KERO Kausha damu Banc ABC wamekataa kutoa makato yao baada ya kuwalipa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mgaa gaa upwa

Senior Member
Joined
Jan 11, 2024
Posts
180
Reaction score
281
Wasalaam.

Ni mwezi Sasa umepita tangu nilipoleta uzi hapa jukwaani unaosema

Banc ABC wamekataa kulipwa, msaada wenu unahitajika.​

Nilipewa ushauri mzuri Sana na Wana JF home of great great thinkers, niliwasiliana na BOT kweli baada ya weekend balance ya mkopo ikatoka ikiwa na limit ya wiki moja niwe nimelipa Deni.

Kama kijana mchakarikaji nilipambana Hadi nikalipa Deni lote ndani ya wiki hiyo na kupeleka bank statement (walivyoagiza).

Malipo yote yalifanyika mwanzoni mwa mwezi wa Tisa na tukaachana.

Cha kushangaza bado niliona makato yao kwenye mshahara wangu na Tena siyo kuona tu, mwisho wa mwezi wakakata mshahara wangu Kama malipo ya mkopo ule ulivyokuwa awali.

Kuwarudia wakawa wakali wananiambia nisubirie, haya Sasa Leo hii tarehe 9/10 Ina maana ikifika mwisho wa mwezi wakakata Tena pesa yangu.

Nimewarudia BOT kwa mfumo uleule wa email Cha kushangaza wanani-forwardia email waliyowatumia makao makuu Banc ABC Hadi leo kimya.

Narudi kwenu Tena lipi lifuatie maana nilishikwa na hasira Hadi nawaza kwenda mahakamani kufungua shauri la madai na wizi huu. Je kuna msaada naweza pata kutoka kwenu.

Welcome JF MEMBERS.
 
Mikopo inatu rostisha kweli watumishi mtu unaishia kuchanganyikiwa..kama mimi nina kimeo letshego faidika mpk 2026...kila siku wanataka nika top up ila nawazuga tu siwezi kujikaanga tena
 
Asante kwa kunisaidia KU-QUOTE
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Mikopo inatu rostisha kweli watumishi mtu unaishia kuchanganyikiwa..kama mimi nina kimeo letshego faidika mpk 2026...kila siku wanataka nika top up ila nawazuga tu siwezi kujikaanga tena
Aisee usije jaribu ku-top up yaani Bora ufe na tai yako shingoni tu
 
Asante nimewaza hilo kwa kuanza kufungua mashitaka mahakamani Kwanza.
Usikurupuke mwenyewe mkuu, onana na mbobezi wa haya makesi mle wote. Ukitaka kula tu mwenyewe ni tatizo. Ukumbuke vita itakuwa wewe na Bank siyo na Loan officer.
 
Asante Ila shida kumpata mwanasheria mwaminifu.

Maana huwezi fahamu anaweza kugeuka akaungana nao baada ya kupewa Cha juu zaidi.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Asante Ila shida kumpata mwanasheria mwaminifu.

Maana huwezi fahamu anaweza kugeuka akaungana nao baada ya kupewa Cha juu zaidi.
Bora kumwamini rubani usiyemjua kuliko kuendesha ndege mwenyewe bila uzoefu. Mengine unamwachia MUNGU kama ipo ipo.
 
Screenshot_20241009-201750.png
kumbe Ni kawaida yao kudhurumu watu na serikali inawaona tu.

Hivi kweli waziri wa fedha na raisi wa nchi anaruhusu watumishi kunyanyasika hivi?

Kesho, kesho Kutwa aje kutuomba kura na sisi tukimsheherekea.

Siwezi kukubaliana na Wazo kwamba hizi taasisi ndogo zinampatia hongo waziri wa fedha, sipendi kuamini hilo.
 
Back
Top Bottom