Kawambwa et al: Tuelezeni bil. 12 mmezitumiaje?

Kawambwa et al: Tuelezeni bil. 12 mmezitumiaje?

Jafar

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2006
Posts
1,136
Reaction score
54
Leo hii bado siku 39 mashindano ya kombe la dunia yaanze huko bondeni. Ninachotaka ile kamati ya Waziri Kawambwa itueleze zile bilioni 12 za kuhamasisha utalii (wakati yeye si waziri wa wizara hiyo) wakati wa kombe hilo mpaka sasa:
1. Mipango na hali halisi wamefikia wapi
2. Ni kiasi gani wameshatumia na kufanyia nini
3. Nini tutarajie kutoka kwenye kamati hiyo
4. Wapi wameshindwa
5. Faida ya ujumla ya mpango huo
6. Mbona hutusikii timu yeyote kuja kwenye joto la Dar kufanya mazoezi? (kumbuka SA wakati huo ni kibaridi cha kufa mtu)

Wasije baada ya mashindano kumalizika ndio wanatuambia eti haikuwezekana.

Naomba kutoa hoja.
 
Wamezitumia kwenye kuandaa upembuzi yakinifu, the kwa semina elekezi, then kwenye warsha ya mrejesho then wakamalizia na mkutano wa wadau wote, hela imeisha.
 
Wamezitumia kwenye kuandaa upembuzi yakinifu, the kwa semina elekezi, then kwenye warsha ya mrejesho then wakamalizia na mkutano wa wadau wote, hela imeisha.

Duh kazi kweli kweli.
 
hivi kawambwa ndo mkiti wa hiyoo kamati?????

ama kwa hakika tatizoo letu ni zaidi ya tujuavyoooooooooooooooo....nijuzeni sifa ya yeye kuongoza kamati hiyoo!!!!
 
Wamezitumia kwenye kuandaa upembuzi yakinifu, the kwa semina elekezi, then kwenye warsha ya mrejesho then wakamalizia na mkutano wa wadau wote, hela imeisha.

Umesahau na kongamano la MAJUMUISHO YA SEMINA-pesa kwishnei
 
Huyu ni laana ya serikali ningekuwa kanisan ningemuita msukule wa jk
ameshindwa kueleza zile million 100 za kamati ya kuchunguza atcl zimeendaje na ripoti kaiweka chumban kwa mkewe awe anaiangalia mara kwa mara....kwa hiyo msiumize sana kichwa na huyu ndie ndondocha wa jk...mjomba mjomba jamani
 
Back
Top Bottom