Hadi pale mtakapoweza kutenganisha utaifa na rangi ya ngozi/asili ya watu husika ndio upumbavu na ushamba utakuwa umewatoka akilini. Hivi aliyeapishwa jana kama makamu wa rais, Kamala Harris, mtamuita beberu, mwafrika, mhindi au mmarekani? Sio kila jambo la nchi ya Marekani linahusu mzungu, acheni ushamba. Asilimia kubwa ya waliowapigia kura Biden/Harris ni watu weusi. Watu wakitizama hafla ya kuapishwa kwa Biden wanafatilia matukio ya nchi ya Marekani sio wazungu, waafrika, wahindi n.k, n.k. Stesheni za Tv nazo zinawapa watazamaji wao kile ambacho wanataka. Hafla yenyewe ilirushwa live na media zote za kutajika, CNN, BBC, France24 ya mfaransa, NHK World ya mjapani, CGTN ya mchina hadi na Aljazeera ya muarabu. Alafu jombaa mbona usitizame CHAN kwenye stesheni yenu pendwa TBC kama nyie ndio mnajitambua zaidi? Mbona unakosa uzalendo wa kutazama taarabu 24/7 kama ambavyo serikali yako imekupangia? Unafata nini kwenye michuano ya CHAN na KBC wakati kuna content za kutazama ambazo ni za kitanzania kwa 100%?