KERO Kelele usiku kucha Mbweni Mpiji-Ungindoni sababu ya vigodoro na pub tumezichoka, tumeripoti serikali za mtaa lakini kazi bure

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Wakuu

Huku Mbweni Mpiji maeneo ya Ungindoni wakiwa na sherehe zao za vigodoro ni kero kubwa, wanakesha usiku kucha na mziki ni mkubwa kiasi kwamba ni changamoto hata kupata usingizi. Mbali na hili ni hatari kwa watoto pia, ukienda kuchungulia mida ya saa tano sita usiku hukosi watoto, kwa watu wazima hamna tabu lakini hawa watoto wanakuwa exposed kwenye mambo ya ajabu sana, waliowahi kuona yanayofanyika huko wakati wa usiku wataelewa ninachosema.

Mbali na hilo, kuna pup ambayo ipo karibu na kanisa, jamani ni balaa, ni kero kwakweli. Kwenye pub wanasema wana kibali cha polisi kukesha. Polisi wanatoa vipi kibali cha watu kukesha kwenye makazi ya watu usiku kucha na hawana sound proof?

Nikaenda kupeleka malalamiko yangu katika ofisi ya serikali ya mtaa wakasema watalishughulikia lakini chochote walichofanya, weekend ni kama sikulala kwa makelele yale. Nadhani kuna rushwa inatolewa ili wafanye sherehe zao mpaka asubuhi, maana hatusikilizwi kabisa.

Soma Pia: Kelele usiku kucha Mtaa wa Alesika, Mbezi Beach kutoka Amigos Pub na Kanisa la Angels Ministry ni kero kubwa, tumechoka!

Sasa pata picha pub inapiga mziki, huku kigodoro kimechanganya, saa saba usiku kuna makelele utafikiri saa sabab mchana. NEMC mje mtupie jicho na huku na uongozi wa serikali ya mtaa uwajibike.
 
Mbwen c tulikubalinaa n ushuwani mkuu,iweje na vigodoro vimeingia uko tenaa..
 
Umewafuata wewe kwao mkuu
 
Huku Mbweni Mpiji maeneo ya Ungindoni wakiwa na sherehe zao za vigodoro ni kero kubwa, wanakesha usiku kucha na mziki ni mkubwa kiasi kwamba ni changamoto hata kupata usingizi....
MBWENI gani?
Hii hii inayopakana na Boko + Bunju, au kuna nyingine?!
 
Una takiwa wewe ndio uhame uko
Huna tofauti na Maasai walio fuata simba ngorongoro
 
Wewe ndio umepeleka kero huko watu walikuwa na utamaduni wao na waliishi nao vizuri sasa umefika unaona ni kero
Sheria zilizowekwa kuhusu kelele zinabagua watu? Kuna wengine hii haiwagusi wanaweza kufanya watakavyo?
 
Nyumba Yako weka alminium huyo hangaika na huo ujinga labda kama unaishi kwenye nyavu watakutesa kweli
 
Mbwen c tulikubalinaa n ushuwani mkuu,iweje na vigodoro vimeingia uko tenaa..
Kuona mtoto wa miaka 15 anaozwa kawaida sana. Kuna kipindi macho yalinitoka.... nilienda kwenye duka la dawa kuchukua dawa, wakati nasubiri kuhudumiwa wakaletwa maharusi kupimwa ukimwi, macho walikuwa watoto ila waliposema umri wao ndio nikachoka kabisa, bwana harusi alikuwa na miaka 16 na bibi harusi miaka 15! walioongozana nao wala walikuwa hawana habari, nikabaki nashangaa tu... ila baada ya kuishi hapo kwa muda nikaelewa, mazingira pia yanachangia
 
Umewafuata wewe kwao mkuu
Nakuuliza kama nilivyomuuliza Mkuu mwingine, kuna watu wana ruhusa ya kupiga kelele usiku kucha kwenye makazi ya watu? Pub inakesha usiku kucha kwamba nihame, kwanini? Dar karibu yote wazaramo na wanaofanana hawakosi kwahivyo wengine ambao hatuna tamaduni za kukesha tuondoke, kuwa serious Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…