Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bangi ni mihadarati na ni kosa ukikamatwa nayo, lakini ni dawa nzuri sana ya kutibu ugonjwa wa masikio.wakubwa nina tatizo la kusikia nakuwa kama kiziwi.
Nimeenda hospital ekanywa nikapewa dawa za miezi miwili lakini sijapata nafuu.
Msaada hata dawa ya kienyeji anayejua ya kutoa kelele masikion.
Hakika maana ishu inaweza kuwa ilikuwa ni upungufu wa hivyo viinilishe tu.Bangi ni mihadarati na ni kosa ukikamatwa nayo, lakini ni dawa nzuri sana ya kutibu ugonjwa wa masikio.
Tafuta bhangi mbichi, pikicha ilainike kuweza kukamua mchuzi.
Na kama ni bhangi kavu, jaza kijiko kikubwa cha bhangi, weka maji yalochemshwa na kupozwa kiasi kidogo, pikicha ili kupata concetration halisi kisha dondoshea tone 1×3 kwa siku, haitachukua muda sikio litaachia.
Unasikia kelele?nimegeuka kiziwi masikio yanalia kama nzi. Msaada wakuu.
Nenda kwa duka la dawa za asili nunua mafuta ya simba.Kwa kuwa yatakuwa yameganda tia kwenye kijiko kisha yapashe moto kwa chini ya kijiko.Halafu changanya na mafuta ya nazi nusu kijiko.Yakishapoa ila kabla hayajaganda tia tone kila sikio.Angalizo yatiwe yakiwa kwenye uvuguvugu usiodhuru ngozi au sikio.Unasikia kelele?
Wewe sio kiziwi.
Kiziwi huwa hasikii kabisa.
Kama uliwahi kuvuta bange na ikakusababishia hilo tatizo, nadhani dawa ni hiyo hiyo bangi. Kuna mtu hapa kakupa formula ya kutengeneza hiyo dawa fuatilia.
Mafuta ya kuku wa kienyeji pia ni dawa kwani yameziba au yana shida gani? Na yameanza lini, unaendesha boda? Una alegi na baridi? Pia mafuta ya kitunguu swaumu au karafuu kama utapata
Yananuka hatari niliwahi kutumiaTafuta mafuta ya kenge,ikiwezekana muue wewe halafu umchune.utayakuta mafuta yameganda kifuani...
Yaweke kwenye kikopo halafu kakitie jikoni kwenye maji ya moto(ili yayeyuke)..
Tafuta nyoya la kuku utakua unachukua mafuta kwa kutumia hilo nyoya unadondoshea sikioni...
Maswali mengine hujayajibu mkuuMie ndiyo nina alegi ya baridi ndiyo kelele haziishi masikioni
Maswali mengine hujayajibu mkuu
Mkuu pole sana kwa maradhi ya masikio kupiga makelele nitafute kwa wakati wako ili niweze kukutibia upate kupona maradhi yako uguwa pole.Wakubwa nina tatizo la kusikia nakuwa kama kiziwi.
Nimeenda hospital ekanywa nikapewa dawa za miezi miwili lakini sijapata nafuu.
Msaada hata dawa ya kienyeji anayejua ya kutoa kelele masikioni.
Mkuu hivi kwa dar mtaalam gani wa audiologists ni mzurihuna tatizo la sikio, una tatizo la mishipa ya neva inayopeleka sauti kwenye akili ili ilete maana, mishipa haifanyi kazi vizuri ndio maana unasikia makelele, unaweza kusikia sauti ya mtu anaongea kwamba ni bezi au sauti laini ila akili inapata shida kutafsiri sauti kuleta maana, hapa muhanga atasema ana nafuu ya kusikia sauti lakini anapata wakati mgumu kuyaelewa maneno.
mafuta ya kuku, mafuta ya kenge, mafuta ya kondoo, maji ya bangi mbichi, kitunguu swaumu, n.k. hizo ni dawa za kutibu sikio linalotoa usaha, kuuma, kuyeyusha wax, n.k. sio dawa ya mishipa ya neva.
hilo tatizo linaitwa tinnitus, kelele zinazosikika kichwani kama mawimbi, filimbi, mivumo, mkwanguo, n.k. hali hii inapelekea na mtu kupungua uwezo wa kusikia.
AINA ZA TINNITUS
1. PRESHA
dalili mojawapo ya presha, mishipa ya sikioni ikifinywa unasikia hizo kelele na kupungua usikivu, nenda hospitalini upime presha, kama unayo watakupa dawa ya kuipunguza, zingatio la muhimu ni kuacha kutumia vilevi kwasababu huwa vinafinya mishipa, kaa mbali na pombe, sigara, bangi, kahawa, n.k. kama huwezi ni kazi bure.
2. KUTUMIA QUININE KUTIBU MALERIA
Wengi ni viziwi tangu wakiwa watoto sababu ya hii dawa, wengine huwa viziwi pamoja na shida ya macho kwa mpigo, quinine huwa inaenda moja kwa moja kufubaza mishipa ya neva ya sikio na hata kwa wengine mishipa ya macho, ndio maana zamani mtu akitumia dawa hii masikio yanaweza kuziba siku 2 mfululizo, tatizo huwa ni pale mtu anavyochomwa sindano ya quinine au kupewa vidonge kuliko kipimo cha kawaida inakuwa ni overdose, huwa wanaanza kupata matatizo ya masikio na wengine macho hata baada ya miaka sita, hawa kutibika inakuwa changamoto kidogo maana muda mrefu umepita, lakini dawa za mishipa ya neva kama neuroton huwa zinasaidia. kaa mbali na vilevi.
3. UPUNGUFU WA VITAMIN B
Wengine ni wale wana upungufu wa vitamin B kana b6 na b12 ambazo ni muhimu kwa afya ya mishipa ya neva, ili kutambua kama upo hili kundi nenda maabatra ya afya kapime viwango vyako vya vitamin b aidha kwa damu au mkojo, ripoti utayopewa itaonesha kama una upungufu wa vitamin b makundi mbali mbali, cheki kama vitamin b6 na b12 zipo chini, kama zipo chini inabidi uiongeze kwa kupigwa sindano, utumie vidonge vya vitamin au kula vyakula vyenye hizo vitamin. kaa mbali na vilevi.
KUFANYA KAZI SEHEMU ZENYE KELELE
Kelele kubwa zikizoeleka kwa muda mrefu, akili inajenga mazoea ya kukaa nazo hata kama haupo eneo la tukio, ndio maana inashauriwa uwe una vaa vifaa vya kupunguza sauti kama upo mazingira ya kelele nzito kwa muda mrefu. kama tatizo limesababishwa hivi inabidi uondoe mazoea yaliyojengwa kwenye akili, unapokuwa sehemu tulivu hasa usiku vaa earphone ama iache redio inacheza muziki laini kwa sauti ya kati tu, hii itasaidia kukandamiza na kuisahaulisha akili yale makelele iliyozoea.