Kazi za wahasibu aprili 2011

SpK

Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
40
Reaction score
5
Ndugu wanajamii,

Mimi ni graduate wa Tanzania Institute of Accountancy (TIA) with an Advanced Diploma in Accountancy (ADA, with 2nd Class) 2006. Nina miaka 30 na nina uzoefu wa miaka 3+. Nimewahi kuwa ACCOUNTANT kwenye kampuni moja kabla haijafungwa kwa sababu ya economic crisis 2009.

Natafuta kazi ya UHASIBU inayolipa kuanzia Tshs 322,760 kwa mwezi bila kujari ni Serikalini au ni Kampuni Binafsi popote Tanzania (kijijini au mjini).

Nimejitahidi kuomba ajira kila zinapotangazwa gazetini lakini bahati mbaya kimya yaani sipati jibu imekuwaje (not shorlisted or whatever).

NAOMBA MSAADA wanajamii wenzangu katika hili hata namna ya kupata kazi ambayo naamini baadaye itanisaidia ku-create another income kwa sababu naamini kuwa na kipato cha ziadi mbali na kazi ya kuajiriwa siyo dhambi.

Naomba kuwasilisha.
 
mmh kweli Bongo ngumu, bro pole sana.

Kama ulifanikiwa kusevu kipato kipindi upo kwenye hiyo Kampuni ya mwazo ni bora ukaongeza Elimu kapige CPA itakusaidia mkaka.
 
Reactions: SpK
usikate tamaa kuendelea ku aplly kwenye makampuni tofauti tofauti ,ila hapa JF wajasiriamali wapo wengi natumai utachukuliwa
 
Reactions: SpK
mmh kweli Bongo ngumu,bro pole sana.Kama ulifanikiwa kusevu kipato kipindi upo kwenye hyo Kampuni ya mwazo ni bora ukaongeza Elimu kapige CPA itakusaidia mkaka.
CPA haisomwi hivyo mkuu, unaweza ukaikamia ikakuona. Ushauri mzuri ni kumpa mchongo wa kazi halafu kumsisitiza afanye CPA ili awe na choice kubwa ya kazi.
 
Mkuu jaribu kuvumilia tu. Mungu hamtupi mja wake kwani mvumilivu hula mbivu!
 
Reactions: SpK
CPA haisomwi hivyo mkuu, unaweza ukaikamia ikakuona. Ushauri mzuri ni kumpa mchongo wa kazi halafu kumsisitiza afanye CPA ili awe na choice kubwa ya kazi.

cpa ianongeza wigo wa kupata kazi, maana ma graduate wa accountant ni wengi mtaani (UDSM, MZUMBE, TIA, CBE, IFM,...) wote hao na nafasi za kazi ni chache. mi namshauri piga CPA (kila mtu na bahati yake unaweza ukapiga ukatoka), kama vp fanya ACCA hiyo haina magumashi kama CPA uwakika wa kuipata ni 90% labda uwe kilaza,
 
Reactions: SpK
mtu hana kazi na unamshauri kwa vi-hela vidogo alivyonavyo asome CPA huku bado akiwa na mawazo ya kutafuta kazi ili aweze kujikimu na kutimiza majukumu mengine ya kimaisha,nafikiri kwa situation aliyonayo kwa sasa aendelee kutafuta kazi and then akiwa fresh atasoma hiyo CPA,maake CPA ni miyeyusho mbaya,......
 
CPA haisomwi hivyo mkuu, unaweza ukaikamia ikakuona. Ushauri mzuri ni kumpa mchongo wa kazi halafu kumsisitiza afanye CPA ili awe na choice kubwa ya kazi.

Usikate tamaa,km CPA ukianza usiache mpk kieleweke,huwa inasumbua.
 
Reactions: SpK

Mimi nitakupatia ya TZS 1,200,000
 
...hukushiriki kuiua kampuni ya kwanza kwa kughushi sifuri sifuri??

Mkuu, ni kwamba kampuni hiyo ilifungwa soon kabla hata sija-enjoy kazi hiyo. I hate ufisadi na sipendi anyone ambaye hana commitment ya kuleta matunda ya dhati kwenye kampuni.
 
Siku hizi mara nyingi kazi ni kujuana. But keep on applying, you will never know
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…