Kauza nyumba kagoma kutoka

Kauza nyumba kagoma kutoka

Mastamind

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
1,304
Reaction score
830
Mwezi Ulopita Nilinunua Nyumba 50M Kutoka kwa Mama Mmoja.

Tuliandikishana kwa Mwanasheria, lakini kipindi tushafanya malipo na tunaelekea kusaini mkataba wa mauziano aliomba apewe siku 2/3 za kujiandaa kutoka, binafsi sikuwa na shida nikamjibu tumalize hili la Kisheria tutazungumza. Tulimaliza mauziano kila mmoja akaenda na njia yake.

Ikaja wakati wa kujenga fence na ukarabati ndani, siku nimetua na mifuko yangu ya cement na vifaa vingine vya ujenzi wa fensi alinizuia nisiweke nyumba kubwa kwani hataki muingiliano na mafundi. Nikasema OK

Ikaja ishu nataka kuanza kupiga Tiles ndani nyumba kubwa, vifaa nshanunua nikamuomba nikute naanza vyumba ambavyo havitumii nako akagoma hataki muingiliano na mafundi, me nimsubiri muda wa mwezi akihama nifanye yangu. Nikasema OK vifaa nikamuomba nivihifadhi chumba nyumba kubwa akaniruhusu.

Ikaja nimekamilisha mageti ya fensi yanahitaji kuchomelewa umeme unatoka ndani kwenye main switch, akagoma napo ananikazia nisubir weekend atakayokuwa na nafasi au mpaka atakapohama.
Muda wa mwezi mmoja ninaomhesabia ni Feb 05,2022 ndipo atoke.

Msaada:
1. Hivi huu utaratibu kwake na kwangu ukoje kisheria mtu anapokuwa ameamua kuuza mali yake lakini bado anaing'ang'ania!?

2. Hivi anavyoonekana huyu mama tarehe hiyo ikifika anaweza kuhama kweli,!?? Na km akigoma nn naweza kufanya?

Ni mama ambaye haoneshi ushirikiano wowote toka tumalize mauziano

Kazi za Fensi zimesimama, za Tiles, za rangi, kifupi hakuna nachoweza kufanya kwenye huo mji kazuia mpaka aondoke
 
Inashangaza sana.

Naomba kujua machache kwenye mauziano yako na huyo mama.

Nakala za mauziano kila mtu anazo?

Upande wako na wake una mashahidi kwenye suala hilo la mauzo?

Vipi kuhusu ofisi ya mtaa au eneo lenye nyumba hiyo wanajua kuhusu hayo manunuzi?

Afya ya akili ya huyo mama inaonekanaje kabla na baada ya kuuza nyumba?

Anakaa mwenyewe humo ndani au ana familia?

Suala la kuuza nyumba hiyo lilianzia kwake au wewe ndiye ulimshawishi kuuza?

Mathalani kama documents zote za mauziano zipo na yamefanyika kwa uhalali basi wewe ndiye unatakiwa kuwa na sauti kwenye hiyo nyumba.
 
Wema usizidi uwezo, ukimchekea chekea huyo mama atakupanda kichwani. Nyumba hiyo ni mali yako sasa kisheria, huhitaji kupangiwa na mtu, ingia ndani ya nyumba yako na mfurumushe huyo mama haraka sana. Usimuonee huruma, isimuonee aibu na usimuogope.
 
Documents zote zakisheria zipo pande zote, yeye ndie alimkabidhi dalali atafute mteja na ndio akanipata
Awali alitaka nipeleka kwa Mwanasheria anayemjua, me nikasema No. Yupo homboy
Hapo anakaa na mwanaye ambaye yuko myumba ya nje
Mtaa bado kuwapa taarifa coz wao hawasimaniii mauziano
Kiafya ya akili ni timamu kwa waliokuwa nae wanamjua yuko vzur
Hati ya Nyumba, Mkataba, Bank Slip ya malipo vyote ninavyo mkuu
 
