Kawambwa kakosea hesabu au vyombo vya habari vimemnukuu vibaya?

Tuko

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
11,180
Reaction score
7,346
Nanukuu kutoka kwenye gazeti ka mwananchi

"...MATOKEO ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yametangazwa. Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, ...
Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisema watahiniwa walikuwa 456,137..."

Hii 60.6% inatoka wapi?
Maana 240903/456137 x 100% = 52.8%

Nimeona hata baadhi ya vyombo vingine vya habari vimeripoti namba hizo hizo...

Someone to clarify?...
 
Huyu jamaa ni kimeo, nakumbuka swala la mitaala, akakanusha, lakini cha kushangaza mkurugenzi wa taasisi ya elimu akajiuzulu, sasa kwanin alijiuzulu , kama kweli ile mitaala ilikuwa halali?
 
Hata kama ungekuwa ni ww lazma uchanganyikiwe......hari mbaya
 
Mkuu usishanagae kwani ingekuwa 52% wamefeli unafikiri haya ni matokeo mazuri. Kwa mtazamo wangu wote waliopata DIV 0 na IV wote wamefeli ukitafuta wastani utakuta waliofeli ni 94% na waliofaulu ni kama 0.43% aibu kubwa ndugu zangu. Hili ni janga lingine la kitaifa. Haya pia ni matokeo ya serikali kupuuza matakwa ya waalimu. Bila CCM kutoka madarakani hakika tutaendelea kuumia milele. Wote tukatae hili 2015 tufanye mabadiliko maana kila sehemu tunaumizwa na hii serikali ya CCM.
 
Nilikuwa najaribu kupata takwimu kwenye website ya NECTa lakini haifunguki.
Kwa haraka haraka nilihisi kuwa huenda hiyo 456,137 ni registered candidates, na kwa kuwa huwa wanakuwapo some absent students, huenda waliofanya mtihani ni less than registered students, so kama denominator itakuwa less than 456,137 basi hata percentage itapanda juu kidogo na kufikia hiyo 60.6%. Ni hisia tu, ningepata figure zote ningejiridhisha, ila sasa website ya matokeo haifunguki
 
Masahihisho: Waliopata ZERO ni 68.1% na sio 60%. Calculation zinatokana na school candidates waliofanya mtihani na sio waliojiandikisha kufanya mtihani.

Toka Gazeti la Mwananchi.

Alisema watahiniwa wa shule (school candidates) walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57, miongoni mwao, 14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo utoro, ugonjwa na vifo.


Ufaulu kwa madaraja
Kwa mujibu wa matokeo hayo, watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni 1,641, wavulana wakiwa 1,073 na wasichana 568, daraja la pili ni 6,453, wavulana wakiwa 4,456 na wasichana 1,997.


Waliopata daraja la tatu ni 15,426, wavulana 10,813 na wasichana 4,613, waliopata wa daraja la nne 103,327, wavulana 64,344 na wasichana 38,983 huku waliopata sifuri wakiwa 240,903, wavulana 120,664 na wasichana 120,239.

Kwa watahiniwa wa shule(school candidates) waliofanya exams walikuwa 397,136, I=1,641, II=6,453, III=15,426, IV=103,327. Jumla ya I-IV=126,847; Hivyo basi Zero ni 397,136 - 126,847=270,289. Hivyo asilimia ya ZERO ni 68.1. Ukichanganya ZERO na IV ni asilimia 94.1, ikiwa na maana kuwa waliopata I-III ni 5.9%.

 
Tuko!
Unamatatizo makubwa;
Unamkosoa Daktari wa falsafa?
Mhadhiri wa Chuo Kikuu?
Kitivo cha uhandisi;
Mhandisi ndiye mtaalamu wa mahesabu/hisabati
Unaamua kumdhalilisha ------ wa Bagamoyo;
Aliyeshindwa kujenga barabara ya kwao (Bagamoyo - Msata)?[INDENT Tuko huna nidhamu kabisa.

