St Lunatics
JF-Expert Member
- Aug 29, 2015
- 6,644
- 11,174
Jana nilikuwa naranda na rafiki yangu sehemu tofauti tofauti mara akatokea mdada mzuri sana, nikajitambulisha jina langu na yeye akaniambia jina lake. Bila ya kuchelewa nikamuomba nitoke nae twende movie akaniambia kuwa amepanga na shoga zake kutoka jana jumamosi lakini yupo free jumapili. Nikamwambia basi tutoke kesho nipatie namba yako tupate kuonge vizuri akasema sawa lakini nifuate pale nitakupatia namba yangu. nilishangaa kwanini mpaka nimfuate anapopataka ndio anipe namba? Sijataka kuuliza hilo suali lakini baada ya kama dakika tano(5) nikamfuata alipo kufika naona shoga zake kama sita wananiangalia machoni kuna wengine wanatabasamu wengine wanatikisa kichwa juu chini na huyu mmoja akamwambia amepasi. Suali langu kwa wadada mpaka shoga zenu waseme anafaa ndio mutukubali?