Kazi za kujitolea nazo ni muhimu katika maendeleo ya Jamii

Kazi za kujitolea nazo ni muhimu katika maendeleo ya Jamii

Abbas Kallage

New Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
2
Reaction score
1
Kazi za kujitolea ni kazi ambazo mtu au watu wanaamua kufanya kwa ajili ya lengo la kutoa msaada katika jamii. Misaada hiyo inaweza ikawa katika mfumo kifedha, mawazo,elimu na nguvukazi, kulingana na mahitaji ya jamii inayosaidiwa.

Kuna baadhi ya watu huwa wanahisi kuwa kazi za kujitolea ni kama kupoteza muda, hii ni changamoto moja wapo katika kazi ya aina hii lakini haina utofauti yoyote ile na kazi nyingine kwani hata kujitolea kuna leta maendeleo.

Kujitolea kunaweza kuhusisha kazi ya kuchimba au kukarabati barabara, kujenga madaraja, ukarabati wa shule au hata makazi ya watu na hata kazi ya kujitolea kwa ajili ya ushauri na hata kuzoa taka. Kazi ya kujitolea ni muhimu kwa upande wa anayesaidiwa hivyo ni hatua na shauku ya mabadiliko kuelekea maendeleo. Mfano, watu wakiamua kujitolea katika ukarabati wa barabara, hii kazi faida yake ni kurahisisha mawasiliano ambayo ni hatua katika maendeleo.

Hizi kazi za kujitolea husaidia pia katika kujenga mahusiano katika jamii yetu. Pia kujitolea katika kazi kuna punguza tofauti za jamii kama umasikini na tofauti mbalimbali za kielimu au mazingira. Ushauri wangu katika jamii yetu leo ni kwamba tuwe tunafanya kazi za kujitolea ili nchi yetu iweze kuendelea na pia tusiangalie maswala ya maslahi kwanza kwenye kujitolea katika kazi.

Pamoja na changamoto mbalimbali katika kazi za kujitolea, jamii inapaswa kuheshimu juhudi zinazofanywa na watu wanaojitolea. Pia makundi ya watu wanaojitolea yanapaswa kuongeza juhudi zao na kuelimisha umma juu ya dhana ya kujitolea.
 
Imagine waziri wa tamisemi akasema ataanza na waliojitolea wapeleke majina wizarani🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom