Kazi nzito Trump aliyonayo

Kazi nzito Trump aliyonayo

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
2,748
Reaction score
5,112
Kati ya kazi nzito bwana Donald Trump alizo nazo ukiondoa changamoto za ndani ni kupambana na haya mataifa yanayo tishia usalama wa marekani kwa miaka mingi ijayo.

Moja kati ya kazi tukufu uliofanya utawala wa Democrats wa bwana Biden ni kuwaweka karibu zaidi maadui wa marekani.

DT kazi ya kwanza ni kudhoofisha ukaribu wa China na Russia. ili uweze kumdhoofisha mmoja kati ya hawa ambao ndio wameshikilia nguvu ya mataifa yaliyo kinyume na sera mbalimbali za marekani basi ni kudhoofisha uhusiano wao.

Ki vipi ataweza kudhoofisha uhusiano wao ? Linabaki swali ambalo litahitaji fikra makini

Je, marekani ataimarisha uhusiano wa karibu sana na Russia na kuondoa tofauti zao ili kumzuia China au ataimraisha uhusiano wa karibu zaidi na China na kuondoa tofauti zao ili kumzuia Russia ? Fikra zangu zaweza kuwa sahihi au sivyo

Tishio kwa Israel na Marekani juu ya maslahi yao ya pamoja ya ME kutoka kwa ukuaji wa kijeshi wa Iran hasa mpango wake mkuu wa umiliki wa silaha za maangamizi

DT na serikali yao wataweza vipi kumzuia Iran kutimiza adhma yake kuu ya kujihakikishia usalama wa taifa lake na washirika wake kwa asilimia kubwa.

Vikwazo kwa DT ni ukaribu wa Iran kwa Russia na China hasa kiulinzi ulio ongezeka chini ya utawala wa Biden unao ondoka.

Ki vipi ataweza punguza ukaribu wa China,Russia kwa Iran ni mbinu gani atakuja nazo ? Vikwazo kwa wingi ? Ama tofauti ?

Tishio la China kiteknolojia, kiusalama na kiuchumi kwa marekani hili ni duru la pili la Trump kuja na mbinu mpya za kumkabiri China

Baadhi ya mbinu alizo taja ni ongezeko la ushuru kwa 100% kwa bidhaa kutoka China , upigwaji wa marufuku wa baadhi ya bidhaa za China nchini Marekani hapa amejiza titi zaidi katika clean energy.

Ni mbinu gani atatumia kumdhibiti China katika teknolojia ya Chips.

Vipi kuhusu mgogoro alioshindwa kuumalizia wa Tiktok je, atauibua tena ili kumdhibiti zaidi China ?

Je, tutegemee mbinu mpya zaidi kumkabili China tofauti na alizo tumia mwanzo ?

Ni kazi nyingi bwana DT anazo zilizo nje ya utawala wa ndani wa marekani za kufanya ili kuimarisha utawala wa marekani duniani kiujumla.
 
Trump anaenda kuimaliza Marekani, hajui lolotee ndio maana ana Overconfident katika maswala mazito.
Jambo linaloleta utata mkubwa ni urafiki wake na Putin,

NATO haijui ni nini kitaendelea maana Putin na Trump ni marafiki wa karibu kiasi kwamba Putin alishangilia sana baada ya Trump kushinda.

Jambo lililowazi ni Ukraine kuchukuliwa na Putin, je baada ya Ukraine kuwa sehemu ya Urusi, tamaa za Putin kujiongezea maeneo zitaishia hapo?

Je, nia yake ya kuirudisha USSR ya miaka ya 90 itaelekea katika taifa lipi jingine?

Je, maslahi na usalama wa umoja wa ulaya utakuwa katika hali gani, chini ya NATO isiyo na muelekeo?

Mimi nadhani, tusubiri na kuona.
 
Kati ya kazi nzito bwana Donald Trump alizo nazo ukiondoa changamoto za ndani ni kupambana na haya mataifa yanayo tishia usalama wa marekani kwa miaka mingi ijayo.

Moja kati ya kazi tukufu uliofanya utawala wa Democrats wa bwana Biden ni kuwaweka karibu zaidi maadui wa marekani.

DT kazi ya kwanza ni kudhoofisha ukaribu wa China na Russia. ili uweze kumdhoofisha mmoja kati ya hawa ambao ndio wameshikilia nguvu ya mataifa yaliyo kinyume na sera mbalimbali za marekani basi ni kudhoofisha uhusiano wao.

