Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limebainisha mikakati na hatua mbalimbali zinazochukuliwa katika kukabiliana na changamoto ya uchafuzi wa mazingira utokanayo na kelele za nyumba za ibada.
Akizungumzia kero ya kelele hasa zile zinazosababishwa katika nyumba za ibada, Meneja wa NEMC Kanda ya Kaskazini, Glory Kombe huwa wanapopokea malalamiko kuhusu sauti zilizozidi viwango kutoka kwenye makanisa, hatua ya kwanza ni kuwashirikisha wataalamu kutoka Jumuiya ya Amani na Maridhiano Tanzania, chombo ambacho kiko chini ya Ofisi ya Mambo ya Ndani.
“Kwa pamoja, wataalamu hawa huandaa kikao kinachojumuisha viongozi wa kanisa linalolalamikiwa na wananchi waliotoa malalamiko hayo. Kwenye vikao hivyo, wahusika huelimishwa kuhusu sheria na kanuni za mazingira zinazosimamia viwango vya kelele vinavyoruhusiwa kulingana na maeneo husika, pamoja na adhabu zinazoweza kutolewa kwa wanaokiuka,” amesema.
Pia soma ~ Utitiri wa Makanisa huku Salasala umekuwa kero kwa kelele, utaratibu wa vibali uangaliwe upya
Amesema kuwa elimu inatolewa juu ya mbinu za kudhibiti na kupunguza sauti, ambapo waumini na viongozi huelimishwa kuwa matumizi ya vifaa kama spika yanapaswa kuendana na uhitaji halisi na idadi ya watu.
“Kwa mfano, kanisa lenye waumini watatu pekee ndani ya jengo halihitaji kutumia spika zinazokuza sauti kiasi cha kusikika umbali mrefu. Wanashauriwa pia kutambua jinsi mazingira ya kijiografia, kama vile miinuko, mabonde, na uelekeo wa upepo unavyoweza kusafirisha sauti kwa urahisi zaidi, jambo linaloweza kufanya sauti ndogo ionekane kubwa kwa majirani.
“Viongozi wanahimizwa kutumia wataalamu wa uhandisi wa sauti na vifaa maalum ili kupunguza mwangwi bila kudhuru afya za waumini wao. Ikitokea baadhi ya viongozi wakakaidi na kuendelea na ubishi baada ya hatua hizo, NEMC hulifikisha suala lao kwa Mkuu wa Wilaya, ambaye ndiye msimamizi mkuu wa amani katika eneo hilo, ili achukue hatua Zaidi,” amesema.
Hali ya Kelele Katika Maeneo ya Goba
Kuhusu malalamiko yaliyoibuka katika maeneo ya Goba jijini Dar es Salaam, Kombe amesema NEMC ilichukua hatua mwaka juzi kwa kuandaa semina kubwa kwa wachungaji wa makanisa mbalimbali ya eneo hilo.
“Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi maalum na ilihusisha mtaalamu wa uhandisi wa sauti aliyetoa elimu ya kina juu ya udhibiti wa sauti. Mfano mwingine ni utatuzi wa mgogoro katika Mtaa wa Kinzudi, ambapo NEMC ilisimamia kikao kati ya kanisa lililokuwa linalalamikiwa na wananchi. Katika kikao hicho, kila upande ulielemishwa kuhusu matakwa ya sheria na haki zao, hali iliyosaidia kupata muafaka,” amesema.
Changamoto za Mipango Miji na Usajili
Hata hivyo, alisema NEMC inakabiliwa na vikwazo kadhaa vinavyotokana na changamoto za mipango miji, akisema kuwa makanisa mengi huanzishwa kwenye nyumba za kuishi za watu binafsi ambao hubadilisha matumizi ya majengo hayo.
“Changamoto inakuwa kubwa zaidi kwa sababu kanuni za Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA) za mwaka 2015 zimetoa msamaha kwa nyumba za ibada; hazilazimiki kufanyiwa tathmini hii isipokuwa tu kama zina majengo ya ziada (complex) kama vile shule. Kwa hivyo, udhibiti huu ulipaswa kufanywa kupitia sheria ndogo za manispaa na sheria za ardhi,” amesema.
Ameongeza, “Uusajili wa makanisa unaosimamiwa na Wakuu wa Wilaya mara nyingi una mianya. Watu huanzisha nyumba za ibada kwenye mabaraza ya nyumba zao bila usajili rasmi. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ina wajibu wa kuhakikisha kila kinachoendeshwa kimesajiliwa kihalali, kwani ofisi ya NEMC haiingilii masuala ya usajili au ugawaji wa ardhi bali huingilia kati tu kunapotokea malalamiko ya kelele.”
Adhabu na Utekelezaji wa Sheria
Kuhusu adhabu, Kombe amesema japo Sheria ya mazingira haitofautishi kati ya nyumba za ibada na maeneo mengine; inaruhusu kutoa adhabu za kiutawala (kama vile faini au maonyo) na adhabu za kimahakama.
“Kutokana na unyeti wa masuala ya kiimani, NEMC imepokea maelekezo ya kushughulikia masuala haya kwa tahadhari kubwa. Hadi sasa, taasisi hiyo haijawahi kutoza faini kwa kanisa au msikiti kutokana na uchafuzi wa sauti. Asilimia kubwa ya wahusika wakishapewa elimu ya madhara, huwa tayari kurekebisha hali hiyo na kuwa wasikivu. Kwa wale wachache wanaokaidi, hupelekewa barua za maonyo za kiutawala,” amesema.