LGE2024 Kayandabila: Uchaguzi hauna uzoefu, fuateni mafunzo ya Uchaguzi wa mwaka huu

LGE2024 Kayandabila: Uchaguzi hauna uzoefu, fuateni mafunzo ya Uchaguzi wa mwaka huu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wasimamizi wasaidizi zaidi ya 600 wa vituo vya kupiga kura uchaguzi Serikali za Mitaa wa jimbo la Tabora wametakiwa kutokutanguliza uzoefu wa usimamizi wa chaguzi zilizopita katika uchaguzi wa mwaka huu badala yake wafuate mafunzo na mwongozo wa usimamizi wanaopewa ili kuweza kufanikisha zoezi hilo kwa uadilifu na amani.

Mkuu wa uchaguzi jimbo la Tabora, Elias Kayandabila ametoa rai hiyo wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wasiidizi wa vituo vya kupiga kura yaliyofanyika mkoani Tabora kwa lengo la kuwajengea uelewa wasimamizi, ambapo yameambatana na kiapo cha uadilifu kwa wasimamizi hao.

Kayandabila amesema kutokana na wengi wao kuwa na uzoefu wa kusimamia chaguzi zilizopita wasitumie uzoefu huo katika uchaguzi wa mwaka huu kutokana na baadhi ya taratibu za uendeshaji wa zoezi hilo kubadilika kwa kiasi kikubwa.

Naye Mratibu mkuu wa uchaguzi mkoa wa Tabora, Elihuruma Nyerra amewataka wasimamizi wa vituo vya kupiga kura kutenda haki na kutanguliza weledi katika kusimamia zoezi hilo ili kuepusha changamoto zinazo weza kujitokeza kutokana na kukusa weledi.

Nao, baadhi wa wasimamizi wa vituo vya kupiga kura, Samwel Nkungu na Joseph Thomas wameahidi kwenda kusimamia zoezi hilo kwa weledi mkubwa kwa kufuata maelekezo na mafunzo waliyopewa ili kukamilisha zoezi hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
 
Back
Top Bottom