Kazi bado ipo, hata vita isimame leo bado itachukua muda mrefu bei ya mafuta na nishati kurudi katika hali ya kawaida

Kazi bado ipo, hata vita isimame leo bado itachukua muda mrefu bei ya mafuta na nishati kurudi katika hali ya kawaida

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
17,595
Reaction score
39,893
Moja kwa moja.

Watu wengi wanadhani vita ikiisha basi maisha yatarudi kawaida na bei za mafuta katika soko la Dunia zitashuka na kurudi katika hali ya kawaida.

Msichokijua kwamba atahari ya hii vita zinaweza kuchukua muda mrefu kwani baadhi ya mashambulizi yameharib kabisa miundombinu ya kuchakata mafuta na miundombinu ya uzalishaji wa gesi . Mfano Qatar wamesema Kwamba itachukua miaka kama mitatu kurekebisha baadhi ya mitambo.

Na hapo bado hatujui kichaa Trump ataamka na mood gani siku zijazo , maana anatishia kulipua miundombinu ya umeme , gesi na mafuta yote ya Iran kwa siku zijazo na MuIran kama mnamjua hachekeshi hawezi Kukubali afe kizembe peke yake atalipua viwanda vyote na miundombinu ya mafuta na gesi middle east kitu ambacho kitapelekea uhaba wa mafuta mkali zaidi kuwahi kushudia Duniani na tutarudi zama za mawe.

Dunia nzima sasa kumechafuka mpaka Ulaya wanalia bei ya mafuta na mafuta ni ghali na Urusi jana kapiga ban hakuna gasoline kuuzwa nje ya Urusi.

Yajayo yanafurahisha Trump na Netanyahu wameingiza Dunia katika hekaheka mpya.

images (32).jpeg

#UziTayari
 
Wamarekani wameshaanza kuamka , wengi hawaelewi sababu ya Rais wao Kukubali kuwaingiza katika vita ambayo haina maslahi kwa US wanaona viongozi wao wanafanya kazi kwa maslahi ya nchi nyingine.

Unaanbiwa kila Rais wa US akiingia Madarakani Waziri mkuu wa Israel anakuja kuomba avamie na kupiga mabomu Iran na wamekuwa wakikataa mpaka mwaka huu Netanyahu amemuokota Trump ametii na ametekeleza .

Wafununu wanadai huenda Trump ametishiwa maisha na Mafia wa Israel kuwa watamfanyia kama alivyofanya Rais Jf Kennedy au mwanaharati Charles Kirk kwa kumuAssasinate au wanemtisha kumfichua skendo zake chafu kwenye maFile ya episten hapo Mzee Trump akawa mnyonge na Kukubali tu
images (37).jpeg
 

Attachments

  • images (37).jpeg
    images (37).jpeg
    23.9 KB · Views: 24
Ndiyo tukaambiwa tusikate miti ovyo , sasa tutaona faida ya kutumia kuni na hasara ya kukata miti. Ile migodi ya mkaa wa mawe ya Marehemu Mkapa alirithi nani ???
 
Trump na netapaka watakufa vifo vibaya sana, kama ilivyo kwa eriel sharon basi huyu kaafir mwenzie anaelekea huko huko.

Iran shikilia hapo hapo mpaka israel warudi walikotoka na kuwaachia waarabu ardhi yao
 
Back
Top Bottom