Nimeanza kujifunza digital skills mwaka 2018 (Social media marketing, SEO, Content marketing, Web design na Canva) kisha nikaunganisha na uwezo niliokuwa nao wa mathematics na Physics na kuandaa study resources kisha kuanza kuuza online.
Mwanzoni haikuwa rahisi ila mpaka sasa sifikirii kabisa kuja kutuma CV kuomba kazi yoyote.
Uzoefu na ujuzi wa kidigitali ambao nimeupata umeweza kuendesha maisha yangu mwaka wa 4 huu.
Kwasasa nafundisha hizo digital skills, nauza kozi na kuuza hizo study resources.
Ulimwengu wa sasa pambana kujenga ujuzi na siyo kuonyesha vyeti.