitaji "labda bunduki".

Hapa pia kuna ukweli, lakini kuna hatari ya kuifanya dhana ya amani iwe nyembamba mno.

Amani si kutokuwepo kwa vita pekee.

Amani ya kisiasa inahitaji wananchi kuamini kwamba taasisi za dola zinawatendea kwa usawa, kwamba uchaguzi una ushindani wa kweli, kwamba haki zao zinalindwa na kwamba wanaweza kupinga Serikali bila kutishwa au kuadhibiwa.

Ndiyo maana kauli za Padri Dkt. Faustine Furaha katika mkutano huo zinapaswa kuchukuliwa kwa uzito. Ameonya kuhusu rushwa, kupungua kwa hamasa ya vijana kushiriki katika uchaguzi na umuhimu wa kurejesha chaguzi zenye ushindani wa kweli.

CCM na makada wake

Jambo lingine ambalo Wasira alilikanusha ni madai kwamba watu wanaozungumza kwa niaba ya wananchi hushughulikiwa au kuadhibiwa.

Alimjibu Profesa Elgidius Ichumbaki wa Chama cha Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dares Salaam (UDASA) kwa kusema wasomi wanapaswa kufanya utafiti na kwamba wasipofanya hivyo wanaweza kuishia kusema kama mitandao ya kijamii "ambayo haina control".

Hili ni jibu linaloweza kuonekana kama kumkosoa msomi kwa hoja yake, lakini halijajibu swali kuu alilouliza Profesa Ichumbaki.

Kama kweli hakuna watu wanaoadhibiwa kwa kuzungumza kwa niaba ya wananchi, basi CCM inaweza kuweka wazi mifano ya watu waliotajwa na Profesa Ichumbaki na sababu zao za kinidhamu.

Kwa sababu ndani ya chama tawala kumekuwa na mjadala kuhusu wanachama na makada wanaokosoa mwenendo wa chama au Serikali.

Katika demokrasia, kukosoa chama chako si lazima kuwe sawa na kukisaliti chama. Mara nyingi ukosoaji wa ndani ndiyo unaoweza kukifanya chama kijirekebishe kabla ya wananchi kukikataa.

Maridhiano yanahitaji zaidi ya kauli

Cha kushangaza zaidi katika mkutano huo ni kwamba wadau wengi walionekana kukubaliana juu ya hitaji la mazungumzo, lakini walitofautiana kuhusu kiwango cha mabadiliko kinachohitajika.

Othman Masoud Othman alionya kuwa Katiba ya sasa yenyewe ni tishio kwa Muungano iwapo mfumo huo hautarekebishwa. Ismail Jussa akatoa somo la Zanzibar kwamba baadhi ya maridhiano yenye mafanikio yalifikiwa kupitia mazungumzo ya ndani, bila kusubiri wasuluhishi wa nje. Haya ni masomo muhimu kwa Tanzania Bara.

Tatizo la CCM si kwamba imekataa kabisa neno "maridhiano". Tatizo ni kwamba kauli zake zinaonekana kuweka mipaka ya maridhiano kabla mazungumzo yenyewe hayajaanza.

Maridhiano ya kweli hayamaanishi CCM kukubali kila dai la upinzani. Wala hayamaanishi upinzani kushinda kila hoja.

Maridhiano maana yake ni kukubali kwamba hakuna upande mmoja unaomiliki ukweli wote, na kwamba mustakabali wa nchi hauwezi kuamuliwa na chama tawala pekee.

Ikiwa CCM inataka kuonyesha kwamba iko tayari kwa maridhiano, inahitaji kwenda zaidi ya kusema "tumeamua Katiba itaandikwa."

Inahitaji kuweka wazi ratiba, mchakato, wawezeshaji, washiriki na mwisho wa safari hiyo.

Inahitaji pia kuonyesha kwa vitendo kwamba wakosoaji wake wanaweza kuzungumza bila kuogopa, kwamba vyama vya upinzani vinaweza kufanya kazi bila kubanwa na kwamba masuala ya kisiasa yanaweza kutatuliwa kisiasa.

Kwa sasa, kauli za Wasira zinaacha picha tofauti. Zinaonyesha chama kinachosema kiko tayari kusikiliza, lakini wakati huohuo kinaonekana kutaka kiamue mipaka ya kile kinachoweza kujadiliwa. Hapo ndipo kauli ya Profesa Ichumbaki inapopata uzito: kama CCM ina mamlaka yote ya kisiasa, ni nani anayesimamia dhamira yake ya kutekeleza yale inayowaahidi wananchi?

Tanzania haihitaji ushindi wa CCM dhidi ya upinzani wala ushindi wa upinzani dhidi ya CCM bali inahitaji mfumo ambao hata CCM ikiondoka madarakani, misingi ya taifa itaendelea kusimama.
 
Attachments

  • Wasira.png
    Wasira.png
    87.7 KB · Views: 8
  • Wasira 2.png
    Wasira 2.png
    169.2 KB · Views: 14
View attachment 3666437

View attachment 3666438

View attachment 3666439

CCM ndio alpha na Omega kwenye siasa na utawala wa Tanzania. Full stop.🐒
 
Emanuel Nchimbi alishamalizq yote, CCM hawataki Katiba mpya ndiyo maana aliwasanua Watanganyika waongeze nguvu ya kuidai na ushahidi ni jinsi maccm yalivyomjia juu hadi kumfukuza kwenye chama lao la kishetani
 
Kila mtu mwenye UFAHAMU anajua CCM haitaki KATIBA MPYA..yaani hapo yenyewe wamefurahi kweli , kutokea hii hali ya mauaji, maana sasa ile AHADI ya kwamba ndani ya Siku 100, KATIBA MPYA imekufa ..
 
..Tatizo ni kwamba Ccm imepiga danadana kwenye kuongoza na kuratibu mageuzi mpaka imefika mahali imepoteza hoja zote.

..Turufu pekee ambayo Ccm inayo, ni umiliki wa vyombo vya DOLA, lakini haina hoja ya, kimageuzi, na kidemokrasia, inayotambulishwa nayo.
 
Screenshot_20260908-123557.png

Mungu chukua haya mazee now yanatakiwa kuwa KABURINI
 
Kuna watu 2 sasa ambao wamekataa taifa hili kuendelea na maigizo..Pole pole na sasa Nchimbi, kwa waliyosema watu hawa 2 sidhani unahitaji mtu mwingine ndani ya kundi hili la wahuni kukubadilisha juu ya kile walisema Polepole na Nchimbi..lbd juha ndie anaweza bado kutaka kumsikiliza wasira..
 
Wewe unataka maridhiano na nani.
 
Hoja ya Wasira tata anauliza inayohitajika ni Katiba Mpya au Katiba iliyorekebishwa? nadhani kabla ya yote ni vyema kukubaliana kuhusu dhana nzima ya katiba inayotengenezwa. Vinginevyo hakuna katiba hapo
 
Back
Top Bottom