KERO Kausha damu ni changamoto kwa waalimu

KERO Kausha damu ni changamoto kwa waalimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

mwakani naolewa

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
148
Reaction score
426
Miongoni mwa changamoto nyingi zinazowakumba watumishi wa serikali ni mikopo almaarufu kama Kausha damu, ambapo inasemekana kua mikopo hiyo imekua changamoto kubwa sana kwa wafanyakazi wa serikali hasa walimu inayopelekea msongo wa mawazo na wengine kujiua.

Amezungumza hayo mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Songea Bi.Elizabeth Mathias akizungumza na watumishi wa Songea ambao ni walimu katika kongamano spesho la walimu lililoandaliwa na benki ya NMB alisema kuwa "mikopo maarufu kama kausha damu ni changamoto kubwa kwa watumishi wakiwemo walimu inayopelekea watumishi wengi kushindws kufsnys kazi kwa ufanisi na wengine kufikia hatua ya kujinyonga kutokana na msongo wa mawazo."

aidha, kuondokana na changaqmoto hiyo benki ya NMB imeamua kuja na kifurushi cha walimu spesho ambacho kitawawezesha kukopa na kuondoa changamoto nyingine za kifedha.
 
Kinachowamaliza waalimu ni taasisi za kifedha km Bayport sasa sijui na yenyewe ni kausha damu
 
Miongoni mwa changamoto nyingi zinazowakumba watumishi wa serikali ni mikopo almaarufu kama Kausha damu, ambapo inasemekana kua mikopo hiyo imekua changamoto kubwa sana kwa wafanyakazi wa serikali hasa walimu inayopelekea msongo wa mawazo na wengine kujiua.

Amezungumza hayo mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Songea Bi.Elizabeth Mathias akizungumza na watumishi wa Songea ambao ni walimu katika kongamano spesho la walimu lililoandaliwa na benki ya NMB alisema kuwa "mikopo maarufu kama kausha damu ni changamoto kubwa kwa watumishi wakiwemo walimu inayopelekea watumishi wengi kushindws kufsnys kazi kwa ufanisi na wengine kufikia hatua ya kujinyonga kutokana na msongo wa mawazo."

aidha, kuondokana na changaqmoto hiyo benki ya NMB imeamua kuja na kifurushi cha walimu spesho ambacho kitawawezesha kukopa na kuondoa changamoto nyingine za kifedha.

Bila wafanyakazi wote Tanzania(Walimu,wanajeshi, mapolisi ,askari wa magreza,migambo,JKT ,Zimamoto , wafanyakazi wa kawaida wa hamashauri, Manesi,n'k) kushirikiana pamoja kuwaondoa chawa miongoni mwao na kuiondoa CCM madarakani hali yao itazidi kuwa ngumu kutokana na tofauti kubwa sana ya mishahara inayotokana na mifumo mibovu ya kukusanya mapato na tozo iliyowekwa na wabunge waovu na watawala waovu na wabinafsi wa CCM.

Mfano : Hivi inaingia akilini kwa Walimu zaidi ya Laki tano kuwa na benki mpaka sasa isiyo na matawi mpaka wilayani ?
Haiingi akilini walimu kuwa na chama cha walimu kilichojaa viongozi machawa wa kutetea Madaraka na rais ambaye ni bilionea badala ya kutetea maslahi na lifumo bora ya maslahi ya Walimu . Utasikia Walimu machawa wa CCM Wakati huo huo Chama na benki ya walimu imekaushwa na CCM ili watu walioshiba ufisadi washinde uchaguzi waendelee kuvimbiwa na walimu wakiwa na mishahara isiyokidhi mahitaji muhimu ya binadamu wakiwa wanaishi maisha duni na kubanwa na hao hao CCM wasifundishe tuition muda wa ziada. Bila kuhoji mbona Madaktari wanaruhusiwa kutibu mitaani muda wa ziada bila kuathiri ajira zao ?
Adui wa walimu ni woga wao na kulamba viatu vya watawala kwa malengo binafsi ya machawa ndani yao.

Chama cha walimu kimekua ni chama cha kutafuta tenda za tisheti na Kofia za Mei Mosi.

Walimu amkeni.

Kataeni tisheti za mei mosi na kofia.

Pesa mnazokatwa zipelekwe Benki ya walimu ziongeze mtaji.
Benki ya Walimu Riba ipunguzwe ifikie 5% .
Wafukuzeni viongozi wote wa CWT machawa na wanaotafuta uongozi kwa malengo yao kuacha kazi ya kufundisha na kuwa makada wa CCM na kujifanya ni usalama wa Taifa.

Hawa Viongozi wengi wa CWT ni machawa . CCM imeweka wezi kila kona ya nchi hii kulinda madaraka yao, maslahi yao na ufisadi wao kila mahali.
 
aidha, kuondokana na changaqmoto hiyo benki ya NMB imeamua kuja na kifurushi cha walimu spesho ambacho kitawawezesha kukopa na kuondoa changamoto nyingine za kifedha.
Nacho kitawalamba tu, bank inataka faida
 
Back
Top Bottom