Kazi: Goli la Geita gold dhidi ya Yanga ni offside

Kazi: Goli la Geita gold dhidi ya Yanga ni offside

Ktk kipindi cha kipyenga cha mwisho kinachorushwa na Azam sports 1 HD, refa mkongwe Othman Kazi amefafanua kuwa mfungaji wa goli la Geita vs Yanga alikuwa ameotea. Pia, penati ya Yanga haikuwa sahihi japo walinyimwa penati nyingine ktk tukio la Ngushi kusukumwa. Tukio pa penati iliyokataliwa lilitokea sekunde chache kabla ya penati ya uongo
Lile goli la geita lilikuwa offside kabisa; hata mimi niliona hivyo. Goli la penalti kwa Yanga lilikuwa sahihi kabisa; kama uliangalia mechi yamarudiano baina ya Real Madrid na Chelsea, utaona goli lililokuwa liwe la tatu kwa Chelsea lilikataliwa kwa vile mpira ulikuwa umegusa mkono wa mfungaji katika mazingira kama ilivyotokea kwa yule mlinzi wa Geita; in fact ilibid warudie playback kwenye AVR na kuona kuwa kweli mpira uligusa mkono wake. Ni contact iliyoleta advantage kwa mchezaji aliyehusika kwani contact hiyo ilifanya mpira ama umfikie yeye vizuri mguuni au usimfikie mpinzani wake vizuri wakati mpira uko kwenye eneo la hatari. Ukimgusa mkononi ukapotelea kwa mpinzani kunakuwa hakuna tatizo.
 
Kwanini wengine wanaiona penati ya yanga si halali?
Yule beki wakati anaokoa ule mpira ulimgonga kwa nguvu mkononi ndani ya box tena golini haswaa sasa kwanini isiwe penati?
 
Ktk kipindi cha kipyenga cha mwisho kinachorushwa na Azam sports 1 HD, refa mkongwe Othman Kazi amefafanua kuwa mfungaji wa goli la Geita vs Yanga alikuwa ameotea. Pia, penati ya Yanga haikuwa sahihi japo walinyimwa penati nyingine ktk tukio la Ngushi kusukumwa. Tukio pa penati iliyokataliwa lilitokea sekunde chache kabla ya penati ya uongo
Hayo Sasa Ndio yanaitwa gold goals🤸🤸
 
Back
Top Bottom