Uchaguzi 2020 Kazi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni nini?

Uchaguzi 2020 Kazi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni nini?

yuda75

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
520
Reaction score
1,385
Habari wadau naomba kujua kazi ya NEC ni nini?

Je, ni kukata wagombea? Je, ni kuelimisha wagombea jinsi ya kujaza form na kuwapa muongozo? Je, ni kupiga kampeni kichama? Je, ni kudidimiza siasa?

Siwaelewi hawa watu, nilijua wao wawe walimu wa mchakato wa Uchaguzi na ujazaji wa fomu kwa usahihi kwa wagombea kwani wagombea wengi hawana elimu kama siasa ya nchi yetu inavyo sema kuwa mgombea hakuna kiwango cha elimu mgombea anatakiwa kuwa nacho ili awe na sifa ya ugombea lakini wagombea wengi elimu yao ipo chini.

Je, hiyo fomu imeandikwa kwa lugha gani? Je, kwanini pasiwe na fomu ya sample mgombea apewe ajaze akikosea arekebishwe ndio apewe nyingine ambayo ndio ya mwisho?

Kwani kazi ya NEC ni nini?
 
Kazi za NEC zipo kwa mujibu wa Ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ukipata nafasi tafuta Katiba usome.
 
Hii NEC mimi nilikuwa naichukulia Kama Taasisi ya kuimarisha demokrasia nchini.

Lakini sasa naona inatumika kama rungu la kudhiti ukuaji na uimarishaji wa demokrasia nchini. Haiwezikani Tume iliyowekwa ili kuratibu na kusimamia kwa usawa ushindani wa vyama vya siasa, ikatumika kuengua watu ili kukipa mteremko Chama fulani.

Nafikiri utaratibu ubadilike, Kama mtu amekosea aruhusiwe kurekebisha na kurejesha fomu baada ya marekebisho ili wananchi ndo waamue. Imagine pemba eti ACT wamekosea wote 18! Kweli jamani?

Afu hivi kweli Msukuma na Kibajaj wanaweza kuwa makini kuliko Boniface Jacob wa Ubungo au Ado Shaibu wa Tunduru? Jamani!!!!
 
Lakini hivi vyama si vina viongozi wake.

Sasa katibu wa wilaya au kata ana kazi gani kama hawezi kumsaidia mwanachama wake kujaza fomu ya kuhombea au nayeye hawezi, lakini pia kama sijakosea TUME ilitoa fursa kupeleka Fomu kuhakikiwa kabla ya tarehe ya Uteuzi.
 
Mngekuwa serious kuiongoza hii nchi msingetuuliza hayo maswali.Nyinyi endeleeni tu kukesha mitandaoni na kusoma vitabu vyenu vya ujasusi badala ya kusoma Sheria na Kanuni za Uchaguzi mnazopewa kwenye vikao na Tume.

Shida yenu wakati tume inapowaalika kwenye vikao vya kikazi mjifunze na kuuliza maswali hayo mnakwenda muda wa msosi na kusaini posho.
 
Ni kweli kazi hasa ya NEC ni hoja ya mjadala! Sababu maamuzi ya kuengua wagombea wa upinza yanayofanywa na NEC yanatia shaka juu ya jukumu hasa la Tume hii ni lipi? Inashangaza eti mgombea anaenguliwa kwasababu ya kukosea mwaka wa kuzaliwa, hivi hapo si anaitwa tu na kuelekezwa aandike upya? Kama ni kuepuka kuchafua form si atozwe tu gharama upya na kupewa form mpya?

Ujazaji wa hizo form za wagombea linapaswa kuwa jukumu la kusimamiwa na NEC na sio kutumika kama mtego wa kunasia wagombea wa upinzani na kupitisha wagombea wa CCM bila kupingwa!

Ieleweke vyema kuwa kwenye mabaraza ya madiwani au Bungeni viongozi wanaochaguliwa hawaendi kushindana kujaza form au kufanya shughuli za kujaza form, bali wanakwenda kuwakilisha wananchi wa kata na majimbo yao ili kufikisha kero zao za maendeleo, Sasa inashangaza mno kuona eti kigezo cha kujaza form kinatumika kama passmark ya mgombea!
 
Mbona NEC inatumia fedha nyingi kuelimisha wapiga kura?

