Kejeli na matusi husababisha wanawake wengi wasijitokeze kuwania nafasi za uongozi

Kejeli na matusi husababisha wanawake wengi wasijitokeze kuwania nafasi za uongozi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Mjini,Esther Matiko wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ametaja baadhi ya kasumba zinazokwamisha wanawake kujitokeza kugombea nyadhifa za uongozi kuwa ni kejeli na matusi kwa wanawake.

Mgombea huyo alibainisha jana wakati akizindua mkutano wa kampeni za uchaguzi uliofanyika ndani ya viwanja vya serengeti maarufu kama shamba la Bibi ambao ulihudhuriwa na wagombea mbalimbali akiwemo Esther Bulaya (CHADEMA)kutoka Bunda mjini,Catherine Ruge mgombe ubunge (CHADEMA)jimbo la SerengetiJulius Mtatiro wa Musoma mjini,na John Heche (CHADEMA) mgombe ubunge jimbo la Tarime vijijini.

"Tunahitaji kuwa na kiongozi wa maono ya maendeleo ambaye anashirikiana na wananchi wake kuibua miradi hata kama ni mwanamke au mwanaume haijalishi,wala hatuhitaji kusikiliza kejeli zinazotolewa juu yangu na baadhi ya watu ambao wengine ni viongozi ambapo wakitoa matusi tena hadharani"alisema Matiko.

Miaka yangu mitano nimefanya maendeleo mengi ndani ya jimbo langu kwa kuzingatia,kipaumbele cha Elimu bora Afya bora,Miundombinu pia michezo haikubaki nyuma aliongeza kusema Matiko.

Matiko alitumia nafasi hiyo kusema kuwashukuru Wananchi kumwamini na kumpa kura za kutosha zilizomwezesha kuingia bungeni na kuwaomba tena kumwamini na kumpa kura za kutosha zitakazomwezesha kuingia bungeni na kuwaletea maendeleo ambapo atahakikisha masilahi ya wafanyakazi yana boreshwa,wafanyabiashara pamoja na wakulima.

Kwa upande wake Catherine Ruge mgombea ubunge (CHADEMA)jimbo la Serengeti alisema kuwa mila kandamizi zinazoambatana na matusi na kejeli kwa wakina mama zinapaswa kukemewa na kukomeshwa na jamii nzima kipindi hiki cha sayansi na tekenolojia.(UTANDAWAZI).

Ruge aliongeza kusema kuwa matusi na kejeli kwa wagombea wanawake ni moja ya kikwazo kwa wanawake kinachowakwamisha kujitokeza kugombea nyadhifa mbalimbali za uongozi.

Ukatili wa kijinsia ambao unaendekezwa na baadhi ya makabila humu nchini haupaswi kuwepo unapaswa kukemewa na jamii nzima kwa ujumla kwa kuzingatia kuwa nchi nyingi wamesaini mikataba ya kimataifa ya kupinga ukatili Tanzania ikiwemo.

Mgombea huyo alitumia nafasi hiyo kutuma salamu kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kutenda haki ya kutangaza mgombea yeyote ambaye atakuwa ameaminiwa na wananchi kwa kumpa kura nyingi za kumtosha kutangazwa kuwa mshindi katika eneo ambalo ameomba kuwatumikia siovinginevyo.


Muungwana
 
Back
Top Bottom