Kazi ni utu, kazi ni ibada

Kazi ni utu, kazi ni ibada

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
346
Reaction score
522
Habari wanazuoni, Leo Najaribu kutafakari juu ya;

đŸ‘‰Thamani ya mtu inajulikana kwa kiwango cha juhudi na ufanisi wake katika kazi,Pia tabia ya mtu na utu wake inaoneshwa vizuri zaidi kupitia jinsi anavyotekeleza majukumu yake ya kazi.

Mfano hai

1.Swali la kwanza ukweni kijana anaetaka kumposa binti kigori, ataulizwa unafanya kazi gani?

2. Binti anaeolewa,ataulizwa unajishughulisha na nini?

3.Wakati unatafuta nyumba yakupanga Baba au mama mwenye nyumba atauliza unafanya kazi gani?

4. Rafiki zako wautotoni mlipotezana zamani mkikutana swali la kwanza watauliza unamishe gani unafanya kazi wapi?

Take home message: KAZI NI UTU.

VIJANA NA WASICHANA;

đŸ‘‰ Vijana na wasichana wanapaswa kujituma kwa bidii, kuzingatia maadili mema, na kutafuta kipato kwa njia halali. Kuacha tamaa za haraka na kujenga tabia za kazi na juhudi ni muhimu kwa maendeleo binafsi na ya jamii. Kila mmoja wetu ana nafasi ya kuchangia katika kujenga jamii yenye maadili na mafanikio ya kweli.

Mwisho nawasalimu Kwa Jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, itikieni Kazi naiendeleee
 
Kuna jamaa mtu wa Pemba, ikifika muda wa swala ile mchana wengine wote wataenda msikitini, yeye haendi msikitini anapiga kazi tu anakwambia hata ile ni ibada.
 
Kuna jamaa mtu wa Pemba, ikifika muda wa swala ile mchana wengine wote wataenda msikitini, yeye haendi msikitini anapiga kazi tu anakwambia hata ile ni ibada.
Shirika la watawa wabenedictine wanaslogan Yao inasema KAZI na Sala ( oral et labora) ,hivi vitu vinakwenda sambamba , maandiko pia matakatifu Biblia yanasema asiyefanyakazi na asile 2 Wathesalonike 3:10
 
"vijana na wasichana" maana yake ni ipi
vijana na wasichana" nazungumzia kundi rika la watu wenye umri wa ujana, na wasichana katika muktadha wa masuala mbalimbali, katika kuhusianisha na haki za kijinsia na utu katika minajili ya kufanya kazi na kujituma..
 
Je,wasichana hawajawahi kuwa vijana?
 
Back
Top Bottom