Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wote waliopo huitikia kwa nguvu kazi iendeleee. Nimekaa na kuutafakari huu msemo nimeona kama ni wa kisiasa zaidi.
Unakwepa kuwa na commitment kwenye maisha ya Watanzania milioni 60, ni kama vile ikifika wakati wa Rais kuulizwa kafanya nini aweze kujitetea kirahisi tu kwa kusema niliwaambia kazi iendelee, nilitumia msemo wa jumla!
Ingawa Rais anajaribu kuendana na hiyo kaulimbiu kwa vitendo kwa kutembea Marekani na kuwa na utayari wa kushirikiana na taasisi za kimataifa lipo jambo ambalo naliona kama vile ni deni kwake. Akiweza kulitimiza kwa vitendo ataliweka jina lake miongoni mwa majina yatakayokumbukwa daima.
Ulikuwepo mpango wa Kilimo Kwanza lakini umekufa kifo cha kawaida kabisa, uliondoka na awamu ya nne ya JK. Ulikuwa ni mpango mzuri uliokosa watendaji na ukakosa kule kujitoa kwa wataalam waliopewa kazi ya kuusimamia kikamilifu.
Huwa ninasikitika sana nikiona hii mito tuliyopewa na Mungu inatitirisha maji kuelekea baharini ufikapo mwezi wa April. Inasikitisha mno na kuona hazina hiyo ya maji mengi yakipotea bure. Ushauri wangu ili nguvu ya awamu ya sita isipotee bure ni kutenga pesa nyingi za kujenga visima vya kisasa vya maji, ili wakati wa mvua nyingi tuweke akiba ya kutumia mwaka mzima.
Tutambue kuwa mahitaji ya chakula ya Ulaya ni ya mwaka mzima. Lakini uzalishaji wetu ni wa misimu bado ni ule wa kusuasua. Tukitaka kwenda sambamba na soko kubwa na la uhakika la Ulaya basi tufufue mradi wenye kufanana na kilimo kwanza. Unaweza usiwe unafanana mia kwa mia na ule wa mwanzo, lakini unaweza kuboreshwa na kutusaidia.
Kuliko kuyaona maelfu kwa maelfu ya lita za maji yakitiririka baharini na kupotea bure, Ni wakati wa kuyatumia kwa faida ya kilimo chetu chenye ukame mwingi.
Yangu ni hayo tu kwa jioni hii.