DOKEZO KCMC sitorudi nikiwa na akili timamu

DOKEZO KCMC sitorudi nikiwa na akili timamu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Darren2019

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2019
Posts
1,112
Reaction score
2,400
KCMC imebaki jina tu, hospitali hii pendwa kwa miongo kadhaa sasa nakiri mbele ya umma, labda nipelekwe sijitambui ila kwa huduma nilizopata na kushuhudia kwa wateja wengne, hakika huu ndio mwisho wangu kutia miguu hospitali hii.

1. Customer care mbovu, hawajali wagonjwa /wateja.
Madaktari wengne wanafoka bila sababu za msingi, wewe daktari uliyenifokea kisa nimekaa kwenye kiti tofsuti na ulichotaka pasipo kufaham nimekusamehe bure.

2. Kujuana kwingi, mtu amekuja saa 1 asubuhi anapewa namba 70 mwingne anakuja saa 6 anapewa namba 40, yaani wewe unapita mizunguko ya kutosha ila wengne wanakuja na kupata huduma ukishangaa kwenye bench.

3. Wahudumu/ madaktari wengi nlowaona ni vijana wadogo wadogo tu, hawako serious wanapiga stori za kubeti na kombe la dunia tu[emoji848]

4. Vipimo vya mchongo, baada ya kumwona daktari anakushauri kuchukua kipimo kingne kwa daktari mwingne anakutajia na pesa umpe, la ajabu zile pesa zinachukuliwa kwa siri na risiti hakuna.

5. No privacy, inakuaje hospitali kubwa kama hii wagonjwa mnasikilizwa kwa pamoja km mko darasani?

6. Mgonjwa anaumwa macho anaambiwa aende arudi siku nyingne muda umekwisha akati ameshinda hospitali tangu asubuhi, eti akameze paracetamol km ana maumivu.
Wewe dada uliyekuwa chumba cha miwani tareh 25-11-2022 saa 11 jioni Mungu akusamehe hukustahili kuwa muhudumu wa afya kabisa.

7. Huduma moja nimetajiwa bei mbili tofauti na wahudumu wawili tofauti tena chumba hicho hicho, tofautivya elfu 30, is it possible?

8. Hospitali ya rufaa haina lens ya miwani kweli hadi waagize tena nisubiri miezi miwili[emoji848]

9. Mgonjwa unatibiwa hupewi maelezo ya tatizo lako kwa ufasaha na hupewi document yoyote kuhusu majibu ya vipimo, taarifa zinabaki kwenye computer zao, huu ni uungwana?

10. Mapokezi naulizwa dini yangu ili nini? Kwamba huduma za afya zinachagua dini???

NB. Nimeandika kwa ufupi tu ila hayo ni baadhi ya mambo yaliyonisibu KCMC na kunifanya niamue rasmi kuipa kisogo hii hospitali.

Sina ubaya na mtu yeyote anayehusika na hospitali hii na wala simfahamu yeyote ila nawasihi watumishi tuheshimu mahali pa kazi.
 
Kcmc, mbali na hospitali yenyewe ndio mitaa niliyokulia mimi.

Nachojua, mara nyingi mgonjwa asipopata huduma alotarajia, basi malalamiko ndio kitu kinachofuata.

Kuna siku nilimpekeka wife hospitali usiku wa saa 7. Aliugua ghafla. Alikuwa akijisikia vibaya, akilalamika moyo kwenda mbio na alikuwa akitokwa jasho haswa. Nikamkimbiza hospitali.(sio kcmc). Hakuna siku nilipatatabu kama siku hiyo.

Nilianza kupata huduma kwa daktari saa 1 baada ya kufika. Akapimwa pressure, mapigo ya moyo, mkojo, na damu. Majibu nikaambiwa hana shida yoyote. Wakanishauri nikamle chai ya mchai chai. Nikafanya hivyo.

Nashukuru mungu alirudia katika hali yake ya kawaida. Na hilo tatizo halijawahi kujirudia. Sijui tatizo lilikuwa ni nini?

Huduma niliyotarajia kupata kulingana na hali ya wife ilivyokuwa kwa kweli ni Mbingu na ardhi.

Mara nyingi matarajio huleta huzuni.
 
Kesi yako inanikumbusha mama Anna Nghwira ambaye alikuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, ambaye alifariki dunia mwaka jana.

