Keenja na Binti yake Eliaisa

Myujumi Juma; Heshima Mbele Dada/Kaka.

Ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kufafanua madai yangu.

Comment imesema: Naomba tuachie wanaohusika kuishughulikia kesi hii, ili haki ya kweli ipatikane kwa wote kadri inavyowezekana.

Mimi nikaitafsiri kama: tuwaachie, tuwaamini, wahusika waendeshe kesi, waendeshe Serikali, watuongozee nchi, tuwaangalie kama watazamaji wa mpira ambao hata timu yao ikivurunda vipi, hawaruhusuiwa kuvamia uwanja kwa sababu wapo wahusika, wachezji.

Nikajibu: Nooooooooh! That is treason! Abdication of your public duty to watch the government is as bad as espionage! Do not pick sides here, pick the country. Look at the mockery of justice that happened here!

Nikimaanisha: Ni wajibu wetu kuichunga Serikali. Hatuna nguvu walizo kuwa nazo wale wanao endesha nchi, kwa hiyo, dogo kuliko yote tunalo weza kufanya ni kujadili, kushauri, kulia, na kuongea kwa kura zetu. Kutokufanya hivyo, kuangalia nyumba yetu inateketea na wahusika wamelala, na tusifanye lolote ni kuisaliti nchi yetu. Ni sawa na mhujumu anaye uza siri za nchi.
 

Hawa jamaa zetu wa kule mkoa wa Kilimanjaro mbona wanakuwa na tamaa sana na wizi wa kijinga.
Na kama mtu anatuhumiwa kwa kosa kama hilo kwa nini awe nje ya nchi?????

Kama hakimu aliweza kumhukumu TID mwaka mmoja jela kwa kupigana, kwa nini hawa MAJAMBAZI wasiswekwe jela kwa wizi wa Tshs 333 million/-?????
Its funny how "Mkono wa Sheria" unavyofanya kazi Tanzania.
 

Ndugu yangu HannibaL; Acha ukabila.
Hata ukiwachukia Wachagga bado Mungu atawabariki tu.
Na fuatilia kama huyu dada Eliaisa amesingiziwa maana alikuwa kazini. Huyu aliyewashtaki ametaka tu kuwakomoa.
 
Ndugu yangu HannibaL; Acha ukabila.
Hata ukiwachukia Wachagga bado Mungu atawabariki tu.
Na fuatilia kama huyu dada Eliaisa amesingiziwa maana alikuwa kazini. Huyu aliyewashtaki ametaka tu kuwakomoa.

Kaka Mswahilina,
Sina ukabila wowote katika hilo suala,ila siwezi kuuunga mkono ujambazi na tamaaa zisizo na msingi. Mara kwa mara nimekuwa nikisoma habari na kuona hawa jamaa zetu(wajomba zangu) wakiwa wanatuhumiwa na kesi nyingi tu za wizi na uporaji. Je ni Ukabila kwa mimi kuuliza kulikoni Je?????

Kusingiziwa sidhani kama ni sahihi.....nafikiri sheria inavyofanya kazi ni lazima kuwe na vigezo sahihi kuweza kufikisha kesi mahakamani.
Tusubiri ushahidi wa muendesha mashitaka na mwanasheria wa mtuhumiwa ...nafikiri ukweli utajulikana tu.

Niwie radhi kama nimekuwa mkabila kwa hilo ndugu yangu.
Nashukuru.
 
hanibal uko wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…