๐™†๐™–๐™ฏ๐™ž ๐™ฎ๐™– ๐™ฃ๐™œ๐™ค๐™ฃ๐™ค ๐™ž๐™ฃ๐™–๐™ฅ๐™–๐™จ๐™ฌ๐™– ๐™ ๐™ช๐™– ๐™๐™–๐™ก๐™–๐™ก๐™ž

Wewe ni Mwafrika (Mtanzania) au ni Mzungu?
Isiwe tunamuhukumu mtu bila kumwelewa!
Mbona hili jambo halina uafrika au uzungu. Yani lipo general kabisa mkuu. Hii issue inajiendesha sana. Lengo ni ijiendeshe ikiwa salama. Tusiwapoteze vijana wetu
 
Kwa tafiti nilizozifanya kwanza kabisa naunga mkono hoja kwa upande mmoja lakini pia napinga hoja kwa upande mwingi

Naungana na mtoa mada kuhusu hili suala la baadhi ya wanaume kuchukua hatua ya kubaka wanawake na kupewa mvua za kutosha 30 na wengine kupigwa maisha kabisa sababu na chanzo kikiwa ni tamaa za kimwili, tamaa za kingono na udomo zege

Sasa pakiletwa urasimishaji wa kazi ya kujipatia vipoozea mtoa mada anaona at least kutapunguza wimbi la ubakaji maana kutakua na kituo maalum cha kwenda kujipatia kiburudisho lakini pamoja na kwamba haijawekwa kua km kazi rasmi pia yapo maeneo yanayotoa huduma hio illegally na yanafahamika

Kibaya ni kwamba sababu inafanyika illegally kuna mambo ya kudhulumiana, penzi haliwi thabiti, upunjwaji huduma kwa walio na kipato kidogo, kutokushtakiana kwenye ngazi za kisheria iwapo mmoja anapodhulumiwa, kupatiwa huduma hafifu/finyu/kupunjwa penzi ukilinganisha na gharama ya huduma unayopatiwa, thamani ya huduma na gharama ya huduma kukosa ulinganifu, gharama ya kununua kiburudisho ni kubwa kwa baadhi ya maeneo ukilinganisha na huduma yenyewe yaan huduma mbovu gharama kubwa, usafi na afya ya mtoa huduma pia ni kikwazo kingine na changamoto ya hali ya juu

Ninachopingana na mleta mada ni kwamba km ikirasimishwa ikawa ndio kazi rasmi basi kila mwanamke ataonekana ni kiburudisho na thamani ya ndoa haitokuepo tena, pia maradhi ni changamoto nyingine maana maradhi ni mengi

Kiufupi wanawake watapoteza soko la kuolewa itakua kila mwanaume au mwanamke ukitaka huduma pendwa ya kupata kipoozeo unawahi kibanda cha huduma km ilivyo vibanda vya Tigo Pesa M-pesa, unaenda unaweka au unatoa itakua ni hivyo yaan hakuna tena ulazima wa ndoa na ndoa & familia itakua ni km hiari tu ya mtu binafsi ima aoe ama asioe na sio kulazimishwa kuoa na kujenga familia

Kwa hio nahitimisha kwa kusema kwamba kikubwa wanaume waache kua madomo zege, changamsha ulimi mwanaume tongoza sana tumia ulimi wako usitumie nguvu tongozaaaa sio mwanamke mmoja kwenye wanawake 15 au 20 unaowatongoza hauwezi kukosa wawili au watatu watakaokukubaria

Kila nikisoma Biblia na Msร afu hua najiuliza shetani alikua na jinsia gani maana kiumbe wa kwanza kabisa kumtongoza mwanamke kwa maneno matamu wazi wazi na inasimuliwa wazi wazi na mwanamke akamkubaria alikua ni shetani sasa hadi leo sijajua shetani alikua na jinsia ipi alikua ni mwanaume au alikua ni mwanamke? Maana mwanamke alitongozwa na shetani ale tunda na yeye akamkubaria bila kubisha wala kusita na akalila

Kwa hio nawasihi sana wanaume wote madomo zege mliopo humu na msiokuwepo humu tumieni ndimi zenu vizuri sio pesa zenu unaweza ukamwaga pesa ikiwa wewe ni domo zege domo zito domo pregnant na ukaishia kula za uso vile vile mwaga mchele mwaga maneno matamu imbisha imbisha acha kua goi goi mwisho wa siku utaishia kubaka tu maana domo haliwezi kujieleza domo zito domo limepata ujauzito fungua mdomo nena maneno mwaga maneno mazuri mazuri km wale Jamaa wanaouza vyombo vya promotion watongozรจ tu wanatongozeka

Ushaelewa au nianze upya?
 

Kongole sana kwa hoja nzito.
Kwanza kabisa mkuu nimefurahi kuona umegundua pia wimbi la wingi wa wanaume wanahukumiwa miaka 30 au kifungo cha maisha kwa kua na hisia na kufanya tendo bila ridhaa. Ingekua wanaipata hii huduma wasingefikia huko, ingekua rahisi kwao kulingana na level ya kipato kuna kitu kdg wangepata.
Kumbuka sasaivi wanawake wanaojiuza ni wengi sana sii Dsm pekee. Wanatoza hela nyingi ambayo hadhi yake sijui kama inaendana na hela wanayotaka. Sii salama, wanajali tu hela unayowapa

Naomba nikujibu kwa hoja nzuri tu hapo ulipopinga. Kwani sasaivi hizi huduma hazipo? Kama zipo mbona watu wanaolewa na kuoa?
Kumbuka sii rasmi, inakuja swala la kua rasmi, serikali/watakaopewa dhamana watasimamia upimwaji wa afya za wahusika ili ifanywe salama. Tofaut na sasa inafanyika bila vipimo bila mtu kujua anaefanya nae ni mzima ama la. Itaondoa utapel uliopo pia

๐Ÿคฃ๐Ÿคฃmadomo zege hawaishi mkuu, miaka yote wapooo. Somo lifundishwe huko shule labda namna ya kujiamini
 
Vipi dada zako au binti zako wakijiunga kwenye hii biashara utawapa support?
 
Je, wizara gani isimamie hii sekta?
 
Vipi dada zako au binti zako wakijiunga kwenye hii biashara utawapa support?
Watu wote wana uhuru wa kufanya wanachotaka. Siwezi kuwasupport lkn wawe huru
 
One minute one hundred[emoji39]
 
Mkuu una maana gani unaposema kukubaria, au ndiyo mbadala wa kukubalia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