Bazazi!
[/INDENT]
 
Last edited by a moderator:
Pity shame, Hapa ndo tunamkumbuka Mbatia, yaani kaja na mswaada wa kuboresha Elimu magamba wa kaupiga chini, Watanzania tuwe makini hakuna nchi inaweza kufelisha hivi yaani waliofaulu ambao wanaweza kwenda kidato cha tanoi ni 5.9% na hii yote 94% ieende mtaani hili ni bomu tumelitengeneza. Waziri wa Elimu hatakiwi kukaa pale ! Aibu aibu aibu
 
Yaani hii kitu sio ya kuchekelea hata kidogo ulivyojichanganya hapo kwenye RED ndo hivyo hivyo Kawambwa nae kajichanganya usipime yaani 94% wamefeli? kudagadeki mwakaa jana ilikua 91% tutegemee mwakani kuwa 97% baada ya hapo 2015 watakaofeli watakua 100% hii ndo nchi Kikwete anatuachia, na hii EAC kudagdeki watotot wetu watakua manamba tu kwenye Ardhi yao !
 
mkuu uko sahihi vijana wamefail sana ni aibu sana kwa taifa letu siasa ni adui wa elimu yetu. Na cha ajabu sana hakuja hata na solution ya nini klifanyike. nilitegemea ameona wananfunzi wamefail sana sasa kama waziri mwenye PhD holder angekuja na nini kifanyike na sikutangaza tu na kualalamika kuwa shule hazikuwa na walimu, maabara, na pengine bila kujua kiini hasa cha tatizo.
Kwa mfano mimi naona tatizo liko kwenye kudahili wanafunzi wa darasa la saba wengi wanaochanguliwa kwenda sekondari ni wale walio fail eg. mwaka huu kunawanafunzi wameingi form 1 wakiwa na wastani wa 30% yaani 15/50 tujiulize kwa huyu mwanafunzi akiingia sekondari anakumbana na changa moto za lugha na mengine kuja kuendana na mazingira inakuwa amefika form 4 na ndio matokeo yake ndio hayo
pili swala la fimbo primary jamani kwa maoni yangu zirudishwe maana mwalimu anashindwa hata jinsi ya kumsaidia mtoto maadili yetu yamebadilika sana watoto hawataki kusoma na mwalimu hana jinsi ya kumlazimisha ili asome
tatu nibora wanafunzi walio fail wapelekwe vyuo vya ufundi agalau wanaweza pata kitu cha kusaidia katika maisha yake
 
Duh haya bana sijui watafanya nini aiseee
Kwani bado kuna vyuo vinayvochukua wenye zero?

Aibu sana yaani 5.6% ndio wamefaulu hakika kazi ipo
Huko mbele tutakapotaka kwenda ngumu sana kufika kwa huu kwenda bora tubadili madarasa tufuge kuku kama hawawezi badili mambo
 
Itasaidia?
Kehasema wasichana wamefeli sababu ya wanamme!
 
Unaamua kumdhalilisha ------ wa Bagamoyo [/INDENT]

WanaJF!
Napenda kufahamu hivi jina la kabila hapa JF ni matusi;
Hapo kwenye vidashi niliandika kabla la mhe Waziri wa elimu:
Naomba kufahamishwa nisije nikala BAN kwa kuandika makabila ya watu.​
Je ni makabila yote au ni kwa kabila la KWE.RE tu ndio ambalo linakuwa censored.


Nawasilisha;​
Bazazi!
 

ndio mkuu tusi kwa mujibu wa mods!!!!!!!!!!!!
 
Tujifunze kwa walioweza,tujiulize kwa zile shule za st zilizofaulisha wao walifanya nini mpaka kufaulisha vizuri,kama shida ni kwenye udahili wa wanafunzi basi tuchukue wale walio bora tu ndio waingie form one,pia mitihani ya form two irudishwe haraka.Poleni sana wanafunzi na wazazi ambao wanenu wamezungusha.
 
Ni kweli ni asilimia 52.813...% hata hivyo hata hawa waliofaulu ni "thekyu vere mechi"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…