Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohammed Ali Kawaida, amesema kuwa tarehe 26 Aprili 1964, wazee wetu walichanganya udongo kama ishara ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hatua iliyozaliwa taifa moja la Tanzania.
Ameongeza kuwa vizazi vilivyofuata vimeendelea kuchanganya damu kwa kuoa na kuolewa baina ya pande mbili za Muungano, kama sehemu ya kudumisha na kuimarisha mshikamano huo wa kihistoria.
Mwenyekiti Kawaida ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Bukombe, katika ziara yake inayolenga kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa mujibu wa Ilani ya Chama, pamoja na kuzungumza na viongozi na wananchi.
Amesema kuwa lengo kuu la Muungano ni kuimarisha undugu na mshikamano wa watu wa asili inayofanana, pamoja na kulinda usalama wa taifa.
Aidha, Mwenyekiti Kawaida amewasihi Watanzania wote kuendelea kulinda na kuuenzi Muungano huo kwa nguvu zote, akisisitiza kuwa yeyote anayetaka kuubeza au kuudhoofisha Muungano, ni adui wa taifa na hastahili kupewa nafasi yoyote katika jamii inayopenda amani na maendeleo.