Kwanini hawatumii fedha kidogo kuelimisha Wagombea?

Kuna watu nikiwakuta mbinguni narudi maana nitajua kuwa hapo si mbinguni bali ni mapokezi ya jehanamu.
 
Huu utaratibu wa kuwaengua wagombea kwa makosa yakiwemo ya kujaza fomu ni utaratibu wa siku nyingi na unakubalika miongoni mwa wadau wakiwemo hao wagombea unaowasema wewe na ndio maana pingamizi la Mgombea wa CHADEMA dhidi ya wagombea wa CCM na CUF kwenye ngazi ya Kiti cha Rais liliwekwa.

Na nyie mnaolalamika hapa ndio mlishangilia siku ile. Sasa hamkujua kwamba kuna wengi watakaokuwa wahanga wa utaratibu huu. Leo wamepatikana mnaanza kutukana NEC. Vumilieni tu maana ndio haki ilivyo, huwa inachomachoma.
Ni kweli kazi hasa ya NEC ni hoja ya mjadala! Sababu maamuzi ya kuengua wagombea wa upinza yanayofanywa na NEC yanatia shaka juu ya jukumu hasa la Tume hii ni lipi?? Inashangaza eti mgombea anaenguliwa kwasababu ya kukosea mwaka wa kuzaliwa, hivi hapo si anaitwa tu na kuelekezwa aandike upya? Kama ni kuepuka kuchafua form si atozwe tu gharama upya na kupewa form mpya?
 
Habari wadau naomba kujua kazi ya NEC ni nini?

Je, ni kukata wagombea? Je, ni kuelimisha wagombea jinsi ya kujaza form na kuwapa muongozo? Je, ni kupiga kampeni kichama? Je, ni kudidimiza siasa?...
Kazi yao kubwa ni kuhakikisha chama chao kinashinda
 
Kwa mujibu wa sheria za uchaguzi na kwa ufuatiliaji wangu binfsi nimeshuhudia siku tatu kabla ya siku ya uteuzi tarehe 25 agosti, tume ilikaribisha wagombea ambao wanataka kuhakiki fomu zao za uteuzi wafike kwenye ofisi za wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata, jimbo na makamu makuu, lakini ni wagombea wachache walikwenda kuhakiki, kuelekezwa na kurekebishiwa fomu zao na wote waliteuliwa.

Sasa kama mmepewa fursa kama hiyo then hamtaki kwenda mnataka tume iwarambe miguu au ije ofisini kwenu iwajazie fomu. Acheni ujinga nyinyi, tume inawachukulia kama watoto na wajinga wa sheria lakini mkiitwa hamtaki kwenda alafu mnakuja kulalamika kwenye mitandao, watanzania tumeamka sasa hatudanganyiki kwa malalamiko yenu tumewazoea.
 
Ni kuhakikisha boss wao anashinda /kupita bila kupingwa
NEC inatakiwa ijione kama Afisa Mkopo wa benki ambaye anapokea ombi la mkopo kutoka kwa mteja. Afisa Mkopo akigundua kuna kosa la spelling au kosa lingine atamwelekeza akarekebishe. Hawezi kumnyima mkopo eti kwa kuwa amekosea kujaza fomu. NEC badilikeni.
 
NEC inatakiwa ijione kama Afisa Mkopo wa benki ambaye anapokea ombi la mkopo kutoka kwa mteja. Afisa Mkopo akigundua kuna kosa la spelling au kosa lingine atamwelekeza akarekebishe. Hawezi kumnyima mkopo eti kwa kuwa amekosea kujaza fomu. NEC badilikeni.
Hiyo yote ukitaka ibadilike na katiba ubadilishwe maana hao hao viongozi wa nec wanateuliwa na rais hivyo ni vigumu sana kumpingwa boss wao
 
Habari wadau naomba kujua kazi ya NEC ni nini?

Je, ni kukata wagombea? Je, ni kuelimisha wagombea jinsi ya kujaza form na kuwapa muongozo? Je, ni kupiga kampeni kichama? Je, ni kudidimiza siasa?...
Wengi hawakosei mfano mwandishi wa habari wa huko morogoro na eti mwandishi wa habari hajui kujaza fomu.
 
Back
Top Bottom