Kazi ya Uwakala wa M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money inaingizaje pesa?

Selcom inaingizaje pesa ya ziada mzee ufafanuzi zaid???
mkuu kuna sehemu nimeandika usome vizuri maelezo nimeandika kwamba lipa zlivyoanza kufungwa tulihamia selcom badae tena tukahamia mlipa saiv tuko sementup.mwaka wa 4 huu wateja washanizoea wakija wananipa simu niwatolee kwahyo sitoe kwenye till ya wakala natolea huko kwngne ili yale makato nibaki nayo kama faida.wazee na wale watu wanaokuwa na haraka sana nawaonyesha namba ya wakala watolee huwa sihangaik nao.
 
mfano hii ya kwangu ni 0.0 mfano hapo mteja ana elfu 48000,inatoka yote alafu nampa 45500 maana yake namkata 2500 tu.

akienda sehem nyngne atakatwa zaid ya elfu 3.

kwa hyo faida yangu inakuwa 2500 mara watu 10 natoka nje naenda kucheza draft.


najua humu kuna masnich,kwa taarifa ni yenu mbongo ukimzuia hivi atatafuta njia nyingine.waambie mabosi wenu waongeze kamisheni tuwafanyie kazi
 
Kuna njia ngapi za kuamisha pesa kutoka lipa kwa mpesa kwenda sehemu nyingine...na wanaanzia shs ngap kuamisha.
 
Hapa Bado kichwa kinauma
 
Kamisheni imekaa kichawi kweli! Yaani kama vile tunawafanyia kazi Serikali na wenye hayo makampuni ya simu! Unahitajika mzunguko mkubwa sana ili kuvuna chochote mwisho wa mwezi.

Anyway, tuvumilie tu. Maana hakuna namna.
 
Mkuu nieleweshe baada ya pesa kuwepo kwenye lipa yangu naitoaje hiyo pesa ili nipate cash na kama kuna gharamaaa inakuwaje?

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu pesa inatolewa kwa utaratibu upi kwenye laini ya lipa kwa MPESA?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…