Kazi ni wito na ibada, Tuitendee heshima Inayostahili

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
638
Reaction score
1,043
Ndugu zangu wapendwa!.

👉🏾Kuna jambo moja ambalo hatufai kulisahau ,kazi ni ibada. Kwa kila jasho tunalomwaga kwa ajili ya riziki halali ni sadaka mbele za Mungu. Ni njia ya kuonesha shukrani, heshima na thamani ya maisha yenye maana.

Lakini swali kubwa ni hili, je, kweli tunaitendea kazi heshima hiyo inayostahili?

Vijana wenzangu, tusidanganywe. Tamaa ya mali za haraka kwani imewateka wengi , wizi, uhujumu, uzembe kazini, na kutotimiza wajibu wetu vimegeuka kuwa “njia za mkato” za mafanikio. Lakini mafanikio ya kweli hayawezi kujengwa juu ya misingi ya uovu. Hayadumu. Hayabarikiwi.

👉🏾Kazi ni zaidi ya mshahara ni wito. Kila mmoja wetu ana nafasi ya kuwa mwanga kazini kwake, kuwa mfano wa kuigwa, na kuwa sauti ya mabadiliko. Tumeumbwa kuleta tofauti. Hatujaitwa kuharibu, bali kujenga.

Tujitazame ndani ya mioyo yetu. Tujikumbushe kuwa kila kazi tunayofanya kwa uaminifu ni sala. Tamaa ya haraka ni mtego wa kupoteza hadhi, utu, na mwisho wa siku uhuru wetu.

👉🏾Leo, naomba tuchukue uamuzi wa kweli,
Tuifanye kazi kwa bidii. Tuifanye kwa heshima. Tuihifadhi kama ibada.

Mafanikio halali yanakuja si kwa pupa, bali kwa ustahimilivu na uaminifu.

Tuchague kuwa sehemu ya kizazi kinachojenga, si kinachobomoa.
👉🏾Oratio et labor sunt cultus.


~Chavalikungu
 
asante kwaujumbe mzuri sana ila napenda utambue kwamba kazi nikama mfumo alie juu ndie mnufaikaji na alie chini ndio mtumwa.
hivo nijukumu la kila mmoja kuhakikisha anapambana kujikomboa.
 
This is real wisdom 💪
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…