Kazi ni nyingi ajira ni chache au "vice versa"?

Kazi ni nyingi ajira ni chache au "vice versa"?

Mimi mstaarabu

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2020
Posts
262
Reaction score
577
Kazi unayofanya sasa hivi uliiisomea? Au ajira yako ya sasa inaendana na ulichosomea?

Wale mnaofanya kazi ambazo hamjasomea na life linasonga tu basi tumia uzi huu kuwapa vijana tips na moyo kwasababu kuna wimbi la depresssion sasa hivi.

Nb: Ndugu zangu wenye degree fanya chochote cha kukuingizia kipato mambo ya cheti weka lamination uhifadhi kabatini.
 
Nimeanza kujifunza digital skills mwaka 2018 (Social media marketing, SEO, Content marketing, Web design na Canva) kisha nikaunganisha na uwezo niliokuwa nao wa mathematics na Physics na kuandaa study resources kisha kuanza kuuza online.

Mwanzoni haikuwa rahisi ila mpaka sasa sifikirii kabisa kuja kutuma CV kuomba kazi yoyote.

Uzoefu na ujuzi wa kidigitali ambao nimeupata umeweza kuendesha maisha yangu mwaka wa 4 huu.

Kwasasa nafundisha hizo digital skills, nauza kozi na kuuza hizo study resources.

Ulimwengu wa sasa pambana kujenga ujuzi na siyo kuonyesha vyeti.
 
Back
Top Bottom