Hahahahahahaha, ninakuhurumia kwasababu Kenya mlijitenga na Africa nzima katika ukombozi kusini mwa Africa, hamuwezi kujua kilichokua kinaendelea. Ngoja nikuelimishe kidogo.
Vyama vyote vya ukombozi mwa nchi kusini mwa Africa, vilikua na makao yao makuu Tanzania, isipokua ANC ambacho kilikua kilishaanza mapambano ya kudai Uhuru kwa amani, lakini walipoona kwamba hawawezi kupata Uhuru kwa amani, Mandela alikuja Tanzania kuomba JWTZ lianzishe vita dhidi ya Makaburu, ndio pakazaliwa"Nkonto Nsizwe", JWTZ ilianza kazi ya kuwapa mafunzo wakimbizi wa SA waliokuwepo Tanzania, na kuanzisha mapambano ya Silaha kutokea Tanzania.
Robert Mugabe akiwa Tanzania na ZANU-PF aliomba aanzishe vita kwa msaada wa JWTZ, lakini hapakuwa na wakimbizi wengi toka Zimbabwe hapa Tanzania, hivyo haikuwezekana, badala yake kutokana na kupakana kwa Msumbiji na Tanzania, Nyerere aliamua kuikomboa Msumbiji kwanza, then iwe rais kuikomboa Zimbabwe kutokea Msumbiji, ndicho kilichofanyika.
Baada ya Msumbiji kupata Uhuru 1975, Mugabe na Emerson Mnagangwa, walihamisha makao yao toka Bagamoyo, Tanzania na kuhamia Msumbiji, baada ya Msumbiji kupata Uhuru, wazimbabwe wengi walikimbilia Msumbiji kama wakimbizi, hivyo ilikua rahisi kwa ZANU-PF kupata vijana na kuwafanyia train, China ya Brigadier General Hashim Mbita, ndiye aliyeongoza mafunzo ya majeshi yote ya nchi za kusini mwa Afrika, ndani na nje ya Tanzania.
Kwahiyo Zimbabwe haijawahi kuwapa mafunzo Msumbiji, majeshi yote ya Msumbiji na Zimbabwe yalipata mafunzo toka Tanzania, Msumbiji walifunzwa ndani ya Tanzania, na baada ya JWTZ kuikomboa sehemu kubwa ya kaskazini mwa Msumbiji, mafunzo yalifanyika ndani ya Msumbiji, jambo lililowalazimisha wareno kukubali kukaa katika meza ya mazungumzo.
Sent using
Jamii Forums mobile app