Kawambwa akerwa daraja la tano kuitwa sifuri - [division five]

Kawambwa akerwa daraja la tano kuitwa sifuri - [division five]

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
images



Dodoma.Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa ameelezea kukerwa na daraja la tano katika muundo mpya wa kupanga matokeo, kuitwa sifuri.
Dk. Shukuru Kawambwa, aliyasema hayo jana mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Alivishutumu vyombo vya habari kwa kuchanganya alama na madaraja yaliyopo katika muundo mpya wa kupanga matokeo ya mitihani nchini.
Alisema kwa muundo mpya, daraja sifuri ni kati ya pointi 48 na 49 ambayo inapatikana baada ya mtahiniwa kupata alama F kwa masomo yote saba.
¡°Ndugu zangu waandishi wa habari, kitu ambacho hamkufanya haki kwa Watanzania safari hii, ni ile kuliita daraja la tano kuwa ni sifuri mkalazimisha na mimi kumwagiza Katibu Mkuu abadilishe na kuita daraja sifuri,¡± alisema na kuongeza:
¡°Unakuaje na daraja la kwanza, la pili, la tatu, la nne lakini unapofika la tano unaita sifuri katika namna ambavyo waandishi wa habari walipenda.¡±
Dk Kawambwa alisema vyombo vya habari vimekuwa vikipenda taswira ya nchi ionekane kuwa ni kufeli. ¡°Lakini ninachosema ni kwamba, pointi ni zile zile tulichoondoa ni daraja la tano.¡±



Chanzo: MWANANCHI
 
Upuuzi mwingine huuu wa watawala wachezea elimu na maisha ya watanzania wakati hana hata mtoto mmoja anayesoma shule za tanzania wote wapo mombasa na malaysia.Tunahitaji mchakato wa elimu mpya kama tunavyofanya ktk katiba mpya.Pia kwa nini hamtaki kuanzisha Tanzania Education Regulatory Authority?kila mwaka, kuanzia rais mpaka waziri mnadanganya tuu
 
Mulugo.jpg




"Naibu waziri Philiph Mulugo - mwaka jana"
Wanafunzi.jpg



"Baada ya ishu ya division five kuchukua headlines, hii ni kauli mpya kutoka Wizara ya elimu"



Elimu ya Tanzania iliingia kwenye headlines siku kadhaa zilizopita baada ya kutangazwa kwamba hakutakua na division zero na badala yake kutakua na division five kwa Wanafunzi wanaomaliza elimu ya sekondari.

November 4 2013 Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philiph Mulugo aliongea kwenye vyombo vya habari na kusema ¡®taarifa zilizotolewa awali zilikosewa kidogo kutokana na mkanganyiko sababu ishu ilikua bado iko kwenye mjadala lakini nataka nikuhakikishie kwamba kutakua na division 1, 2, 3, 4 na kutakua na division zero kama kawaida, haijaondolewa¡¯
¡®kinachofanyika tu hapa ni zile point kutanuka baada ya kutoa yale madaraja zile alama kurundikana sehemu moja, tumezihamisha angalau alama zipishane alama 10 mpaka 15 kwa hiyo F itakua ni 0-19 na daraja jingine lililoongezeka pale ni E ambalo 20-29 alafu daraja la D kutakua alama 30 -39, C ni 40 mpaka 49, B ni 50 mpaka 59, B ni 60 ¨C 74 alafu A ni 75 mpaka 100¡ä ¨C
 
Upuuzi mwingine huuu wa watawala wachezea elimu na maisha ya watanzania wakati hana hata mtoto mmoja anayesoma shule za tanzania wote wapo mombasa na malaysia.Tunahitaji mchakato wa elimu mpya kama tunavyofanya ktk katiba mpya.Pia kwa nini hamtaki kuanzisha Tanzania Education Regulatory Authority?kila mwaka, kuanzia rais mpaka waziri mnadanganya tuu
Nakubaliana nawe Mkuu, hii elimu inakuwa kama kichwa cha mwendawazimu kila mmoja anaamua vyake. Ina maana huyo Kawambwa hajui hata vigezo vilivyotumika? Anadai zero inaanzia pointi 48 wakati wapo hata waliopata pointi 41 wana 0? Hii ni hatari sana
 
Nipo kwenye mchakato wa kuomba uraia hapa Kenya ili angalau watoto wangu wapate elimu iliyo na mashiko. Unawaonea watu huruma kwenye Elimu? Halafu iweje? Pumbavuu. Unamaanisha mtoto akipata 0 aandikiwe dv5? Utakuwa umemsaidiaje kwa hilo? Upuuzi huo. Huku kenya watu wako na msimamo kwenye elimu. Upuzi ndo hawataki. Mhandisi mnamfanya waziri wa elimu? Hapo hakuna ujenzi ni ubomoaji. Shenzi type A+
 
Back
Top Bottom