Ki vipi ataweza kudhoofisha uhusiano wao ? Linabaki swali ambalo litahitaji fikra makini

Je, marekani ataimarisha uhusiano wa karibu sana na Russia na kuondoa tofauti zao ili kumzuia China au ataimraisha uhusiano wa karibu zaidi na China na kuondoa tofauti zao ili kumzuia Russia ? Fikra zangu zaweza kuwa sahihi au sivyo

Tishio kwa Israel na Marekani juu ya maslahi yao ya pamoja ya ME kutoka kwa ukuaji wa kijeshi wa Iran hasa mpango wake mkuu wa umiliki wa silaha za maangamizi

DT na serikali yao wataweza vipi kumzuia Iran kutimiza adhma yake kuu ya kujihakikishia usalama wa taifa lake na washirika wake kwa asilimia kubwa.

Vikwazo kwa DT ni ukaribu wa Iran kwa Russia na China hasa kiulinzi ulio ongezeka chini ya utawala wa Biden unao ondoka.

Ki vipi ataweza punguza ukaribu wa China,Russia kwa Iran ni mbinu gani atakuja nazo ? Vikwazo kwa wingi ? Ama tofauti ?

Tishio la China kiteknolojia, kiusalama na kiuchumi kwa marekani hili ni duru la pili la Trump kuja na mbinu mpya za kumkabiri China

Baadhi ya mbinu alizo taja ni ongezeko la ushuru kwa 100% kwa bidhaa kutoka China , upigwaji wa marufuku wa baadhi ya bidhaa za China nchini Marekani hapa amejiza titi zaidi katika clean energy.

Ni mbinu gani atatumia kumdhibiti China katika teknolojia ya Chips.

Vipi kuhusu mgogoro alioshindwa kuumalizia wa Tiktok je, atauibua tena ili kumdhibiti zaidi China ?

Je, tutegemee mbinu mpya zaidi kumkabili China tofauti na alizo tumia mwanzo ?

Ni kazi nyingi bwana DT anazo zilizo nje ya utawala wa ndani wa marekani za kufanya ili kuimarisha utawala wa marekani duniani kiujumla.
Kazi anayojipa usa kuishape dunia naona ni ngumu sana hataiweza tena ..na akishupaza shingo ataanguka nayo . Usa ijue to kwa sasa is no longer super power alichopaki nacho ni hio dollar yake amabya itadhoofika kupitia global South cooperation
 
Trump's dream is to prioritize the interests of the United States and make it more of an economic threat but he is not inclined to be belligerent the way most American presidents especially associated with the Republican Party have always been.

He will definitely impose the huge taxes on imports as a means of improving his country's economy and to achieve this means countries like China will have to be badly affected.
 
Vita ya kiuchumi ni mbaya, na sio vita kama weusi tunavyowaza kwa kupigana na kupotezana kila leo
America adui yake ni Ulaya wanaotengeneza vitu china
Ndio maana kila wakati anahakikisha China wanalipa kodi kubwa sana kudhibiti hao European countries
 
Safari hii Ayatolah atashirikiana na Mashoga katika kumuua Raisi Trump.
 
Bila shaka wewe jamaa ndio unaongoza hapa JF kwa kuandika ujinga ujinga,
Inaonekana unatembea na Kichwa kitupu.
Ungeniuliza ni kwasababu gani nimeandika hivyo bila ya kumwaga Povu lote hilo.😆🤣
 
Unapenda ushoga ?
Trump kasema anaanzisha Vita dhidi ya Ushoga kwahiyo sio ajabu Mashoga yakaungana na Ayatolah kwenye Bifu na Trump.

Tatizo liko wapi hapo?!🫴

Shughulishen akili.
 
Katika huu uzi kuna mahali nimezungumzia habari za usenge na wasenge ?
 
Ungeniuliza ni kwasababu gani nimeandika hivyo bila ya kumwaga Povu lote hilo.😆🤣
Huna uwezo wa kujibu hata ukiulizwa,
Unaweza kuthibitisha hapa ni nani aliyetaka kumuua Trump?
Najua umeandika kwa msukumo wa chuki ya kidini.
 
Hakuna namna ambayo USA inaweza kukua zaidi au kubakia kuwa superpower bila kuungana kisera (kibiashara na kivita) na Russia, China au Western Europe. USA haiwezi kusimama tena yenyewe. Bahati mbaya sana Trump anaamini USA inaweza kusimama yenyewe. Muda utamfundisha kitu.
 
Back
Top Bottom