Pre GE2025 Kazi anazofanya Rais Samia kwa wananchi, hazimpi uhakika wa kurudi Ikulu? Nauliza, pikipiki zina lengo gani kwa wapiga kura?

Pre GE2025 Kazi anazofanya Rais Samia kwa wananchi, hazimpi uhakika wa kurudi Ikulu? Nauliza, pikipiki zina lengo gani kwa wapiga kura?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Bulelaa

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
1,342
Reaction score
3,247
Wana lumumba mpogo?

Kazi nyingi asifiwazo Rais mtukufu wetu mama Samia, mmezipima mkaona hazitoshi kuwashawishi wananchi kumrudisha Ikulu siyo?

Hizo pikipiki mamia kwa mamia zilizoandikwa kwa jina la Samia 2025, wazalendo watumie jina gani kuziita

Ni zawadi au nini?

Ni rushwa kwa wapiga kura au takirima na au nini hasa?

Kwanini isitoshe kuziamini kazi zake mnazozisifia kwamba zimewagusa wananchi na zitoshe kumpa kura tena?

Kwani mnamashaka tena na kazi zake mnazotuorodheshea kila leo hapa jf, kwamba mama kawazidi marais wote kwa kazi zilizotukuka na kwamba anaupiga mwingi?
 
Wana lumumba mpogo?

Kazi nyingi asifiwazo Rais mtukufu wetu mama Samia, mmezipima mkaona hazitoshi kuwashawishi wananchi kumrudisha Ikulu siyo?

Hizo pikipiki mamia kwa mamia zilizoandikwa kwa jina la Samia 2025, wazalendo watumie jina gani kuziita

Ni zawadi au nini?

Ni rushwa kwa wapiga kura au takirima na au nini hasa?

Kwa nini isitoshe kuziamini kazi zake mnazozisifia kwamba zimewagusa wananchi na zitoshe kumpa kura tena?

Kwani mnamashaka tena na kazi zake mnazotuorodheshea kila leo hapa jf, kwamba mama kawazidi marais wote kwa kazi zilizotukuka na kwamba anaupiga mwingi?
Tuambiane tu ukweli hakuna kitu kitamrudisha ikulu zaidi ya Tume isiyohuru.

The rest tuendelee na maisha tu.
 
Haya majangili yote ya mali za umma karibu yote yamesoma bure wakati wake, alishindwa ni nini kuacha katiba bora wakati wa uongozi wake?
Sasa amefanya mazuri yote hayo Bado unamdai Katiba mpya ilhali Hilo unaweza kuifanya wewe?

By the way, Mzee Warioba ni kijana wa Nyerere na amekwisha fanya KAZI iliyotukuka.
 
Hebu acha lawama kwa huyu marehemu.. Hiyo katiba mmeshindwa nini kuibadilisha..
Hizi ndio kumlaani babu mzaa babu yako sababu alikuwa na chogo alilokuachia wewe unalaumu kasababisha wajukuu zako kupata chogo wakate wewe ulikuwa na opportunity ya kudilute genes hizo mbovu kwa kutafuta mlimbwende asiye na chogo kuliko huyu uliyenae sasa mwenye chogo....

Vilevile unasahau enzi zile chogo labda ilikuwa ndio fashion...
 
Mkuu, heshima kwako boss!

Tumekubaliana kwamba, sio muda wa kulaumu yaliyopita, ni muda wa sisi kuyakabili uso kwa uso kwa yanayotukwamisha
Ni mgumu sn sababu watawala inawapa mwanya wa kuiba mali za umma bila kusumbuliwa na yeyote, wote wana kinga
 
Back
Top Bottom