capacity 0GB
Member
- Jul 6, 2020
- 43
- 52
KAWE INA HESHIMA TAYARI, INAHITAJI MAENDELEO
Je, ni kweli Kawe inahitaji heshima?
Jimbo la Kawe ni moja kati ya majimbo muhimu sana hapa Dar es Salaam.
Kule Masaki na Oysterbay wanakaa watu muhimu katika taifa. Mabalozi wengi wanakaa jimbo la Kawe.
Vitengo muhimu kwa ustawi wa nchi viko kwenye jimbo la Kawe.
Kwa upande wa makazi pia, maeneo ya Mbezi Beach, Mikocheni, Bunju, Goba, Salasala, Madale yote haya yamejaa watu wa maisha ya kati na juu ambao wana mchango mkubwa katika taifa hili. Haimaanishi watu wengine sio muhimu, kila mtu ni muhimu kwa kiwango chake kulingana na nafasi aliyopo.
Kwa mtazamo huu, jimbo la Kawe tayari lina heshima. Jimbo la Kawe halikutakiwa kuwa jimbo la watu wanaolalamika kwa kukosa huduma muhimu kama barabara za ndani, hospitali na maji. Kawe ina heshima ndio maana wakazi wa huko wamekuwa wastaarabu sana kipindi hiki chote cha miaka 10.
Kwa heshima iliyonayo jimbo la Kawe, mwakilishi wake angekuwa ameweka mbele maslahi ya jimbo lake kwa kutanguliza hoja za wananchi na sio kulalamika bungeni na kugoma.
Yaani baada ya miaka 10 Mdee ndo amejua kuwa Kawe inahitaji heshima?
Heshima gani wakati watu hawana maji kule Ndumbwi?
Heshima gani wakati madaraja hayajaisha huko Boko? Mbezi Beach na Mbezi juu imejaa barabara za vumbi? Heshima gani hiyo?
Heshima gani wakati fedha za mfuko wa jimbo zimetafunwa?
Heshima gani wakati mwakilishi aliyechaguliwa na watu wa Kawe anaongoza migomo bungeni?
Watu wa Kawe wana heshima, ila kwa aliyoyafanya Mdee kwa miaka 10 amewadharau sana.
Watu wa Kawe msirudie makosa haya.
Mmemstahi sana huyu Mdee kwa miaka hii 10.
Safari hii mchague Askofu Gwajima mtu makini anayejua wanachohitaji wananchi wa Kawe.
Ni wakati wa kuachana na longo longo na kuchagua mtu jasiri, hodari, mchapakazi na mpenda maendeleo atakayeishawishi serikali kuleta maendeleo kwenye jimbo la Kawe.
Wanakawe achaneni na Mdee, hajawaheshimu miaka 10 yote hii, ataweza kwa miaka hii mitano (5)?
Mchague Gwajima kwa maendeleo ya Kawe na Magufuli kwa Maendeleo ya Tanzania atunze heshima mliyonayo.
Salum Kipanga
Mbezi - Mtoni,