Mkuu Fanya utaratibu mapema wa kumwondoa kwa sheria kadri unavyo chelewa unatoa nafasi ya yeye kukuloga, kutumia fedha ya malipo vibaya na kuona hana pa kwenda zaidi ya kukatalia hapo

Fanya haraka mkuu
[emoji120]
 
Wema usizidi uwezo, ukimchekea chekea huyo mama atakupanda kichwani. Nyumba hiyo ni mali yako sasa kisheria, huhitaji kupangiwa na mtu, ingia ndani ya nyumba yako na mfurumushe huyo mama haraka sana. Usimuonee huruma, isimuonee aibu na usimuogope.
[emoji120]
 
business carriage transfer of possession ishamaha kwako since sales contract ishafanyika na malipo tayar sio agreement we tumia ubinadamu then shusha kibano siku zikiisha ushajua tabu yake

sema nyumba zina mengi usimchukize yatwakuta yale unaanza tu kukaa daily mnepelekewa moto watu wakati wanaanza kukaa wana mazindiko yao atatoka tu usiwaze

ila chunga sana
 
Mwezi Ulopita Nilinunua Nyumba 50M Kutoka kwa Mama Mmoja.
Tuliandikishana kwa Mwanasheria, lakini kipindi tushafanya malipo na tunaelekea kuasain mkataba wa mauzioano aliomba apewe siku 2/3 za kujiandaa kutoka, binafs sikua na shida nikamjibu tumalze hili la Kisheria tutazungumza.
Tulimaliza mauziano kila mmoja akaenda na njia yake,
Ikaja wakati wa kujenga fence na ukarabati ndani, siku nimetuwa na mifuko yangu ya cement na vifaa vingne vya ujenzi wa fensi alinizuia nisiweke nyumba kubwa kwani hatak muingiliano na mafundi.
Nikasema OK
Ikaja ishu nataka kuanza kupiga Tiles ndani nyumba kubwa, vifaa nshanunua nikamuomba nikute naanza vyumba ambavyo havitumii nako akagoma hataki muingiliano na mafundi, me nimsubiri muda wa mwezi akihama nifanye yangu. Nikasema OK vifaa nikamuomba nivihifadh chumba nyumba kubwa akaniruhusu.
Ikaja nimekamilisha mageti ya fensi yanahitaji kuchomelewa umeme unatoka ndani kwenye main switch, akagoma napo ananikazia nisubir wikend atakayokua na nafas au mpk atakapohama.
Muda wa mwezi mmoja ninaomhesabia ni Feb 05,2022 ndipo atoke.

Msaada:
1.Hivi huu utaratibu kwake na kwangu ukoje kisheria mtu anapokua ameamua kuuza mali yake lakin bado anaing'ang'ania!??

2.Hivi anavyoonekana huyu mama tar hyo ikifika anaweza kuhama kweli,!?? Na km akigoma nn naweza kufanya,!??
Ni mama ambaye haonyeshi ushirikiano wowote toka tumalze mauziano
Kazi za Fensi zimesimama, za Tiles, za rangi, kifupi hakuna nachoweza kufanya kwenye huo mji kazuia mpk aondoke
Huyo mama ni mchawi, jihadhari, atakuroga umuoe, uisahau familia yako
 
Nenda kamfungulie kesi na uombe maombi yakumtoa
 
Fata taratibu umuondoe aisee hapo ni kwako na inaonekana una ustaraabu flani which is good kwa binadamu ila aistake advantage ya wema unaomuonesha maana hata hiyo pesa uliyotoa na gharama utazoingia ni kubwa ila kaa nae afu muoneshe upande mwingine ulio nao no fear !!
 
Anzia serikali ya mtaa, uwaeleze changamoto zako, ingawa mwanzoni hukuwashirikisha ila jaribu kuwaona unaweza kupata pa kuanzia. Ikishindikana, dai akurudishie pesa yako pamoja na fidia ili umuachie nyumba yake.
 
We jamaa ushauri umepewa mrejesho hutaki kutoa.

Hebu Tuambie ulitumia njia gani kumuondoa kama alikataa kutoka!? Ama alitoka tu kwa hiyari yake.
 
Back
Top Bottom