Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kuna hizi bar hasa za daraja la kati na chini paka huwa wametamalaki wanakodolea macho, wanajipitisha kwenye miguu, wanangurumia wateja na wengine wanawarukia hadi kuwaparua wateja ili wawape nyama au samaki.
Sasa paka wenyewe huwa katika hali mbaya sana ya kiafaya, wengine wakiwa na chawa, wamenyonyoka ngozi au hata ngeu za ajabu ajabu.
Kinachokera na kusumbua ni kwamba wamiliki wa Bar au migahawa wamewaachia wateja jukumu la kupambana na hii mifugo yao jambo ambalo sio sahihi kabisa. Inakera sana mtu ananukala huku anapambana na hii mifugo badala ya wahudumu kuwajibika kuwadhibiti.