Nzelu za bwino
JF-Expert Member
- Jan 12, 2020
- 400
- 484
Salaam wana jukwaa,
Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi ya kushuhudia UCHAGUZI WA kihistoria ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo.
Pia nichukue nafasi hii kumpongeza mh Tundu Lissu kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa CHADEMA.
Nampongeza mh John Heche kuchaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa chama.
Kipekee nampongeza mwenyekiti anaemaliza muda wake mh Freeman Mbowe kwa kuanda uchaguzi ulio huru,haki na wazi.
na BAADA ya matokeo kuonyesha ameshindwa kakubali haraka sana na kumpongeza mshindan wake hakika hii ndio demokrasia na na siasa ya watu waliostarabika.hongera Mbowe.
BAADA ya kueleza hayo napenda kueleza kazi tatu muhimu zilizo mbele ya Viongozi wapya.
Soma Pia: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%
1,kuunganisha wanachama waliogawanyika pande mbili wakati wa uchaguzi.hii kazi inahitaji kufanya kwa uangalifu na busara sana.bila kuunganisha makundi hayo chama kitabaki kinafanya siasa ya kujipinga chenyewe.matokeo ya asilimia 51 kwa 49 sio kitu chakubeza hata kidogo.
2.kuandaa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa udiwan,wabunge na rais utakao fanyika mwaka huu 2025 nalo nijambo muhimu sana bila kujali chama kitashiriki au la.
3.kutafuta pesa ya kuendeshea chama kuelekea uchaguzi mkuu nalo ni jambo muhimu.nimesema hili BAADA ya kusikia kwamba sehemu kubwa ya maandalizi ya kufanikisha mkutano mkuu wao yalitokana na kujitolea kwa mbowe na marafiki zake.
Je katika muda mfupi uliobaki kuelekea uchaguzi mkuu wataweza kufanya haya yote kwa wakati moja?
Nawasilisha.