Huyo mama alikuwa ana bifu kubwa na zito (binafsi?)na hospitali ya KCMC, mara zote alikuwa akiwasema vibaya tu, lakini tunaambiwa kuwa huyo mama alikuwa akiumwa ghafla, wasaidizi wake watamuwahisha hapo hapo KCMC kutibiwa na anapona, lakini shukrani hatoi zaidi ya kuropoka shombo na kuwakejeli.

Sasa mziki ukatokea baada ya kutumbuliwa ukuu wa mkoa wa Kilimanjaro, halafu mwezi huo huo kuna mama fulani ambaye ni rafiki/ndugu yake alifikishwa hapo KCMC mbio mbio ikisemekana akiwa ameshafariki dunia lakini ndugu wakidai alikuwa bado yupo hai ila KCMC ikazembea. Sasa ghafla hiyo issue ikamuibua te mama Nghwira na kuja kulalamika kuwa ndugu/rafiki yake amepoteza maisha kwa sababu ya uzembe wa KCMC!

Haukupita muda mrefu sana mama Nghwira akaugua akiwa Arusha na kulazwa Mount Meru Hospital, watu wa karibu wanasema hali yake ilipaswa kulazwa KCMC lakini kwa sababu ya mtazamo wako kuhusu KCMC mama akaachwa hapo hapo Mount Meru Hospital mpaka akafariki dunia.

Funzo ni nini?
Matatizo ya hospitali za umma za Tanzania tunayafahamu, mengi yanafanana, sio busara sana kujiapiza kuwa hutataka kutibiwa huko wakati hatuna option bora zaidi.
 
Mkuu funzo lako limenipa furaha sana. Asante sana mkuu.
 
KCMC imebaki jina tu, hospitali hii pendwa kwa miongo kadhaa sasa nakiri mbele ya umma, labda nipelekwe sijitambui ila kwa huduma nilizopata na kushuhudia kwa wateja wengne, hakika huu ndio mwisho wangu kutia miguu hospitali hii.

1. Customer care mbovu, hawajali wagonjwa /wateja.
Madaktari wengne wanafoka bila sababu za msingi, wewe daktari uliyenifokea kisa nimekaa kwenye kiti tofsuti na ulichotaka pasipo kufaham nimekusamehe bure.

2. Kujuana kwingi, mtu amekuja saa 1 asubuhi anapewa namba 70 mwingne anakuja saa 6 anapewa namba 40, yaani wewe unapita mizunguko ya kutosha ila wengne wanakuja na kupata huduma ukishangaa kwenye bench.

3. Wahudumu/ madaktari wengi nlowaona ni vijana wadogo wadogo tu, hawako serious wanapiga stori za kubeti na kombe la dunia tu[emoji848]

4. Vipimo vya mchongo, baada ya kumwona daktari anakushauri kuchukua kipimo kingne kwa daktari mwingne anakutajia na pesa umpe, la ajabu zile pesa zinachukuliwa kwa siri na risiti hakuna.

4. No privacy, inakuaje hospitali kubwa kama wagonjwa mnasikilizwa kwa pamoja km mko darasani?

5. Mgonjwa anaumwa macho anaambiwa aende arudi siku nyingne muda umekwisha akati ameshinda hospitali tangu asubuhi, eti akameze paracetamol km ana maumivu.
Wewe dada uliyekuwa chumba cha miwani tareh 25-11-2023 saa 11 jioni Mungu akusamehe hukustahili kuwa muhudumu wa afya kabisa.

6. Huduma moja nimetajiwa bei mbili tofauti na wahudumu wawili tofauti tena chumba hicho hicho, tofautivya elfu 30, is it possible?

7. Hospitali ya rufaa haina lens ya miwani kweli hadi waagize tena nisubiri miezi miwili[emoji848]

8. Mgonjwa unatibiwa hupewi maelezo ya tatizo lako kwa ufasaha na hupewi document yoyote kuhusu majibu ya vipimo, taarifa zinabaki kwenye computer zao, huu ni uungwana?

9. Mapokezi naulizwa dini yangu ili nini? Kwamba huduma za afya zinachagua dini???

10. Nimeandika kwa ufupi tu ila hayo ni baadhi ya mambo yaliyonisibu KCMC na kunifanya niamue rasmi kuipa kisogo hii hospitali.
Kiongozi mmoja alisema anakiri hospitali hiyo imetawaliwa na ukabila, labda haya unayolalamikia ni matokeo yake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom