Uchaguzi 2020 Kawe ina heshima tayari, inahitaji maendeleo

Kwa sasa wanaKawe tunahitaji mtu atakaye tuwakilishia kero zetu na zikatekelezwa
 
Mwanzoni nilikuwa naipenda chadema sana lakini jambo moja nimegundua huwezi kupenda kitu kwa muda mrefu kama akikupi faida yoyote, miaka kumi ya changamoto imetosha.
 
Gwajima ndo chaguo la Wanakawe. Mdee amefanya nini kwa miaka 10 kama sio migomo na kelele bungeni.
 
hili
haswaaaa heshima ipo na tunataka maendeleo barabara ,vituo vya afya, mashule, ambulance ndio tunataka kwa sasa
 
Halima umejua leo kama kawe inastahili heshima baada ya miaka kumi [emoji1787][emoji1787] umechelewa sasa hivi tunaenda na Gwajima hata ufanyeje wanaKawe hatutabadilisha msimamo wetu
 
Pole sana dini zote zilimkuta mwanadamu kwa hiyo sioni sababu ya Gwajima kutokuwa mbunge kawe ,ngoja tusubiri tarehe 28 itazungumuza yenyewe.
 
Halima unayemtetea hajafanya lolote kwenye jimbo la Kawe, kaishia kugoma tu.

Barabara za Mbezi Juu, Wazo na Madale hazipitiki.

Hela za mfuko wa jimbo haifahamiki zimetumikaje...

Mdee unamshabikia kwa mazuri yapi?
 
Kawe tunataka maendeleo na wa kuyaleta ni Gwajima awamu hii tunakwenda na Gwajima

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Kawe tunahitaji mtu kama Gwajima ili iendelee kuwa na heshima ikiambatana na maendeleo.
 
Halima unayemtetea hajafanya lolote kwenye jimbo la Kawe, kaishia kugoma tu.

Barabara za Mbezi Juu, Wazo na Madale hazipitiki.

Hela za mfuko wa jimbo haifahamiki zimetumikaje...

Mdee unamshabikia kwa mazuri yapi?

..serikali nzima na wakubwa wote nchi hii wanaishi jimbo la kawe.

..sasa ilikuwaje wasipeleke maendeleo huko? au walikuwa wakifanya hujuma?

..fedha za mfuko wa jimbo matumizi yake yanasimamiwa na mkurugenzi wa wilaya, ambaye ni mteule wa ccm.

..Tuikatae ccm kwa kulibagua kimaendeleo jimbo la kawe.

..Tumkatae Gwajima kwasababu ni TAPELI. Aliahidi kumfufua Amina Chifupa. Aliahidi kununua treni. Atimize ahadi hizo kwanza ndipo tuamini kwamba anaweza kutimiza ahadi za ubunge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…