Huna ushahidi wowote ule kama wale wote wanaobishana humu jukwani kuhusu Yanga na simba ni mafukara. Hivyo kama wewe ulikuwa fukara kwa sababu hiyo, basi ilikuwa ni bahati mbaya sana kwako. Humu kuna watu wana biashara zao, wengine wana kazi zao za maana tu! Na bado ubishani kama kawaida.
Halafu siyo vizuri kuwapangia watu maisha yao. Kama vipi wewe tuache tufurahie maisha yetu bhana. Wewe endelea tu kutuwakilisha huko kwenye kulalamikia tozo, na sisi tutakuwakilisha huku kwenye ubishani wa Yanga na Simba