Kazi kuu za Jeshi la Wananchi ni mbili tu kulinda mipaka ya nchi na kulinda Katiba

Kazi kuu za Jeshi la Wananchi ni mbili tu kulinda mipaka ya nchi na kulinda Katiba

Jeshi letu linatumika hadi kwenda kulinda amani ya nchi kigeni wakati huku nyumbani kuna kikundi cha wahuni wachache wanaikanyaga Katiba kwa kuendesha chaguzi haramu ambazo zinaingiza watawala haramu madarakani nalo jeshi linahusika kutazwazwa kwa watawala haramu.
Tunataka wazalendo ndani ya Jeshi letu. Hatutaki wanajeshi "maokoto"
 
Chadema mlisusia uchaguzi,sasa mnatapatapa
 
Katika nchi yetu kuna chombo kikuu kilichopewa majukumu makuu mawili yaani
1. Kulinda mipaka
2. Kulinda Katiba

Katika kutekeleza majukumu hayo chombo hiki hakiwezi kurelegate majukumu yake kwa yeyote yule.

Mfano wa jukumu la kulinda mipaka ni pale Iddi Amin alipovamia nchi yetu na kutangaza eneo la kagera kuwa ni sehemu ya Uganda. Jeshi letu liliingia kazini na the rest is history.

Jukumu la Pili la kulinda katiba.mfano mzuri ni pale alipofariki Rais Magufuli, kuna watu walitaka kupindisha katiba makamu wake asiwe rais. Jeshi lilisimama na kuwaambia NO. Lazina katiba iheshimiwe.

Sasa jukumu la kulinda katiba siyo la Kumlinda mtawala peke yake, bali ni kuangalia kiujumla wake pale Katiba inapokanyagwa na kuendelea kukanyagwa tu with impunity. Kwa mfano katiba yetu inasena wazi kuwa TANANIA NI NCHi YA KIDEMOKRASIA YA MFUMO WA VYAMA VINGI. Lakini tunaona mfumo huu unabagazwa, unaharibiwa kimakusudi, mamilioni ya Watanzania wanakosa uwakilishi katika siasa kwa sababu kuna kundi linavuruga mifumo ya uchaguzi. Mahakama zinachezewachezewa, hakuna haki tena mahakamani. Hapo jeshi lazima likumbushe kuwa WALINZI WA KATIBA tupo!

Hatujui kwa kweli katika mazingira kama haya Jeshi linatimizaje wajibu wake wa kulinda katiba. Maana lisipolinda katiba basi linageuka jeshi lisilotimiza wajibu wake ipasavyo na wananchi watajitenga nalo au kulidharau.

Hatusemi Jeshi livunje katiba, bali lilinde katiba. Na linaweza kulinda katiba kwa kuwatahadharisha wenye mamlaka kuwa Jeshi halioni afya kutokana na mwenendo wao wa kuongoza nchi. Na kwamba Jeshi halitokuwa tayari kutii amri haramu ikiwemo kuwageuzia silaha za moto wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Mwalimu Nyerere alitoa kauli nzito akasema kuwa JESHI LETU SIYO JESHI MAAMUMA. Akasema kuwa Jeshi letu litalinda mfumo wa chama kimoja kama ndiyo mfumo uliopo na litalinda mfumo wa vyama vingi kama ndiyo mfumo uliopo kwa mujibu wa sheria. Sasa sijajua Jeshi letu linalindaje mfumo wa vyama vingi wakati tunaona mfumo huu ukihujumiwa waziwazi.

Mimi nahofia, isije ikafikia hatua wananchi wakaliona Jeshi kama hired Merceneries wa kulinda kundi fulani la watawala ambao wanahujumu kila aina ya FAIR GROUNDS katika nchi.

Najiuliza Jeshi litajisikia ufahari gani kufanya Gwaride la kumkaribisha na kumpa kiapo cha utii Amiri jeshi mkuu aliyepatikana katika uchaguzi feki, usiohusisha wananchi mamilioni kwa mamilioni wanaotaka fairness ktk kuwapata viongozi wao. Sasa hapo litakuwa kweli jeshi la wananchi au jeshi la genge la waiba uchaguzi?.

Mwisho nimalize kwa kusema kuwa, Jeshi lina wajibu wa kulisaidia Taifa hili kulinda amani kwa kuilinda katiba. Lisipoilinda katiba ipasavyo, hii nchi haitokwenda, itakuwa vulnerable kwa adui wa ndani na nje, na kwa kweli baada ya hapo kazi ya jeshi kulinda mipaka itakuwa ngumu sana. Ni bora sasa likatimiza majukumu yake ya kulinda mipaka na katiba ipasavyo na kwa wivu mkubwa.

Nimalizie kulikumbusha jeshi kiapo liliilokula mbele ya Amiri jeshi mkuu baba wa Taifa mwalimu Nyerere ktk miaka ya 1960's kuwa HATUTAGEUZA SILAHA ZETU KWA WANANCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Majukumu ya JWTZ yapo 6 kisheria sheria ya ulizi wa Taifa sura 192

1. Kulinda uhuru na mipaka
2.kuhifadhi amani na usalama
3.kutoa misaada kwa vyombo vya usalama vya ndani
4.kushiriki katila kulinda amani kimataifa
5. Kuhudumia na kutoa misaada kwa jamii
6.kutekeleza maelekezo ya Rais

Hapo nilikuwa nakuongezea tu, si kwaubaya
 
Nimesikitishwa sana na Taarifa kuwa Wanajeshi wanasombwa na magari kwenda kwenye mikutano ya kampeni ya CCM na kuvalishwa nguo za kiraia kama wana CCM washiriki. Hii kwa kweki siyo kazi ya jeshi!
Tanzanian 😭😭😭😭😭
 
Back
Top Bottom