Kazi si kuvaa Dela bali kazi ni kulishikilia

Kazi si kuvaa Dela bali kazi ni kulishikilia

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Bila Shaka baadhi yetu tumeshawahi kusikia msemo huu huko mtaani, naam msemo huu ninaweza kuutumia kama ushauri Kwa vijana wenzangu ambao wanafunga ndoa na hasa hasa katika msimu huu WA mfungo mtukufu ambao tunatarajia hivi karibuni.

Kwanza Kwa wale ambao hawajui Dela ni nini? Ni nguo ambayo imeshonwa mfano WA kanzu hivi na mara nyingi huwa ni ndefu Sana kiasi kwamba mvaaji hulazimika kulishikilia ili apate kutembea vizuri maana Bila hivyo anaweza kulikanyaga na kuanguka au anaweza asiwe huru pale atembeapo. Aina hii ya vazi kuivaa sio tabu Kwani unalivaa kirahisi Tu, kazi au shughuli ipo kwenye kulishikilia na hapo ndo kibarua kizito

Napenda kuongea na waoaji kwamba Kama ilivyo rahisi kuvaa Dela basi hata kuoa ni Jambo rahisi pia,lakini shughuli inakuja kwenye kuyaishi Maisha ya ndoa kama ambavyo shughuli inakuja pale unapolazimika kulishikilia Dela Mda wote.

Wanaume ambao mnatarajia kuoa niwaambie wanawake ni viumbe muhimu Sana lakini vina changomoto nyingi Sana katika sayari hii ya dunia, kwahiyo msitarajie kila siku mtakuwa na good time na wake zenu laa! Itafika kipindi mtakuwa na nyakati ngumu Sana ambazo kama hujajizatiti vizuri basi si ajabu ndani ya miezi mitatu ukajikuta unajilaumu kwanini uliamua kuoa au kumuoa huyo baby mama.

Na wana maneno makali mithili ya Kisu kikali na maumivu yake ni Makubwa mno Kwa mwanaume ambaye hajajitayarisha kisaikolojia kudili nayo, hayo maumivu haya poni Kwa kumpiga au kumtolea lugha chafu Bali yahitaji hekima kubwa na Busara kudili nayo,na kubwa zaidi inahitajika kuwa na Subira kubwa kuweza kusavaivi.

Mwanamke ameumbwa na ubavu uliopinda kwahiyo ukijaribu kuunyosha utakatika na ukiuacha hivyo basi unapinda, umeona eeh Yani hapo kama ule msemo WA ndugu zetu wamakonde " ukisimama nchale na ukikaa nchale" nadhani unajua nazungumzia nini hapa,Kwa wale ambao bado hamjanipata ni kwamba tarajia na tambua kuwa always utapata changamoto nyingi toka Kwa wake zenu lakini kubwa ni kuendelea kulishikilia Dela Kwa nguvu zote.

Ni hayo Tu!
 
Dah! Ndoa ni jumba la misumali au gunia la chawa.

Ila ujumbe mzuri sana [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Dah! Ndoa ni jumba la misumali au gunia la chawa.

Ila ujumbe mzuri sana [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Ndoa INA raha zake na changamoto zake,lkn ukipata chaguo sahihi changamoto zinakuwa chache sana
 
Ndoa INA raha zake na changamoto zake,lkn ukipata chaguo sahihi changamoto zinakuwa chache sana
Ni kweli kabisa ila ikiwa wote mna Nia ya kujenga Nyumba Moja bila kugombania fito.

Tatizo wengi hutaka watoe fito ndani na kwenda kujenga nje.
 
Ni kweli kabisa ila ikiwa wote mna Nia ya kujenga Nyumba Moja bila kugombania fito.

Tatizo wengi hutaka watoe fito ndani na kwenda kujenga nje.
Kweli kabisa na hapo ndo penye tatizo kubwa Sana.

Ila Kwa asilimia kubwa wengi wetu huwa tuna fall in love na watu ambao sio sahihi, Yani mwanzoni tunahisi tunapendana lakini baada ya Mda tunakuja kugundua haikuwa kweli na hapo ndio tunaanza kutafuta pale ambao tunadhani ndio sehemu sahihi zaidi, matokeo yake tunaanzisha balaa kubwa majumbani kwetu.
 
Ndoa ina raha yake jamani,unatoka zako misele mke anakupikia chakula unakila then na yeye una mla😀😀
Kweli chief, wawili ni wawili Tu kwakweli ndio maana Mimi nasema hivi haijalishi ndoa zina changamoto gani lkn hakika kuna Raha yake bwana
 
Back
Top Bottom